Saturday, January 12, 2019

Aina ya viungo katika mpira wa miguu

Na Mwandishi wetu
Eneo la kiungo ni moja kati ya maeneo muhimu zaidi ndani ya uwanja. Mara nyingi timu inapokuwa na viungo imara hufanya vizuri pia. Eneo la kiungo ndilo huleta ladha halisi ya soka. Viungo huamua timu icheze vipi, timu ikabe na kushambulia vipi. Eneo la kiungo ni injini ya timu.

Kuna aina nyingi ya viungo. Soka la zamani lilikua na viungo ambao walikua imara zaidi kwenye eneo fulani la kiungo. Ni tofauti na sasa ambapo viungo wengi wanaweza kucheza kwenye aina tofauti tofauti ya kiungo. Mchezaji anayecheza kama holding midfielder anaweza kutumika pia kama deep lying playmaker, central, au defensive midfielder.
Image result for jonas mkude images
Jonas Mkude- Defensive midfielder Simba SC

Hii inatokana na uwepo wa mifumo mingi kwenye soka la sasa, tofauti na zamani ambapo mfumo maarufu ulikua ni 4-4-2. Ifuatayo ni aina tofauti tofauti za viungo.

CENTRAL MIDFIELDER.
Huyu ni kiungo kati. Anapokua uwanjani anapatikana zaidi kwenye eneo la kati ya uwanja. Majukumu yake ya kwanza ni kuichezesha timu. Timu inacheza kupitia yeye, anaweza kuwa na majukumu kiasi ya kusaidia ukabaji na kwenda mbele kusaidia mashambulizi. Typically central midfielder ni Xavi Hernandez. Viungo kama vile Toni Kroos na Ivan Rakitic wanawakilisha central midfielders kwa sasa.

DEFENSIVE MIDFIELDER.
Huyu ni kiungo mkabaji. Kazi yake ya kwanza uwanjani ni kukaba. Mara nyingi kiungo wa aina hii hana majukumu ya kushambulia kama viungo wengine. Kazi yake ya kwanza ni kukaba na kupokonya. Huyu anaweza kuzunguka eneo kubwa la uwanja akihakikisha anautafuta mpira, akiupata anawapa wachezaji wengine watengeneze mashambulizi. Genaro Gattuso, Javier Mascherano, Roy Keane, Patrick Viera na N'Golo Kante ni viungo wanawakilisha kundi la defensive midfielders.

HOLDING MIDFIELDER.
Wakati mwingine anajulikana kama deep lying midfielder. Huyu ni kiungo ambaye huwa hafanyi movements nyingi ndani ya uwanja. Anakaa karibu na mabeki wake. Kazi yake kubwa ni kuzuia mipira na kuichezesha timu akiwa chini. Anaweza asiwe ‘powerful’ kama defensive midfielder lakini ni vyema akawa na jicho zuri la kupiga pasi fupifupi huku akiwa ni mtaalamu pia wa kupiga pasi ndefu kwa uhakika. Xabi Alonso anawakilisha vyema kundi hili.

DEEP LYING PLAYMAKER.
Tofauti yake na deep lying midfielder au holding midfielder ni kwamba, deep lying playmaker focus yake ya kwanza uwanjani ni kuifanya timu iende mbele zaidi. Anaweza asiwe na majukumu makubwa ya kukaba na kuzuia lakini anahakikisha anai-push timu iende mbele. Mara nyingi viungo wa aina hii wanakua na uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mbali zenye uhakika, pasi ya ‘kuhamisha uwanja’. Mfano mzuri ni kiungo mtaalamu Andrea Pirlo. Nchini Italy viungo wa aina hii hujulikana kama “Regista”. Nchini Brazil kama “meia-armador”.

BOX TO BOX MIDFIELDER.
Maana yake ni kwamba, huyu ni kiungo ambaye anauwezo wa kukaba kwenye box la timu yake na kwenda kushambulia kwenye box la timu pinzani. Mara nyingi hawa ni viungo wenye kasi na uwezo mzuri wa kucheza muda mrefu uwanjani bila kuchoka. Kiungo wa aina hii anakua na kazi ya kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja. Mfano mzuri wa kiungo aina hii ni Yaya Toure na Arturo Vidal.

