Saturday, January 12, 2019

Aina ya viungo katika mpira wa miguu

Na Mwandishi wetu
Eneo la kiungo ni moja kati ya maeneo muhimu zaidi ndani ya uwanja. Mara nyingi timu inapokuwa na viungo imara hufanya vizuri pia. Eneo la kiungo ndilo huleta ladha halisi ya soka. Viungo huamua timu icheze vipi, timu ikabe na kushambulia vipi. Eneo la kiungo ni injini ya timu.

Kuna aina nyingi ya viungo. Soka la zamani lilikua na viungo ambao walikua imara zaidi kwenye eneo fulani la kiungo. Ni tofauti na sasa ambapo viungo wengi wanaweza kucheza kwenye aina tofauti tofauti ya kiungo. Mchezaji anayecheza kama holding midfielder anaweza kutumika pia kama deep lying playmaker, central, au defensive midfielder.
Image result for jonas mkude images
Jonas Mkude- Defensive midfielder Simba SC

Hii inatokana na uwepo wa mifumo mingi kwenye soka la sasa, tofauti na zamani ambapo mfumo maarufu ulikua ni 4-4-2. Ifuatayo ni aina tofauti tofauti za viungo.

CENTRAL MIDFIELDER.
Huyu ni kiungo kati. Anapokua uwanjani anapatikana zaidi kwenye eneo la kati ya uwanja. Majukumu yake ya kwanza ni kuichezesha timu. Timu inacheza kupitia yeye, anaweza kuwa na majukumu kiasi ya kusaidia ukabaji na kwenda mbele kusaidia mashambulizi. Typically central midfielder ni Xavi Hernandez. Viungo kama vile Toni Kroos na Ivan Rakitic wanawakilisha central midfielders kwa sasa.

DEFENSIVE MIDFIELDER.
Huyu ni kiungo mkabaji. Kazi yake ya kwanza uwanjani ni kukaba. Mara nyingi kiungo wa aina hii hana majukumu ya kushambulia kama viungo wengine. Kazi yake ya kwanza ni kukaba na kupokonya. Huyu anaweza kuzunguka eneo kubwa la uwanja akihakikisha anautafuta mpira, akiupata anawapa wachezaji wengine watengeneze mashambulizi. Genaro Gattuso, Javier Mascherano, Roy Keane, Patrick Viera na N'Golo Kante ni viungo wanawakilisha kundi la defensive midfielders.

HOLDING MIDFIELDER.
Wakati mwingine anajulikana kama deep lying midfielder. Huyu ni kiungo ambaye huwa hafanyi movements nyingi ndani ya uwanja. Anakaa karibu na mabeki wake. Kazi yake kubwa ni kuzuia mipira na kuichezesha timu akiwa chini. Anaweza asiwe ‘powerful’ kama defensive midfielder lakini ni vyema akawa na jicho zuri la kupiga pasi fupifupi huku akiwa ni mtaalamu pia wa kupiga pasi ndefu kwa uhakika. Xabi Alonso anawakilisha vyema kundi hili.

DEEP LYING PLAYMAKER.
Tofauti yake na deep lying midfielder au holding midfielder ni kwamba, deep lying playmaker focus yake ya kwanza uwanjani ni kuifanya timu iende mbele zaidi. Anaweza asiwe na majukumu makubwa ya kukaba na kuzuia lakini anahakikisha anai-push timu iende mbele. Mara nyingi viungo wa aina hii wanakua na uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mbali zenye uhakika, pasi ya ‘kuhamisha uwanja’. Mfano mzuri ni kiungo mtaalamu Andrea Pirlo. Nchini Italy viungo wa aina hii hujulikana kama “Regista”. Nchini Brazil kama “meia-armador”.

BOX TO BOX MIDFIELDER.
Maana yake ni kwamba, huyu ni kiungo ambaye anauwezo wa kukaba kwenye box la timu yake na kwenda kushambulia kwenye box la timu pinzani. Mara nyingi hawa ni viungo wenye kasi na uwezo mzuri wa kucheza muda mrefu uwanjani bila kuchoka. Kiungo wa aina hii anakua na kazi ya kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja. Mfano mzuri wa kiungo aina hii ni Yaya Toure na Arturo Vidal.

