Tuesday, August 14, 2018

Kuna tofauti gani kati ya mavazi ya hijab, niqab na burka?

Hijab, niqab, burka kuna aina mbalimbali za mavazi ya kujifunika yanayovaliwa na wanawake wa kiislamu duniani.
Lakini si kila mtu hukubaliana navyo, na nchini Denmark, ulaya, marufuku ya kuvaa ushungi wenye kufunika uso ilianza kufanya kazi tarehe 1 mwezi Agosti
Denmark imeungana na Ufaransa na mataifa mengine baadhi ya Ulaya kupitisha amri hiyo.Waziri wa sheria wa Denmark Søren Pape Poulsen amesema ni lazima tuangalie. ishara ya uso wa kila mmoja wetu.
Mwanamke akiwa amevaa Chador
Mwanamke amevalia Chador
Wanawake wengine huvaa vilemba kufunika kichwa na nywele, huku wengine wakivaa burka au niqab, ambayo pia inafunika uso wao.
Hizi ni aina mbali mbali za mavazi ya ushungi
HIJAB
Neno Hijab linaeleza kitendo cha kujifunika kwa ujumla.Vazi hili huvaliwa na wanawake wa kiislamu.Vilemba hivi vinakuwa vya mitindo na rangi mbalimbali.Mara nyingi aina hii huvaliwa ikifunika kichwa na shingo lakini uso huwa wazi.
NIQAB

Niqab ni ushungi kwa ajili ya kufunika uso maeneo ya kuzunguka macho huwa yanaonekana,huvaliwa sambamba na kitambaa cha kichwani
BURKA

Burka ni ushungi unaofunika uso na mwili, mara nyingi huacha nafasi machoni kidogo kwa ajili ya kuona.
AL- AMIRA
Al-amira ni ushungi wa vipande viwili vikiwa vinavaliwa na kitambaa mithili ya kofia cha aina ya pamba au polista.
SHAYLA
Shayla ni vazi refu,lenye umbo la mstatili maarufu katika maeneo ya Ghuba.Huzungushiwa kuzunguka kichwa kisha kubanwa na pini na kuegeshwa mabegani.
KHIMAR
Khimar ni ushungi ambao huning'inia mpaka usawa wa juu ya kiuno.Hufunika nywele, shingo na mabega kabisa lakini uso huonekana vizuri.
CHADOR
Chador huvaliwa na wanawake wa Iran wanapokuwa nje ya nyumba, ni vazi la kufunika mwili mzima.Mara zote huvaliwa na kilemba kichwani kwa ndani

         Kutoka BBC Swahili

No comments:

Post a Comment