ATTACKING MIDFIELDER.
Huyu ni kiungo mbunifu, mwenye kazi ya kutengeneza mashambulizi. Ni vizuri zaidi kama akicheza nyuma ya viungo wawili. Hapo kazi yake itakua rahisi sana. Wanafahamika kama “trequatista” nchini Italy. Wanaweza kutumika kama ‘secondary strikers’. Mesut Ozil, Kevin De Bruyne, Suso na Ricardo Kaka ni mfano halisi wa attacking midfielders.

WIDE MIDFIELDER.
Mara nyingi viungo wa aina hii hutumika zaidi kwenye mfumo wa 4-3-3. Hawa ni viungo wa pembeni wanaocheza pembeni ya duara la kati, mmoja ‘base’ yake ni upande wa kushoto mwingine kulia. Mara nyingi viungo wa aina hii wanakua na kazi ya kuzuia na kutengeneza mashambulizi pia. Dunia ya sasa haina viungo wa aina hii wengi. Mfano halisi ni Blaise Matuidi. Toni Kroos na Luka Modric kwenye Real Madrid ya hivi karibuni walikua wakicheza kama wide midfielders ambapo base ya Kroos ni upande wa kushoto huku Modric akicheza kulia.

ADVANCED PLAYMAKER.
Hawa hawapatikani sana kwenye soka la sasa. Kiufupi advanced playmaker hucheza ‘shimoni’ nyuma ya mshambuliaji mmoja. Aafahamika kama 'secondary striker' Kutokana na aina ya uchezaji wake, anaweza kutajwa kama mshambuliaji ingawaje si mshambuliaji halisi. Mara nyingi wanakua na uwezo mzuri wa kufunga magoli, kutengeneza magoli, kupiga chenga na kufanya ‘dribbling’. Kwenye soka la zamani hawa walivaa jezi namba 10. Mfano mzuri ni kina Michael Platini, Francisco Totti. Kwa sasa Lionel Messi anawakilisha vyema kundi hili.

WINGER
Huyu ni mshambuliaji wa pembeni. Muda mwingi anautumia akiwa pembeni ya uwanja kulia au kushoto. Ni kiungo mshambuliaji mwenye kasi na mbio. Ana kazi ya kushambulia kutokea pembeni huku akimsaidia ‘fullback’ wake kukaba upande huo huo aliopo. Anaweza kufunga au kupiga krosi nzuri kuja katikati, eneo la box la timu pinzani. Mfumo wa 4-4-2 ndio uliozalishwa wachezaji wa aina hii. Ryan Giggs, Osmane Dembele, Leroy Sane, Luis Nani, Cristiano Ronaldo hasa yule wa Manchester United ni baadhi ya mawinga.

INVERTED WINGER.
Majukumu yake ni sawa ni ‘winger’ wa kawaida. Kinachotofautisha ni kwamba huyu ni mchezaji anayecheza upande wa kulia huku akiwa anatumia mguu wa kushoto, au anacheza upande wa kushoto huku akiwa anatumia mguu wa kulia. Mara nyingi atakimbia pembeni ya uwanja na kuingia ndani ya uwanja. Hakimbii sana pembeni ya uwanja. Arjen Rooben, Eden Hazard, Douglas Costa na Riyad Mahrez ni mfano wa wachezaji aina hii.

FALSE NUMBER 10.
Wakati mwingine anaweza kutambulika kama ‘false number 9’ pia. Kiuhalisi huyu ni kiungo mshambuliaji au winga mwenye uwezo wa kufunga magoli. Anacheza kama mshambuliaji wa kati ingawaje si mshambuliaji halisi. Muda mwingi hakai sehemu moja kusubiri mipira kama ilivyo kwa ‘perfect number 9’. Atazunguka kulia, kushoto na katikati kujaribu kutafuta mipira ili aweze kufunga.

Thursday, December 20, 2018

Fahamu muongozo wa kununua computer kwa kuangalia Processor


Image result for intel processor images
Intel Processor
Na Adimu Nihuka Jr
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au Amd,lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor? Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer.

Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka. jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi

Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1.Atom processor
Processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor-
Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium-
Hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo-
Hii ni maarufu kwa performance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3-
Hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5-
Ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi
kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7-
Hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon-
Hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server.

Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages. Generation ya processor(muhimu). Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye performance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx) Mfano Intel i3-4130.

Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130. Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)

Mfano i3-2140 Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth. Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni;
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana.
Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni
ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu. Mfano i7-4940MX



Sunday, December 16, 2018

Tatizo la nguvu za kiume

Na Mwandishi wetu
BASI LEO LIFAHAMU TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA CHANZO CHAKE

Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote. Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake.

Kuna sababu nyingi mno zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume. Mtu aweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo?

NGUVU ZA KIUME NI NINI?

Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na:
~ Hamu ya mapenzi,
~Kusimama kwa uume barabara,
~ Kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa,
~ Uwezo wa kurudia tendo la ndoa,
~ Pumzi,
~ Wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo lenyewe.

NI VIUNGO GANI VINAHUSIKA NA NGUVU ZA KIUME?

Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni:
#Ubongo,
#moyo,
#mishipayaneva
#mishipayaateri,
#mirijailiyondaniyauume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni:
#neva maalumu za parasympathetic,
#tezidume (prostate gland),
#ini,
#figo,
#Homoni ya testestorone,
#Kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine,
#utiwamgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga. Pia vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor,
#tezipituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao #tunicaalbuginea, misuli iitwayopubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.
Nadhani unaona jinsi ilivyo vitu vingi.

NINI MAANA YA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME?

Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapnzi,

2. Uumme kusimama kwa uregevu; au

3. Kuwahi kufika kileleni; au

4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa); au

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa; au

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo; au

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji; au

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Yapo maradhi kadhaa, mitindo ya maisha, na  vyakula tunavyokula ambavyo vinapelekea viungo tajwa kutofanya kazi vizuri. Baadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation) kwa muda mrefu; kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Hata hivyo kuna vitu unaweza kufanya ili kurejesha nguvu zako za kiume.

Uume wako unatakiwa usimame kwenda juu na siyo usimame kwenda mbele tu au kurudi chini. Na ukisimama kwenda juu uwe umenyooka usiwe umejikunja kama ndizi hapana maana hilo ni tatizo uume wa hivyo una kitu kinaaitwa plaque... ni mafuta yamegandana na kuufanya ukisimama unakuwa kama na ulemavu fulani hivi. Usidharau tu.

Wengi hata hawaijui miili yao vizuri. Na hasa kwenye suala hili la NguvuZaKiume. Wengi hawafatilii wanaona aibu kumbe wanalea tatizo ambalo soon linaweza kuwaathiri zaidi!

Machache kati ya yaliyo mengi ni hayo. Ili kujua zaid afya ya uzazi na kupata elimu bure tembelea page yetu #fahariyamwanaume.

Pamoja na hayo yoote na dalili hapo juu, unatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.
Wasiliana nasi kwa namba:
 +255752083947,
+255658259125 au
Click https://wa.me/+255738479968

TUTAKUSAIDIA KUJITAMBUA, KUKUPA ELIMU BURE NA MBINU ZA KUONDOKANA NA MATATIZO YAHUSUYO NGUVU ZA KIUME IKIWA NI PAAMOJA NA KUPEWA TIBA LISHE/TIBA VIRUTUBISHO.

