Friday, April 27, 2018

Jinsi ya kufanya endapo computer yako itakataa kuwaka na kuonyesha baadhi ya files katika screen

Usikurupuke kupeleka computer yako kwa fundi,kwa tatizo ambalo unaweza kulirekebisha wewe mwenyewe.

Kama una computer ambayo ukiiwasha inawaka bila kuonesh kitu kwenye screen,tafadhali fuatilia kwa makini maelzo haya ambayo yanaweza kurudisha computer
yako katika hali yake ya kawaida.

kwanza kabisa tatizo la computer yako kutokuonesha kitu (black Screen au dead screen linatokana na sababu mbali mbali.

1. Tatizo kwenye RAM au RAM slots

2. Processor
(ni mara chache sana processor kuzingua, hua hazizingui ovyo ila ikitokea bahati
mbaya,)

3. Graphics card
ni card inayohusika na vinavyoonekana kwenye pc viwe kama ambavyo Vinatakiwa
kuonekana.Kama ikiwa hijaunga vizur, processor ita terminate booting process

4. Inverter
ndio inayofanya screen ya computer yako ionekane.
kama shida ikiwa kwenye inverter, uki connect external screen (desktop au Tv), utaona computer inawaka kama kawaida.

JINSI YA KUTATUA HILI TATIZO:
kabla hujafanya jambo lolote, naomba nikujulishe kuwa computer yako inawaka vizur, ila BIOS haifanyi.

 kwa maana kwamba, ikisha power up, cha kwanza kabisa processor hua inafanya check up kujua kama kila kitu kwenye mother board + input
na output system zipo sawa sawia.
processor ikiona shida yoyote ile, haitoendelea na booting(kuwaka). na hapo ita display error kwenye pc yako. kwa kua pc yako haioneshi error yoyote, tunaweza
kuhisi kua RAM inaleta shida kwa sababu, chochote ambacho computer inakifanya,kinafanyika kwenye Random-Access memory.

Kama RAM ikiwa mbovu, basi lazima screen yako haitoonesha kitu chochote. lakini pia pengine screen yako imekufa
(inverter imeharibika au kioo kimepasuka) sasa ili umjue mchawi nani, itabidi ui connect na screen ya nje. screen ya nje inaweza kua TV au projector.
Utachomeka VGA cable au HDMI cable kwenye computer yako na ile Tv yako au desktop ya computer au projector halafu utaiwasha pc yako.
kama screen ya nje ikiwaka, basi shida ni screen, hapo itakulazimu kununua screen mpya au inverter mpya depending on where the problem is.
lakini pia lazima ufanye RAM TEST.

Kama computer yako ina slot 2 za ram, basi zitoe zote na ku test RAM moja moja kwenye kila slot na kuangalia kama itawaka.(nlishawai ku solve tatizo kwa njia hii) kama ikigoma, basi tatizo litakua kwenye graphics card,ni vigumu sana kurekebisha tatizo lililopo kwenye graphics card.
itabidi uipeleke kwa fundi mzuri ili aichome tena graphics card kwa moto mkali.

PLAN B:
1- toa betri na charger, then bonyeza button ya kuwasha kwa sec 30 ili u drain CMOS battery.
2- rudisha betri na charger halafu bonyeza fn + esc na button ya kuwasha kwa pamoja, pc yako itawaka. ikigoma fuata maelekezo ya hapo juu.

No comments:

Post a Comment