Intel Processor |
Na Adimu Nihuka Jr
Computer nyingi tunazonunua
huwa zinatumia processor za intel au Amd,lakini ni intel ambaye ametawala sana
kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi
processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka
kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa
nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu
kuhusu hii processor? Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer
yako kinachobeba maagizo ya program za computer.
Maagizo hayo yanaweza kuwa ya
kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka. jinsi
processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka
na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina
nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga
processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1.Atom processor
Processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo
kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana
na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor-
Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye
vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium-
Hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa
vikubwa.
4. Core 2 duo-
Hii ni maarufu kwa performance yake ya multitasking, inauwezo
wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3-
Hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake
zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa
wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5-
Ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na
thread, software nyingi
kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri
sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi
multitasking.
7.Core i7-
Hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na
pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa
watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon-
Hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel
lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server.
Unapohost website processor kama
hii ndio inayoprocess webpages. Generation ya processor(muhimu). Ni muhimu sana
kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo
zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye performance kama
zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa
mbuzi kwenye gunia.
Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani
la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth
generation(4xxx) Mfano Intel i3-4130.
Processor yenye namba inayoanziwa
na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130. Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140 Sishauri kabisa
kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second
generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na
third/fourth. Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo
ni;
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila
baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka
kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor
Kama umechunguza mbele ya
processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani
usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je
nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za
desktop.
Bila herufi – hii
inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha
processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor
yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K.
ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha
processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo
dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu
i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi
na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop
ndogo.
S- herufi hii inamaanisha hiyo
proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia
processor kupata joto sana.
Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana
hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha
processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka
desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo.
Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya
desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia
zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi
common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha
processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye
vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia
power ndogo, perfomance yake nayo pia ni
ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata
U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high
perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije
ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi
sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza
game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio
procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore
lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore
kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni
xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya
desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu. Mfano i7-4940MX
No comments:
Post a Comment