Na mwandishi wetu
Je fikra za kununua mipira ya kondomu dukani zinakutia hofu ama aibu? Je unajipata ukinunua karibu kila kitu katika duka la jumla ama lile la dawa ilki ujipatie mipira ya kondomu?
Fikisha app
Sasa kuna suluhu.
Kampuni moja nchini Kenya kwa jina Ad Visions imeanzisha programu tumishi kwa jina 'Fikisha' inayoweza kutumika kununua mipira tofauti ya kondomu na kukuwasilishia pale ulipo.
Kuna baadhi ya watu huwa wanona sana aibu kwenda madukani kununua condom na kuna kipindi huwa wanawatuma watoto wadogo na kuna kipindi wakaamua kuipa majina tofauti tofauti kama vile komando, mipira, n.k hii yote ili kuficha aibu ya kusema neno "condom" mbele ya watu wengi hasa madukani.
Wabunifu wa kenya ndipo wakaja na hiyo program(app) wezeshi ya kuagiza condom kwa njia ya mitandao.
No comments:
Post a Comment