Sunday, July 29, 2018

Kikosi cha Yanga fc dhidi ya Gor Mahia leo July 29, 2018

Kikosi cha Yanga dhidi ya Gor Mahia FC kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrewa Vincent
5. Abdalah Shaibu
6. Papy Tshishimbi
7. Yusuph Mhilu
8. Raphael Daudi
9. Matheo Antony
10. Pius Buswita
11. Deus Kaseke

Kikosi cha akiba
12. Benno Kakolanya
13. Haji Mwinyi
14. Said Juma
15. Said Mussa
16. Emmanuel Martin
17. Juma Mahadhi
18. Ibrahim Ajibu

Uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa uliofanywa na Mh Rais wa Tanzania Dr John Magufuri

Na mwandishi wetu
TAARIFA KAMILI YA IKULU JUU YA UTEUZI WA WAKUU WAPYA WA WILAYA NA MIKOA
1. Bw. ALLY SALUM HAPI (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya AMINA MASENZA ambaye amestaafu.
2. Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU ambaye amestaafu.
3. Bw. ALBERT CHALAMILA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Anachukua nafasi ya Bw. AMOS GABRIEL MAKALA ambaye amehamishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu RAPHAEL MUHUGA amestaafu.
4. Brigedia Jenerali NICODEMAS ELIAS MWANGELA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Anachukua nafasi ya Luteni Mstaafu CHIKU GALLAWA ambaye amestaafu.
Wakuu wa Mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.



Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa kama ifuatavyo:
1. Bw. KESSY MADUKA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MADENGE
2. Bw. ABOUBAKAR MUSSA KUNENGE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Bibi THERESIA MMBANDO.
3. Bw. DAVID KAFULILA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
4. Bw. DENIS BANDISA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Anachukua nafasi ya SELESTINE GESIMBA
5. Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Bibi. WAMOJA DICKOLAGWA.
6. Bw. ABDALLAH MOHAMED MALELA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
7. Bw. RASHID KASSIM MCHATA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Anachukua nafasi ya Bw. CHARLES PALLANGYO.
8. Bw. MISSAILE MUSSA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
9. Bi. CAROLINE ALBERT MTHAPULA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MARA.
10. Dkt. JILLY ELIBARIKI MALEKO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi ya ALFRED LUANDA.
11. Bw. CHRISTOPHER DEREK KADIO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Mstaafu CLODWING MTWEVE.
12. Bw. ERIC SHITINDI ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Anachukua nafasi ya BW. JACKSON SAITABAU.
13. Prof. RIZIKI SALAS SHEMDOE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Bw. HASSAN BENDEYEKO.

Makatibu Tawala wa mikoa wafuatao wamehamishwa vituo vyao vya kazi.
1. Bibi REHEMA MADENGE aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa DODOMA, amehamishiwa katika Mkoa wa Lindi.
2. Bibi THERESIA MMBANDO aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa DAR ES SALAAM amehamishiwa katika Mkoa wa Pwani.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kwa baadhi ya Wizara kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. JOSEPH BUCHWESHAIJA kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Anachukua nafasi ya Prof. ELISANTE Ole GABRIEL.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. ANDREW WILSON MASSAWE kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. ELISANTE Ole GABRIEL kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo).
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano)
5. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. EDWIN PAUL MHEDE kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na wengine kuhamishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JERRY CORNEL MURO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. FRANK JAMES MWAISUMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido. Anachukua nafasi ya Bw. DANIEL GEOFREY CHONGOLO.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PATROBAS KATAMBI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi MWANAHAMISI ATHUMAN MUKUNDA kuwa Mkuu wa Wilaya ya BAHI. Anachukua nafasi ya ELIZABETH SIMON KITUNDU.
5. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi Bw. DANIEL GEOFREY CHONGOLO aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido kwenda Wilaya ya Kinondoni.
6. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bibi SARA MSAFIRI ALLY aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwenda Wilaya ya Kigamboni. Anachukua nafasi ya Bw. HASHIM SHAIBU MGANDILWA.
7. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. SAID MKUMBA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Anachukua nafasi ya JOSEPHAT PAULO MAGANGA
8. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bw. JOSEPHAT PAULO MAGANGA na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. Anachukua nafasi ya HERMAN CLEMENT KAPUFI.
9. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali PATRICK NORBERT SONGEA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Anachukua nafasi ya SHAABAN ATHUMAN NTARAMBE.
10. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. RASHID MOHAMED MWAIMU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa. Anachukua nafasi ya Kanali SHABAN ILANGU LISSU
11. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali SIMON M. ANANGE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.
12. Mhe. Rais Magufuli amemteua Luteni Kanali MICHAEL MASALAMA NGAYALINA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe. Anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI.
13. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. LENGAI Ole SABAYA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.
14. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. HASHIM SHAIBU MGANDILWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa. Anachukua nafasi ya Bw. JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI.
15. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ELIZABETH SIMON KITUNDU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati. Anachukua nafasi ya RAYMOND HIERONIMI MUSHI
16. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang. Anachukua nafasi ya SARA MSAFIRI ALLY.
17. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. MARY-PRISKA WINFRED MAHUNDI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MANASE MADUSA.
18. Mhe. Rais Magufuli amemteua Ndg. NGOLLO MALENYA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga. Anachukua nafasi ya Bw. JACOB JOSEPH KASSOMA.
19. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. MOSES JOSEPH MACHALI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
20. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. SEVERIN MATHIAS LALIKA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.
21. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILIS MESHACK NYIMBO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana. Anachukua nafasi ya MARY ONESMO TESHA.
22. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILEMON SENGATI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu. Anachukua nafasi ya HADIJA RASHID NYOMBO.
23. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali LUCAS BONIPHACE MAGEMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe. Anachukua nafasi ya ESTOMIH FRANCIS CHANG’AH.
24. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ZAINAB RASHID MFAUME KAWAWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo. Anachukua nafasi ya Bw. MAJID HEMED MWANGA.
25. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. JOKATE MWEGELO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Anachukua nafasi ya Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM.
26. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. SOPHIA KIZIGO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo. Anachukua nafasi ya Bibi. LUCKINESS ADRIAN AMLIMA.
27. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. JASINTA VENANT MBONEKO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Anachukua nafasi ya JOSEPHINE RABBY MATIRO.
28. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. RAHABU MWAGISA SOLOMON kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
29. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PASACAS MURAGIRI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida. Anachukua nafasi ya ELIAS CHORO JOHN TARIMO.
30. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. KOMANYA ERIC KITWALA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
31. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. KISA KASONGWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

