Adimu Nihuka Jr |
Imetungwa na Adimu Nihuka Jr
MUME= mke wangu nakupenda kwa
utu wako na jitihada zako na uraahim na upole wako kwangu na watoto wetu na
namna unavyoheshimu wazee wangu na kuwafanya kama wako. sioni raaha ukiwa mbali
na macho yangu na ninapokua kokote hua nawaza mbio kurudi nyumbani. mapishi
yako na huruma zako zanilewesha mwenzangu. nakupenda kwa utu wako na subra na
kunijali mimi mumeo nikiwa nacho au kama sina. mapenzi yako yana harara na joto
kwangu na niko taabani kwa hubba zako . killa
nikirudi nyumbani hupata utulivu na killa ninapokwenda kusali masjid nguo zangu
hunukia manukato mazuri unayoniwekea. na duaa yako na tabassamu zako killa
nikienda kazini na kurudi nyumbani zinanipa nyingi ilhaamu kuzidi kukupenda
habiby wangu kipenzi.
MKE= najivunia kua na mume mwema kama wewe na raaha zako hazina
kifano mume wangu. sauty yako nikiisikia mlangoni unapobisha mimi hua sijifai
sijitambui kwa hubaa zako na kukimbimilia mlangoni kukukopokea mume wangu
habiby. nashkuru kupata mume kama wewe unayeniongoza katika haqq na kuniombea
duaa na kunifundisha mengi mazuri na kunipa killa aina vitu kadri ya uwezo
wako. nikiwa na udhaaifu wanipumbaza na nikiwa na msiba wanipa nasaha njema,
unawaheshimu wazee wangu na ndugu zangu na killa alo wangu, na huchoki
kunihimiza kufanya ibaada na kunijali kwa hisia zangu. subra yako kwangu nikiwa
na mimba na utulivu wako na mahaba yako ya dhaty ndio yanayonifanya nizidi
kukupenda laazizi wangu. sina cha kuongezea illa natosheka na hubba zako na
nitazidi kukupenda kwa killa hali mume wangu na Mola akuhifadhy na akupe mazuri
maishani mwako.
No comments:
Post a Comment