SHARE NA UNAOWAPENDA ELIMU HII YA BURE

Saturday, December 15, 2018

Maajabu ya Roboti huko nchini Urusi

Na Mwandishi wetu
Roboti moja iliyokuwa kwenye tamasha la maonesho yaliyofadhiliwa na taifa ilishangaza wengi kwa uwezo wake wa juu.
Vazi la Roboti likivutia umati mkubwa wa watu
Roboti mithiri ya mwanadamu huko urusi
Roboti Boris aliyeonyeshwa katika kipindi cha runinga nchini humo, alionesha uwezo mkubwa wa kutembea, kuongea na kucheza dansi.
Lakini muda mfupi baadaye, waandishi habari wakahoji uwezo mkubwa wa roboti hiyo.
Katika picha ambayo ilichapishwa baadaye kwenye mitandao ya kijamii, shingo ya binadamu, ilionekana bayana.
Loh, ukweli ukabainika kuwa halikuwa roboti bali mtu aliyevalia magwanda ya plastiki tu.
Vazi hilo liitwalo Alyosha the Robot, lililoundwa na kampuni iitwayo Show Robots na linagharimu dola 2,975.
Huku waandalizi wa tamasha la teknolojia ya Proyektoria - wakiwalenga vijana chipukizi katika maonyesha hayo, wakiwa bado hawajatangaza kuwa kwa hakika hilo lilikuwa Roboti- matangazo ya runinga ya Russia-24, yalitangaza kuwa ni roboti halisi.
Tovuti ya mtandao wa TJournal nchini Urusi, ndio iliyokuwa ya kwanza kushuku iwapo hiyo ilikuwa ni roboti halisi au la....ikiuliza maswali chungu nzima ikiwemo:
  • Ni kwa nini muundo wa roboti hiyo haina vifaa vya kutuma na kupokea ujumbe maarufu kama sensors?
  • Jinsi gani wanasayansi wa Urusi walifaulu kuunda roboti haraka hivyo, huku kukiwa hakuna taarifa au ripoti zozote zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na maandalizi ya uundaji.
  • Je, mbona hakuna taarifa zozote za utalamu huo wa kisasa kwenye mitandao ya kijamii?
  • Mbona roboti ilikuwa ikifanya ishara nyingi pale lipokuwa ikicheza muziki?
  • Kwanini ilikuwa na umbo ambalo binadamu anaweza kuingia ndani na kutoshea barabara?
  • Kwanini sauti yake ilikuwa imerekodiwa badala ya kutoa sauti moja kwa moja mbele ya umati?
Katika tovuti ya kampuni hiyo iliyounda vazi hilo la Alyosha Robot, bidhaa hiyo inaelezewa kama iliyo na uwezo "sawa kabisa na roboti halisi".

KUTOKA BBC SWAHILI

Fikisha App: Programu tumishi inayokuletea kondomu ulipo nchini Kenya

Na mwandishi wetu
Je fikra za kununua mipira ya kondomu dukani zinakutia hofu ama aibu? Je unajipata ukinunua karibu kila kitu katika duka la jumla ama lile la dawa ilki ujipatie mipira ya kondomu?

Image result for fikisha app image
Fikisha app 

Sasa kuna suluhu.
Kampuni moja nchini Kenya kwa jina Ad Visions imeanzisha programu tumishi kwa jina 'Fikisha' inayoweza kutumika kununua mipira tofauti ya kondomu na kukuwasilishia pale ulipo.

Kuna baadhi ya watu huwa wanona sana aibu kwenda madukani kununua condom na kuna kipindi huwa wanawatuma watoto wadogo na kuna kipindi wakaamua kuipa majina tofauti tofauti kama vile komando, mipira, n.k hii yote ili kuficha aibu ya kusema neno "condom" mbele ya watu wengi hasa madukani. 

Wabunifu wa kenya ndipo wakaja na hiyo program(app) wezeshi ya kuagiza condom kwa njia ya mitandao.

Wednesday, December 12, 2018

Tofauti kati ya modem, switch, hub na Router katika Networking

Na Adimu Nihuka Jr
Watu wengi sana hushindwa kutofautisha kazi au matumizi ya vifaa vya network, kwa mfano juu ya matumizi ya Router na Switch au utofauti wa Hub na Switch.

 Nimekuwekea post hii ili uweze kuwa makini kutofautisha vifaa hivyo na kujua matumizi yake.
Vifaa vya mtandao wa Kompyuta ni units ambazo hupatanisha data katika mtandao wa kompyuta na pia vinaitwa vifaa vya mtandao. Units ambazo zinapokea data au kuzalisha data zinaitwa hosts au data terminal equipment.