(Orodha imetolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Dar es Salaam)

Sunday, July 22, 2018

Jinsi ya kufuta corrupted files katika computer


Na mwandishi wetu
Hakuna kitu kinachokera kwenye matumizi ya computer kama kupokea ujumbe au sauti kuwa kuna file ime- corrupt kwenye computer yako. Najua wengi sana hatuelewi ni njia gani ya kuweza kutafuta hyo file na mwisho huishia kubadilisha WINDOWS. sometimes kubadilisha windows inakuwa sio solution coz unaweza kubadilisha window na bado ukakutana na tatizo lile lile. Hapa nimekuwekea njia mbili zitakazo weza kukusaidia kutafuta hyo corrupted file na kuweza kufix tatizo lake.

---> KUTUMIA COMMAND
funga program zote na kisha RESTART computer.
wakati tu computer imeanza KU -RESTART bonyeza F8 kwenye keyboard. kama utakavyoona kwenye maelezo kwenye screen. lengo ni kuiingia kwenye SAFE MODE kama utaona option ya SAFE MODE wakati wa kufunguka basi ingia hapo

baada ya kukamilika kufuka kwa SAFE MODE nenda kwenye My Computer kisha right click kwenye Drive ambayo ndio kuna corrupted file (kutokana na ujumbe uliopokea) kisha bonyeza PROPERTIES ya hiyo drive

bonyeza kwenye TOOLS kisha utabonyeza kwenye CHECK NOW (inayopatikana hapo kwenye “Error- checking”).
KUMBUKA: itachukua muda kutafuta kulingana na ukubwa wa hard disk yako

baada ya kumaliza kuscan nenda kwenye START BAR kisha fungua RUN

kwenye RUN dialog utaandika ( sfc/scannow) bila bracket kisha bonyeza
OK
Hii ni sawa na njia ya scan now isipo kuwa hii inaangalia kiundani zaid mpaka zile file ambzo zisingeweza kuonekana na CHECK NOW

baaka ya kumaliza hapo ni kufanya system restore

ingia CONTROL PANEL kisha tafuta sehem ya “Recovery”

bonyeza kwenye “Open System Restore” kisha fuata maelezo hapo itakuwa umemaliza tatizo lilokuwa lina sumbua computer yako




---> KUTUMIA SOFTWARE
Kuna software nyingi zipo ambazo zinaweza kusolve tatizo lako kama hz
- File Cure
- RegCure Registry Cleaner
- PC Tools Spyware Doctor with AntiVirus 2011

Unaweza kuchagua moja kati ya hzo hapo juu fuata maelezo ya kila moja ili kujiridhisha kwenye ufanyi kazi wake



Friday, July 20, 2018

Misingi mitano katika ujasiriamali

Na mwandishi wetu

Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.

