Na mwandishi wetu
Ni mfumo wa Matangazo kwa njia ya mtandao unaihusisha matangazo kwenye kurasa za tovuti , programu , blogu , majukwaa na huduma zingine za mawasiliano haswa kwenye mtandao .
Google Adsense ina aina 2 za matangazo kuna yale ya maandishi pekee yaani Text na yanayotembelea kama picha na video yote ni mazuri na yote yana gharama zake .
GOOGLE ADSENSE NA MAISHA YAKO
Kwa kutumia Google Adsense unaweza kupata karibu laki 9 na zaidi kila mwezi na ukasahau kufanya shuguli zingine , Adsense inaweza kufunga Akaunti yako muda wowote au blogu yako muda wowote ule usipozingatia Masharti yao , kwahiyo usitegemee sana ,
GOOGLE ADSENSE INAFANYAJE KAZI
Kama unatovuti yako ukiweka matangazo ya mfumo wa adsense utalipwa kutokana na wingi wa watu wanaitembelea tovuti hiyo na jinsi watu watakavyo gonga click matangazo hayo.
Mfano mrahisi ni Bwana JUMA ana kampuni yake inaitwa MAISHA , badala ya kutengeneza matangazo makubwa kwenye magazeti pamoja na kufungua tovuti ataenda kuongea na google au wawakilishi wa google atatoa tangazo lake atasema jinsi anavyotaka liangaliwe kwa mfano idadi ya nchi au maeneo ndani ya nchi husika , Matangazo ya MAISHA yanaweza kuonekana kwenye blogu ya YONA inayoitwa Naombakazi.com na tovuti nyingi za watu mbalimbali zilizokuwa na huduma za Adsense .
Kwahiyo juma atafaidika kwa tovuti yake kutembelewa na watu wengi kutokana na kutangaza kupitia adsense na watu wanaotembelea NAOMBAKAZI kuona kiunganishi cha tovuti yake.
NOTE > Kufuatilia masharti na maelezo mengine ni muhimu sana kwa mfano unatakiwa usiwaambie watu wagonge matangazo yako waache wa gonge click wenyewe ukifanya hivyo unaweza kufungiwa .
SWALI MUHIMU
Je ukubwa wa Tovuti au Blogu au umaarufu ndio kuongeza kipato cha Adsense ?
Jibu ni hapana utaweza kupata mapato zaidi kutokana na jinsi ulivyoweka matangazo yako na jinsi watu wanavyogonga matangazo hayo hapo ulipoweka kwenye kurasa za tovuti au blogu yako
USAJILI WA GOOGLE ADSENSE UKOJE
Wale wanaotumia huduma za Gmail ambayo ni mali ya Google ni rahisi kujisajili ili kutumia mfumo wa Adsense kwenye blogu na tovuti zao unaweza kutembelea www.google.com/adsense
NOTE>Kila mtu anahaki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kufuatilia malipo yake mwenyewe na kulipwa yeye.
KUKUBALIWA NA PIN NUMBER
Usajili wa Goolge Adsense hauwezi kukamilika kama huna PIN NUMBER na kujaza vitu vingine vya kuthibisha jinsi unavyolipa kodi , kama uko nchi za ulaya kuna namba unatakiwa kuandika ndio utapewa PIN NUMBER .
Kama uki nje ya ulaya kama Tanzania , unaweza kutumiwa PIN NUMBER kutumia DHL ambapo utaingiza namba hiyo kukamilisha mfumo wa usajili au unaweza kuwatumia google kitambulisho au aina nyingine ya utambulisho kuthibitisha uwepo wapo kama kadi ya benki au passport.
NOTE> Bila pin Number hutoweza kutambulika kwenye mfumo wa google adsense na malipo yako hutopatiwa .
MALIPO YA GOOGLE ADSENSE
Google huwa inalipa wenye Adsense kwenye tovuti zao kila mwisho wa mwezi kwa mfumo wa cheki , benki au western Union kutegemea na nchi ambayo mtu yupo , malipo hulipwa pale kunapokuwa na kiasi cha pesa kuanzia dola 100 kwa mwezi ambapo dola 17 hutumika kama gharama za kusafirisha cheki kama uko nchi ambayo wanatuma cheki .
Kwahiyo unavyofanya kazi hii ya matangazo hakikisha unapata hela nyingi zaidi ili uweze kulipa gharama za benki na usafirishaji wa cheki yako , angalau uweze kuwa na dola za kimarekani 700 kila mwezi .
NOTE > Malipo ya kila mwezi hulipwa mwezi unaofuatia kama yalifikia zaidi ya dola 100 za kimarekani
MALIPO YANAVYOTUMWA
Kwa nchi ya Tanzania malipo ya Google Adsene huja kwa njia ya DHL ambapo hufika kila tarehe 2 kila mwezi , malipo yakifika kwenye ofisi za DHL wateja hupigiwa simu na kupelekewa au kama unaweza kufuatilia mwenyewe kutumia tracking number ya DHL kujua kama mzigo umefika au la .
Jambo la kujua ni kwamba watu wengi hufikiri cheki zinatumwa kwa njia za posta za kawaida hapana ni DHL .
UTARATIBU WA KIBENKI
Unatakiwa uwe na Akaunti kwenye benki yoyote Tanzania.
@softwaretz
No comments:
Post a Comment