Hub Network:
Hub Network ni kifaa cha mtandao ambacho hutumika ku connect Multiple network hosts. Network hub pia hutumika kusafirisha data. Data husafirishwa kwa mfumo wa packets kwenye Computer network. Hivyo wakati host inatuma data packet kwenye network hub, hub ina copy data packet kwenye port zake zote zilizokuwa connected. Ports zote zinajua kuhusu data na port inatambua ni wapi data inatoka.
Hata hivyo kwa sababu ya utaratibu wake wa kufanya kazi, Hub haipo na ulinzi wa kutoka (not secure and safe) Aidha ina copy data packets kwenye interface zote or port na kufanya iwe slow na kufanya msongamano ambao unasababisha matumizi ya mtandao kubadili. Hivyo basi zinapotumwa data packet nyingi zaidi kwa wakati mmoja hub huwa inashindwa ku control na kufanya ifanye kazi yake kwa taratibu na hata kusababisha kuharibika kwa data packet zingine. Lakini switch anauwezo wa kuyakabili hayo yote.

Network Switch
Network Switch ni kama hub, Sitch pia inafanya kazi katika safu ya LAN(local Area Network) lakini unaweza kusema kwamba Swich ina akiri kuliko hub. Wakati hub inafanya kazi ya usambazaji data, Swich pia anafanya hivyo na pia ana filter na kusambaza kiakili zaidi kwa kudeal na data packet.
Hivyo, wakati packet inapokewa kwenye interface ya swich, ina filters packet na kutuma kwenye interface husika iliyopokea. Kwa lengo hili, Switch pia ina maintains CAM(Content Addressable Memory) table na ina system ya Configuration and memory yake yenyewe. Kwahiyo hata kama zitatumwa data packet nyingi kwa wakati mmoja Switch anatambua kila interface ya packet iliyotumwa na kurudisha kwenye interface iliyotumika kwa haraka bila kuchanganya wala kuharibu packet data (swich is more intelligent than Hub)

Modem
Modem ni kifaa ambacho huwa tunakitumia mara kwa mara kwene maisha yetu ya kila siku. Hivyo kama unataka kupata internet connection kupitia waya (Kuna aina tofauti ya waya) nyumbani kwako. Waya hutumika kubeba internet data nje ya dunia ya internet.
Hata hivyo, Kompyuta zetu zinazalisha data binary au data digital katika aina ya 1s na sekunde 0 na kwa upande mwingine. Waya hubeba Analog na hapo ndipo modem inapotumika.
Modem inasimama kwa(moduleta + QAM). Hiyo ina maana modulates na demodulates ishara kati ya digital data ya kompyuta na analogue signa ya telephone line.

Network Router
Router ni kifaa cha mtandao ambacho kinajukumu la kuendesha traffic kutoka mtandao mmoja hadi mwingine. Mitandao hii miwili inaweza kuwa kampuni binafsi na umma. Unaweza kufikiri router kama polisi wa usalama barabarani ambaye anaongoza traffic tofauti za mtandao kwa mwelekeo tofauti.
Router inafanya kazi ya kuunganisha LAN moja na LAN nyingine.
Image result for image of router
Router

Bridge
Kama router inaunganisha aina mbili tofauti ya mitandao, ni kama daraja ambalo linaunganisha sehemu mbili tofauti kwenye mtandao. Bridge hutumika kuunganisha sehemu mbili tofauti kwa mfano, maxmum length ya UTP Cable ni mita 100, zaidi ya hapo inabidi itumike bridge ili kuunganisha wire huo ili network ipatikane kiurahisi.

Repeater
Repeater ni kama kifaa cha electronic kwamba kina amplify sinal zinazopokea.

 Katika maneno mengine, unaweza kufikiri repeater kama kifaa ambacho kinapokea mawimbi na kuyapokeza katika ngazi ya juu au nguvu ya juu ili mawimbi yaweze kufunika umbali mrefu.

