Sunday, May 13, 2018

Biashara za mitandaoni zinazotengeneza mamilioni ya pesa

Na Adimu Nihuka Jr
( A) Kutengeneza pesa kupitia blogu au website yako,

Hasahasa blogu siku hizi zimekuwa ni chanzo kikubwa sana cha pesa kwa watu wengi. Blog zina namna nyingi mtu anaweza akajipatia fedha kama vile;

Kuuza na kutangaza bidhaa za kawaida, mfano unaweza kuuza dawa za asili, nguo, urembo nk kupitia blogu yako.Kuweka matangazo ya google, Google Adsense. Ikiwa blog yako inapata idadi kubwa ya watembeleaji kwa siku, unasaini mkataba na Google wanakupa matangazo unaweka na pindi mteja anapobonyeza tangazo hurekodiwa na google hukulipa baada ya kipindi fulani.Kuuza nafasi za matangazo kama vile wafanyavyo watu wa magazeti, unaweka tangazo na kutoza kiasi cha fedha ulichopanga.

Uzuri wa blogu kwenye kujiendesha yenyewe ni kwamba wewe baada ya kuweka maandishi yako na picha, ukahakikisha umeyafanyia utafiti wa kutosha (Search Engine Optimisation) SEO, kazi kubwa hubakia kwa mtandao wenyewe kwani wewe hutajua saa wala siku wateja watakapotembelea blogu yako. Utashangaa tu namba ya idadi ya watembeleaji ikipaa juu.

Tena unaweza pia ukaiongezea vitu vingine vitakavyoifanya blogu ijiendeshe yenyewe zaidi(Automation) kwa mfano vitu kama autoresponder au email list ambayo wasomaji na watumiaji wa blogu yako wanapata huduma mbalimbali kama kudownload vitabu vya bure au kupokea makala moja kwa moja ‘automatically’ hata kama wewe muda huo upo katika mihangaiko yako mingine.

(B) Kuingiza pesa kupitia mtandao wa You Tube

Kwenye intaneti pia unaweza ukatengeneza pesa nyingi kwa kuweka picha za video katika mtandao wa youtube ambapo watazamaji watakapofungua video zako, you tube huweka na matangazo yao pale hivyo kukulipa kulingana na ni idadi gani ya watazamaji wanaozifungua video hizo na kuzitazama. Ukiweza kuupload video zinazotazamwa na watu wengi sana kwa siku ndivyo hivyohivyo napo utakavyolipwa fedha nyingi.

(C) Biashara ya kununua na kuuza Blogu.

Unaweza kuingiza kitita cha fedha kwa kufanya biashara ya kununua na kuuza blogu zilizokwishatengeneza na watu wengine ambazo zimeshapata idadi kubwa ya watembeleaji. Hii pia hufanyika katika akaunti za mitandao mbalimbali ya kijamii kwa mfano hata hapa Tanzania wapo watu wanaokuza akaunti mfano za Instagram na kuziuza kwa bei kubwa kwa watu wengine mara baada ya kuwa na wafuasi wengi.

(D) Kutengeneza Apps za kwenye simu au kompyuta namichezo ya kompyuta.

Siku hizi kuna kitu kinakuja kwa kasi ya ajabu na huenda baadae kidogo kikaja kufunika mambo mengi; “Mobile Apps” ni applications za kwenye simu za kisasa ‘Smart phones’ ukifanikiwa kutengeneza moja tu ikapendwa na watu, unaweza ukauza dunia nzima na watu kama kawaida yao wakaanza kudai umeingia kwenye biashara haramu
@softwaretz

UKITAKA MSAADA ZAIDI KUTENGENEZEWA AU KUFUNDISHWA CHOCHOTE HAPO NITAFUTE  +255742989953

AU NJOO INBOX @halftime1

No comments:

Post a Comment