Pamoja na biashara kuonekana kuwa kimbilio la wengi sio wote wanaoingia kwenye biashara wanafanikiwa. Tafiti zinaonesha kwamba asilimia tisini ya biashara zinazoanzishwa zinakufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Na hata hizo zinazovuka mwaka mmoja asilimia tisini hufa baada ya miaka mitano. Hivyo kama mwaka huu zimeazishwa biashara mia moja basi miaka mitano ijayo ni biashara moja tu itakayokuwa bado inadumu.

Kwa nini biashara nyingi zinashindwa kudumu?
Biashara nyingi zinakufa kutokana na ukosefu wa elimu muhimu kuhusiana na biashara na ujasiriamali. Watu wengi wanaoingia kwenye biashara wanaingia kwa kuangalia tu ni kitu gani watu wengine wanafanya na wao kufanya hivyo hivyo.
Biashara ni rahisi sana kufanya ila ni ngumu kuendesha na kuikuza mpaka iweze kukupa faida kubwa sana. Ili uweze kuendesha na kukuza biashara itakayokupa faida kubwa ni muhimu kuchukua muda na kujifunza vitu vya muhimu vinavyohusiana na biashara.
Leo tutajifunza misingi mitano muhimu ya biashara ambayo kila biashara inatakiwa kuizingatia. Wewe kama mjasiriamali una jukumu la kujifunza na kufuata misingi hii ili uweze kufikia malengo yako kwenye ujasiriamali na biashara.

Misingi mitano muhimu ya biashara.
Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufata misingi ifuatayo.

Misingi mitano muhimu ya biashara.
Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufuata misingi ifuatayo.

1.Kutengeneza thamani.
Ili biashara iweze kukua na kutengeneza faida ni lazima itengeneze bidhaa au huduma ambayo ni ya thamani kwa wateja. Ni lazima utoe bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji sana ili kuboresha maisha yao. Kama hujaanza biashara fikiria ni kitu gani cha thamani ambacho watu wanakihitaji ila wanakikosa, kisha anza kuwapatia na utajenga biashara kubwa. Kama tayari unafanya biashara angalia ni kitu gani cha thamani unachotoa kwa watu na angalia jinsi unavyoweza kuboresha ili kupata wateja wengi zaidi.

2.Soko.
Kuwa na kitu chenye thamani pekee bado haikutoshi kutengeneza biashara kubwa, ni lazima kuwe na soko linalohitaji bidhaa au huduma hiyo. Hata kama soko lipo bado sio rahisi kwa kila mtu kujua kwamba unatoa huduma muhimu. Hivyo ni muhimu kutafuta soko la biashara yako kwa njia mbalimbali zikiwemo matangazo. Inakubidi uhakikishe watu wanajua uwepo wa biashara yako na utengeneze uteja ili watu waje kupata thamani unayotoa. Kukosa soko la uhakika ni chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.

3.Kuuza.
Ili biashara ikue ni lazima uweze kuuza thamani uliyotengeneza. Ni muhimu uweze kuwashawishi watu wanunue bidhaa au huduma unayotoa. Kuuza ndio moyo wa biashara ambapo kama usipokuwa makini ni rahisi kwa biashara kufa.

4.Kufikisha thamani.
Kama umewaahidi wateja wako kwamba bidhaa ama huduma unayotoa itaboresha maisha yao basi hakikisha hicho ndio kitu kitakachotokea kwa wateja. Ni lazima uweze kufikisha thamani uliyoahidi kwa wateja. Kwa kushindwa kufanya hivi wateja watakuona wewe ni tapeli na hawatanunua tena bidhaa yako. Kama biashara itashindwa kutengeneza wateja wanaojirudia ni lazima itakufa.

5.Fedha.
Usimamizi wa fedha ni muhimu sana kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.

Misingi hii mitano ni muhimu sana kwa biashara. Hakuna msingi ambao unaweza kusema ni muhimu zaidi ya mwingine, yote inategemeana. Ili biashara yoyote iweze kudumu ni muhimu kuzingatia misingi hiyo.

Wednesday, July 4, 2018

Kikosi cha simba sc kitakachoanza dhidi ya singida united katika KAGAME Cup leo July 4, 2018

Na mwandishi wetu
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Singida United, Kombe la CECAFA KAGAME

1. Deo Munishi
2. Nicholas Gyan
3. Jamal Mwambeleko
4. James Kotei
5. Pascal Wawa
6. Mzamiru Yassin
7. Said Ndemla
8. Mwinyi Kazimoto
9. Meddie Kagere
10. Mohamed Rashid
11. Moses Kitandu

Kikosi cha akiba

12. Ally Salim
13. Mohamed Hussein
14. Paul Bukaba
15. Rashid Juma
17. Abdul Hamis
18. Marcel Kaheza
19. Adam Salamba