Thursday, September 6, 2018

Madhara yatokayo na uvaaji wa nguo za mitumba

Picha katika soko la mtumba Ilala
Baadhi ya nguo za mitumba

Na Mwandishi wetu.
Ninapo taja masoko makubwa ya nguo za ndani za mitumba, hapa nazungumzia Mwenge, Ilala, Tandika na hata Manzese.
Wanawake ndio watumiaji wa kubwa kwani kwa upande wa wanaume nguo zao kubwa za ndani ni kaoshi, soksi na taiti.
Lakini kwa upande wa wanaweke hupendelea zaidi kutumia sidiria, nguo za kulalia, taiti na hata chupi.
Nguo hizi za ndani za mtumba, hupendwa zaidi kwasababu baadhi husema ni imara na zina dumu lakini pia hupatikana kwa bei raisi sana, zingine huuzwa miatano au elfu moja na zipo za mpaka elfu kumi na zote ni za mtumba.
amoja na urahisi huo, watumiaji wanafahamu nini juu ya madhara ya kuvaa nguo hizi za ndani zilizo valiwa na watu wengine ambao hatuwajui? Hatujui afya zao na wala magonjwa ambayo huenda wanayo.
BBC imezungumza na baadhi ya watumiaji wa nguo hizo za ndani baadhi wanaonyesha kuto jua lolote kama yanaweza kuwepo madhara.
"Mi hayo madhara hata siyajui ila napata zangu nguo kwa bei poa na napendeza kama kawaida. Kama kuna madhara haya," anasema bi Aisha wa soko la karume".
Hata hivyo Ally Saleh mtumiaji wa nguo za ndani za mitumba anasema yeye huangalia zilizo mpya mpya.
"Mimi huwa nachukua ule mtumba wa grade A na zangu zinakuwa mpya mpya hazijatumika sana, ila kuhusu madhala labda zile zilizo chakaa kupita kiasi. Mie singlendi zangu ata boksa napata kali mtumbani," Ally anaiambia BBC.
Wengine wanafurahia ubora hali inayopelekea kufumbia macho juu ya elimu waliyo nayo.
"Mie naambiwa tu kwamba zina madhara lakini ukiziona zinaonekana bora na nzuri kuliko za dukani yaani ukivaa sidiria ya dukani inafanya matiti yanakuwa mama ni bebe, wakati ya mtumba kwa raha zangu kitu talk to me inakamata muruaa," Nola Almasi anaiambia BBC.
Hata hivyo kumekuwa na maoni mbali mbali juu ya madhara ya nguo za ndani za mitumba wengine husema zinaleta saratani, fangasi na baadhi huamini zinaharibu kizazi. Pamoja na yote yasemwayo baadhi yetu hufumbia macho na huamini kuwa ni propaganda za ushindani wa kibiashara.
Hata hivyo katika nguo hizo za ndani za mitumba zipo nyingi ambazo hazijatengenezwa kwa mali ghafi ya pamba, zimetengenezwa kwa polyista malighafi ambayo hainyonyi maji. Hali inayopelekea baadhi kupatwa na muwasho sehemu za siri.
Daktari Fredrick Mashili wa hospitali ya taifa Muhimbili ili kufahamu zaidi juu ya ukweli wa madhara ya nguo za ndani za mitumba.
"Kunakuwa na uwezekano wa kuwepo madhara kiafya na mara nyingi ni matatizo ya ngozi zaidi ndo yanaweza kusababishwa na hizo nguo, kutokana na ukweli kwamba huenda aliyekuwa anazitumia hizo nguo anatatizo flani la ngozi.
Kwa mfano ukiongelea vitu kama fangasi ambavyo vinauwezo wa kukaa kwenye mazingira magumu na kuishi kwa muda mrefu sana, kwa maana hiyo hata kama zilikuwa zimesafirishwa kwa muda fulanikwenye hali ya ukavu na nini bado kunakuwa na uwezekano wa kuwepo kwa vimelea au vitu fulani ambavyo ni sehemu ya fangasi ambavyo baadae mtu mwingine akivaa anauwezo wa kupata hilo tatizo," Daktari Mashili anaiambia BBC.
Hata hivyo daktari huyo anasisitiza kuwa upo uwezekano wa kuwepo kwa magojwa mengine ya ngozi ambayo haya sababishwi na fangasi na hii inategemea ni muda gani tangu nguo hizo zimetoka kwa mtumiaji wa awali na kuanza kutumiwa na mtumiaji wa sasa.
Daktari Mashili amesisitiza kuwa, kama kuna ulazima wa kuzitumia nguo za ndani za mitumba ni vyema mtu akazisafisha na dawa zile kali ambazo zinaweza kusaidia kuuwa viji dudu kuliko kufua tu kawaida na kisha kuivaa.
Tangu mwaka 2009, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), lilipiga marufuku uuzaji wa nguo za ndani za mitumba na kutoa kipindi cha ukomo kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo. Baada ya kipindi cha mpito kuisha, TBS walifanya maamuzi ya kukamata na kuchoma nguo hizo za ndani za mitumba ili kutekeleza agizo la sheria ya mwaka 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani zilizokwishatumika.
Hata hivyo harakati hizo hazikufua dafu kwani mpaka sasa nguo za mitumba bado zipo katika takribani kila soko la nguo za mitumba Tanzania.

