Na Adimu Nihuka Jr
Facebook na Instagram zinazindua programu mpya itakayodhibiti muda unotumiwa na wateja wao katika programu hizo.
Programu hiyo itapatikana katika ukurasa wa mipango ama settings katika programu zote mbili kupitia kubofya "Your Activity" katika Instagram ama "Your Time katika Facebook"
Tangazo hilo linajiri kufuatia malalamishi kwamba utumizi wa muda mrefu unaweza kuathiri vibaya afya ya akili.
Watumiaji sasa wataweza kuona kiwango cha muda waliotumia katika mitandao hiyo miwili na kujikumbusha muda waliofikia ili kufunga ujumbe wanaopata kwa muda fulani.
''Lakini baadhi ya watu wanasema kuwa haitoshi. Siwezi kusema kuwa ni mabadiliko makubwa ama iwapo itabadilisha mambo mengi kuhusu vile watu wanavyotumia facebook ama Instagram'', alisema Grant Blank kutoka kwa taasisi ya Oxford.
Facebook ilichapisha chapisho la blogi mwezi Disemba 2017 ambalo lilitambua athari mbaya za kutumia mtandao miongoni mwa wateja wake.
Katika jaribio moja , wanafunzi katika chuo kikuu cha Michigan ambao wailoambiwa kuingia katika mitandao yao ya facebook kwa dakika 10 walisalia na hali mbaya mwisho wa siku ikilinganishwa na wale waliotakiwa kuingia mara kwa mara katika mitandao hiyo-wakichapisha ama kuzungumza na marafiki zao.
Uchunguzi mwengine ulibaini kwamba watumiaji wanaoingia katika mitandao hiyo ili kusoma kilichoandikwa mara nne ama hata kupenda machapisho kadhaa waliripotiwa kuwa na matatizo ya kiakili.
Katika kutazama ni muda gani anatumia katika mitandao ya facebook na instagram ,Em ambaye ni Vlogger na mwana-instagram anasema kuwa hajui iwapo itasaidia kwa kuwa najua kwamba natumia sana mitandao ya kijamii.
Lakini hakubaliani kwamba kuwepo kwa kikumbusho cha taarifa zinazoingia kutasaidia.
''Pengine itanifanya kuwacha simu yangu. Iwapo kikumbusho hicho kitajitokeza na kusema kwamba umekuwa ukitumia programu hii kwa saa sita, nitajibu kwa kusema lo! huo ni muda mwingi , nimepoteza muda mwingi sana''.
Harry Hugo mwanzilishi mwenza wa kampuni ya kidijitali , The Goat Agency anasema kuwa mabadiliko hayo yalisubiriwa kwa muda mrefu.
"Huku kukiwa na maswala ya kuathirika kiakili-hususan miongoni mwa vijana, ambao wanatumia muda wao mwingi katika mitandao- ni muhimu kwamba tunafaa kuweka vitu vinavyoweza kudhibiti mitandao ya kijamii.
Iwapo wanaelewa kwamba wanatumia saa nyingi katika mitandao hiyo, pengine itawafanya kufikiria mara mbili.
Harry anasema kwamba alikuwa akitumia twitter kwa saa 15 na 16 kwa siku wakati alipokuwa kijana-lakini anaamini kwamba mojawapo ya vidhibiti hivyo ni kujizuia.
''Ni sisi tunaofungua simu , ni sisi tunaofungua programu ya instagram. hatuwezi kusema kwamba Apple ama facebook ndio itakayotusaidia kutatua tatizo hilo''.
''Ni kweli programu hizo zinaweza kutumiwa kutudhibiti lakini hazitafanya mabadiliko hayo kabisa kabisa''.
Kutoka BBC Swahili
No comments:
Post a Comment