Na mwandishi wetu
Fursa 101 ni mfumo mpya unaowaunganisha wajasiriamali wadogo, wa Kati na hata wakubwa pamoja
Ndani ya fursa 101 kuna fursa zaidi ya 101 tutakazokuwa tunajifunza kila siku ili kwa wale wasio na biashara kabisa wapate nafasi ya Kusimamisha biashara zao.
Zaidi ya hayo fursa 101 tunatumia word of mouth kuunganishana na kuinuana kibiashara kama familia moja.
Kila mkoa una familia ya fursa 101 ambayo Sote ni sehemu ya familia hiyo na tunaweza kupokelewa huko.
Tufahamu kuwa ili tufike mbali tunahitajiana. Huwezi kufanikiwa peke yako. Kupitia Philosophy yetu MIMI NI SABABU YA MAFANIKIO YAKO. WEWE NI SABABU YA MAFANIKIO YANGU i.e Ukitaka kufanikiwa wape nafasi wengine, ukitaka kuuza waweke Karibu wateja wako watarajiwa, waunganishe wengine, wahamasishe wengine.
It's people helping people. Business owners supporting business owners.
Lengo ni kwamba kila mwezi tutakuwa tunakutana. Kila mwanachama Fursa 101 ataonyesha biashara yake. Wanachama wana wajibu wa kuwa Balozi wake. Kumuunganisha na network zao.
Wenye Bidhaa wataonyesha. Wenye Huduma wataelezea.
Watalaamu wa biashara, walimu wote wawepo pamoja, taasisi husika zote ziwepo pamoja.
Hivyo basi kila wanachama wa mkoa wanakutana na kuhamasishana, kujuana, kujenga ukaribu, kuunganishana, kupeana nafasi ya kufanikiwa pamoja. Mwanachama yeyote anaweza kwenda mkoa wowote na kupokelewa Kama mwanafamilia kupitia mabalozi Walio kila mkoa..
Kabla hatujaanza kuchambua fursa mbalimbali lazima tufahamu kuwa fursa ya kwanza ni watu.
Tunataka kupitia fursa 101 kila mwanachama akuze biashara yake. Awe connected na wanachama wote wa mikoa yote TANZANIA nzima. kuanzia sumbawanga mpaka Mwanza, kuanzia Mtwara mpaka Dsm. Kuanzia Arusha mpaka Tanga. Kuanzia Tanzania mpaka kenya, uganda, Rwanda na nchi zote za Afrika. Kumbukeni givers gain. Ukitaka kufanikiwa kibiashara jenga na watu, wakupe biashara, wakupe wateja, wakupe nafasi na ufike mbali. Biashara ni sanaa ya kujenga mahusiano. Kupitia fursa 101 tuwe familia moja na kuunganishana kama ndugu wenye lengo moja, mwelekeo mmoja na imani moja.
Mfahamu kuwa Tanzania nzima inahitaji mfumo huu. Tupo mwanzoni, tunapoangalia mbele tunakoenda wanachama fursa 101 tunaangalia watalaamu watakaoungana nasi, Serikali, taasisi na biashara zitakazozaliwa.
Tutafundishana fursa 101.
Tutatumia tekinolojia kuunganisha watu. Tutajenga mfumo wa mabalozi wa bidhaa or huduma zetu ili kuwezesha wanachama kuuza katika mikoa kupitia mabalozi .
Lengo letu ni moja kujenga mfumo wa umoja, wenye lengo moja, mwelekeo mmoja na kumpa nafasi kila mwenye bidhaa or huduma yake kuuza kwa wengine.
Kupitia fursa 101 tunabadilisha namna ya kufanya biashara Tanzania.
Tutazalisha biashara mpya. Tutazalisha wajasiriamali wapya.
Naomba niwaambie wanachama biashara ni kutokana na watu unaojuana. Wajasiriamali wengi wana bidhaa nzuri, huduma nzuri lakini hakuna mauzo. Hakuna biashara. Why? kwasababu hawajazungukwa na watu potential. Fursa 101 inataka kujenga mfumo unaotuunganisha watu potential, Wateja potential , wanachama wote tukisaidiana na mabalozi wetu kuleta wafanyabiashara na watu potential pamoja na kuwafanya sehemu ya familia Tutafika mbali.
Tutauziana huduma, bidhaa na kupeana fursa zilizo katika kila mkoa. Tutakuwa na trainers, watalaamu wa kilimo, biashara, mauzo, networking, uwekezaji, mitaji, kuuza, business plans, taasisi mbalimbali wanachama, insurance, benki nk.
Katika Kila mikutano ya mwezi kila mwanachama apate nafasi ya kuelezea biashara yake. Huduma yake, bidhaa yake. Kama maonyesho, mafunzo yawepo na watalaamu wa ubora ili tuboreshe bidhaa or huduma zetu. Tunataka kila mtu awe mtu wa watu. Tujenge mahusiano pamoja kupitia biashara zetu. Masomo. Taasisi mbalimbali. Kila mkoa tutaweka target zetu.
Mpaka October 27 siku ya Fursa 101 Forum & Expo kila mkoa uwe na wanachama kuanzia 500.
Wajasiriamali wangapi watazaliwa kupitia mfumo huu?
Biashara ngapi zitakua kupitia mfumo huu?
Nina Imani na wewe. Ninakuamini .
Karibu Fursa 101
Mimi ni Balozi Fursa 101
Mimi ni sababu ya Mafanikio yako.
Fursa 101
No comments:
Post a Comment