Kutoka BBC Swahili

Monday, September 3, 2018

Fursa 101 ni nini?

Na mwandishi wetu
Fursa 101 ni mfumo mpya unaowaunganisha wajasiriamali wadogo, wa Kati na hata wakubwa pamoja

Ndani ya fursa 101 kuna fursa zaidi ya 101 tutakazokuwa tunajifunza kila siku ili kwa wale wasio na biashara kabisa wapate nafasi ya Kusimamisha biashara zao.

Zaidi ya hayo fursa 101 tunatumia word of mouth kuunganishana na kuinuana kibiashara kama familia moja.

Kila mkoa una familia ya fursa 101 ambayo Sote ni sehemu ya familia hiyo na tunaweza kupokelewa huko.

Tufahamu kuwa ili tufike mbali tunahitajiana. Huwezi kufanikiwa peke yako. Kupitia Philosophy yetu MIMI NI SABABU YA MAFANIKIO YAKO. WEWE NI SABABU YA MAFANIKIO YANGU i.e Ukitaka kufanikiwa wape nafasi wengine, ukitaka kuuza waweke Karibu wateja wako watarajiwa, waunganishe wengine, wahamasishe wengine.
It's people helping people. Business owners supporting business owners.

Lengo ni kwamba kila mwezi tutakuwa tunakutana. Kila mwanachama Fursa 101 ataonyesha biashara yake. Wanachama wana wajibu wa kuwa Balozi wake. Kumuunganisha na network zao.
Wenye Bidhaa wataonyesha. Wenye Huduma wataelezea.

Watalaamu wa biashara, walimu wote wawepo pamoja, taasisi husika zote ziwepo pamoja.

Hivyo basi kila wanachama wa mkoa wanakutana na kuhamasishana, kujuana, kujenga ukaribu, kuunganishana, kupeana nafasi ya kufanikiwa pamoja. Mwanachama yeyote anaweza kwenda mkoa wowote na kupokelewa Kama mwanafamilia kupitia mabalozi Walio kila mkoa..

Kabla hatujaanza kuchambua fursa mbalimbali lazima tufahamu kuwa fursa ya kwanza ni watu.

Tunataka kupitia fursa 101 kila mwanachama akuze biashara yake. Awe connected na wanachama wote wa mikoa yote TANZANIA nzima. kuanzia sumbawanga mpaka Mwanza, kuanzia Mtwara mpaka Dsm. Kuanzia Arusha mpaka Tanga. Kuanzia Tanzania mpaka kenya, uganda, Rwanda na nchi zote za Afrika. Kumbukeni givers gain. Ukitaka kufanikiwa kibiashara jenga na watu, wakupe biashara, wakupe wateja, wakupe nafasi na ufike mbali. Biashara ni sanaa ya kujenga mahusiano. Kupitia fursa 101 tuwe familia moja na kuunganishana kama ndugu wenye lengo moja, mwelekeo mmoja na imani moja.

Mfahamu kuwa Tanzania nzima inahitaji mfumo huu. Tupo mwanzoni, tunapoangalia mbele tunakoenda wanachama fursa 101 tunaangalia watalaamu watakaoungana nasi, Serikali, taasisi na biashara zitakazozaliwa.