ATTACKING MIDFIELDER.
Huyu ni kiungo mbunifu, mwenye kazi ya kutengeneza mashambulizi. Ni vizuri zaidi kama akicheza nyuma ya viungo wawili. Hapo kazi yake itakua rahisi sana. Wanafahamika kama “trequatista” nchini Italy. Wanaweza kutumika kama ‘secondary strikers’. Mesut Ozil, Kevin De Bruyne, Suso na Ricardo Kaka ni mfano halisi wa attacking midfielders.

WIDE MIDFIELDER.
Mara nyingi viungo wa aina hii hutumika zaidi kwenye mfumo wa 4-3-3. Hawa ni viungo wa pembeni wanaocheza pembeni ya duara la kati, mmoja ‘base’ yake ni upande wa kushoto mwingine kulia. Mara nyingi viungo wa aina hii wanakua na kazi ya kuzuia na kutengeneza mashambulizi pia. Dunia ya sasa haina viungo wa aina hii wengi. Mfano halisi ni Blaise Matuidi. Toni Kroos na Luka Modric kwenye Real Madrid ya hivi karibuni walikua wakicheza kama wide midfielders ambapo base ya Kroos ni upande wa kushoto huku Modric akicheza kulia.

ADVANCED PLAYMAKER.
Hawa hawapatikani sana kwenye soka la sasa. Kiufupi advanced playmaker hucheza ‘shimoni’ nyuma ya mshambuliaji mmoja. Aafahamika kama 'secondary striker' Kutokana na aina ya uchezaji wake, anaweza kutajwa kama mshambuliaji ingawaje si mshambuliaji halisi. Mara nyingi wanakua na uwezo mzuri wa kufunga magoli, kutengeneza magoli, kupiga chenga na kufanya ‘dribbling’. Kwenye soka la zamani hawa walivaa jezi namba 10. Mfano mzuri ni kina Michael Platini, Francisco Totti. Kwa sasa Lionel Messi anawakilisha vyema kundi hili.

WINGER
Huyu ni mshambuliaji wa pembeni. Muda mwingi anautumia akiwa pembeni ya uwanja kulia au kushoto. Ni kiungo mshambuliaji mwenye kasi na mbio. Ana kazi ya kushambulia kutokea pembeni huku akimsaidia ‘fullback’ wake kukaba upande huo huo aliopo. Anaweza kufunga au kupiga krosi nzuri kuja katikati, eneo la box la timu pinzani. Mfumo wa 4-4-2 ndio uliozalishwa wachezaji wa aina hii. Ryan Giggs, Osmane Dembele, Leroy Sane, Luis Nani, Cristiano Ronaldo hasa yule wa Manchester United ni baadhi ya mawinga.

INVERTED WINGER.
Majukumu yake ni sawa ni ‘winger’ wa kawaida. Kinachotofautisha ni kwamba huyu ni mchezaji anayecheza upande wa kulia huku akiwa anatumia mguu wa kushoto, au anacheza upande wa kushoto huku akiwa anatumia mguu wa kulia. Mara nyingi atakimbia pembeni ya uwanja na kuingia ndani ya uwanja. Hakimbii sana pembeni ya uwanja. Arjen Rooben, Eden Hazard, Douglas Costa na Riyad Mahrez ni mfano wa wachezaji aina hii.

FALSE NUMBER 10.
Wakati mwingine anaweza kutambulika kama ‘false number 9’ pia. Kiuhalisi huyu ni kiungo mshambuliaji au winga mwenye uwezo wa kufunga magoli. Anacheza kama mshambuliaji wa kati ingawaje si mshambuliaji halisi. Muda mwingi hakai sehemu moja kusubiri mipira kama ilivyo kwa ‘perfect number 9’. Atazunguka kulia, kushoto na katikati kujaribu kutafuta mipira ili aweze kufunga.

No comments:

Post a Comment