Tutafundishana fursa 101.
Tutatumia tekinolojia kuunganisha watu. Tutajenga mfumo wa mabalozi wa bidhaa or huduma zetu ili kuwezesha wanachama kuuza katika mikoa kupitia mabalozi .

Lengo letu ni moja kujenga mfumo wa umoja, wenye lengo moja, mwelekeo mmoja na kumpa nafasi kila mwenye bidhaa or huduma yake kuuza kwa wengine.

Kupitia fursa 101 tunabadilisha namna ya kufanya biashara Tanzania.
Tutazalisha biashara mpya. Tutazalisha wajasiriamali wapya.

Naomba niwaambie wanachama biashara ni kutokana na watu unaojuana. Wajasiriamali wengi wana bidhaa nzuri, huduma nzuri lakini hakuna mauzo. Hakuna biashara. Why? kwasababu hawajazungukwa na watu potential. Fursa 101 inataka kujenga mfumo unaotuunganisha watu potential, Wateja potential , wanachama wote tukisaidiana na mabalozi wetu kuleta wafanyabiashara na watu potential pamoja na kuwafanya sehemu ya familia Tutafika mbali.
Tutauziana huduma, bidhaa na kupeana fursa zilizo katika kila mkoa. Tutakuwa na trainers, watalaamu wa kilimo, biashara, mauzo, networking, uwekezaji, mitaji, kuuza, business plans, taasisi mbalimbali wanachama, insurance, benki nk.

Katika Kila mikutano ya mwezi kila mwanachama apate nafasi ya kuelezea biashara yake. Huduma yake, bidhaa yake. Kama maonyesho, mafunzo yawepo na watalaamu wa ubora ili tuboreshe bidhaa or huduma zetu. Tunataka kila mtu awe mtu wa watu. Tujenge mahusiano pamoja kupitia biashara zetu. Masomo. Taasisi mbalimbali. Kila mkoa tutaweka target zetu.
Mpaka October 27 siku ya Fursa 101 Forum & Expo kila mkoa uwe na wanachama kuanzia 500.

Wajasiriamali wangapi watazaliwa kupitia mfumo huu?

Biashara ngapi zitakua kupitia mfumo huu?

Nina Imani na wewe. Ninakuamini .

Karibu Fursa 101
Mimi ni Balozi Fursa 101

Mimi ni sababu ya Mafanikio yako.
Fursa 101

Thursday, August 16, 2018

Difference between http and https

What is the difference between http and https?

Some of you may be aware of this difference, but it is
worth sharing for many that are not.

The main difference between http:// and https:// is all about keeping you secure.

HTTP stands  for Hyper Text Transfer Protocol.
The S (big  surprise)  stands for "Secure". If you visit a Website or web page, and look at the address in the web browser, it is likely begin with the following: http:///.

This means that the website is talking to your browser using
the regular unsecured language. In other words, it is possible for someone to  "eavesdrop" on your computer's conversation with  the Website. If you fill out a form on the website, someone might see the information you send to that site.
     
This is why you never ever enter your credit card number in an
Http website! But if the web address begins with https://, that means your computer is talking to the website in  a
Secure code that no one can eavesdrop on.

Now, you understand why this is so important, right?
     
If a website ever asks you to enter your Credit/Debit card
Information, you should automatically look to see if the web
address begins with https://.
     
If  it doesn't, you should NEVER enter sensitive Information such as a credit/debit card number.
     
PLS PASS IT ON (You may save someone a lot of grief).


While checking the name of any website, first look for the domain extension (.com or .org, .co.in, .net  etc). The name just before this is the domain name of the website. Eg, in the above example, http://amazon.diwali-festivals.com, the word before .com is "diwali-festivals" (and NOT "amazon"). So, this webpage does not belong to amazon.com but belongs to "diwali-festivals.com", which we all haven't heard of before.
You can similarly check for bank frauds.
Before your ebanking logins, make sure that the name just before ".com" is the name of your bank. "Something.icicibank.com" belongs to icici; but, icicibank.some1else.com belongs to "some1els.

You've hopefully learned something new, now please share and educate others.