Friday, May 18, 2018

Jinsi ya kupata mtaji wa Biashara

Na mwandishi wetu.
Mitaji haisubiriwi!
Ni kweli biashara inahitaji mitaji ili iweze ku scale up lakini mitaji haisubiriwi. Ukiona viwanda vya Bakhresa Industries utadhani wameshiba mitaji, la hasha wao pia wanatafuta mitaji kwa viwango vyao.

Mohamed Enterprises, viwanda vyake vilipoanza kukua alihitaji mitaji mikubwa, na kulikuwa madeni makubwa anatakiwa kulipa lakini Benki za Tanzania hazikuwa na uwezo wa kumpatia mitaji. Alihangaika sana. Yaani kiasi alichohitaji benki hazikuweza kumpatia, unadhani aliishia hapo…akaondoka kwenda South Afrika akapata mitaji ndipo alipokuja akaipeleka biashara yake juu na kuwa juu ya wengine.

Kila biashara inahitaji mtaji, wewe unayelia sijui mimi sina mtaji …usidhani wengine wana mitaji imepandwa majumbani kwao, wapo uwanjani wanatafuta. Hakuna aliyeshiba mitaji

Nisingependa kukutia moyo, kupata mitaji siyo jambo rahisi lakini inapatikana. Yeyote anayekuambia mitaji ni rahisi kupatikana mwambie akupe mtaji wake akatafute mwingine. Kupata mitaji yataka moyo. Lazima upambane kwa nguvu, kama umekaa mahali kusubiri milango ifunguke bila kutafuta utasubiri sana.
Watu wengine ni wa ajabu sana, hawatumii nguvu yoyote kupata Zaidi ya kuishia kusema hakuna mitaji.

Wengine wanasali wakisubiri kwa matumaini wakitegemea mitaji itatokea isikojulikana bila kufanya chochote.
Wakati watu hao wanasubiri wasisahau kuwa muda unazidi kuyoyoma. Mwezi mmoja unakuwa miezi sita. Miezi sita inakuwa mwaka. Mwaka unakuwa miaka mitano. Wakati muda unayoyoma kwa matumaini , ukumbuke mawazo makubwa waliyokuwa nayo, ndoto kubwa walizokuwa nazo zinazidi kuota kutu, zinapitwa na wakati na kufifia kila siku.

Maisha ya watu wengi yanapotea wakiwa wanasubiri mambo yatakuwa mazuri kwa matumaini, bila kufanya jambo. Mwezi unakatika kwa matumaini. Mwaka wa pili unakatika kwa matumaini. Miaka mitano inapotea kwa matumaini. Simaanishi usiwe na matumaini, lakini huwezi kuishi kwa kutegemea matumaini bila kufanya jambo.

Nikikutana na mtu ana wazo kubwa halafu anasubiri mtaji kwa matumaini hiyo ni horrible excuse. Ni upuuzi. Ni kupoteza Maisha. Huwezi kupata matokeo duniani bila kusababisha, lazima ufanye kitu.
Kuliko kukaa na kusubiri kwa matumaini ili mambo yatokee , kuna mambo ya kufanya.

#Vunja vunja ndoto yako na kuigawa katika vipande vipande.
Najua hujanielewa hapa. Assume biashara inahitaji mtaji wa million 50, ukikaa kusubiri kupata pesa yote Tshs.50 million kwa matumaini itakuchukua miaka.
Muda mwingine unaweza kugundua kuwa biashara yako inahitaji laki moja tu kama kianzio, ili utengeneze mazingira ya kupata Tshs.50million.

 Ukiniambia huwezi kupata laki moja kwa ndugu na marafiki siwezi kukuelewa unless umezungukwa na watu makapuku waliopitiliza, hilo nalo ni kosa la jinai.
Siyo vibaya kuwa na ndoto kubwa lakini lazima ujifunze jinsi ya kupanda ngazi moja moja, ukiwa unatembea njiani lazima ukutane na mengine ya kukupeleka mbele. Usidharau mwanzo wako mdogo.

Inawezekana unataka kulima ekari 100, lakini unaweza kuanza ekari moja ukauza na kuwaonyesha wengine faida za ekari moja, unadhani nani hatawekeza kwako?

# Badili nafasi.
Kuna ndoto nyingine si kutokana na ukosefu wa mtaji ila sehemu uliyosimama siyo. Watu uliozungukwa siyo. Mazingira uliyozungukwa, watu uliozungukwa wana nguvu sana ya kukuzuia kwenda mbele “Change your position”

# Jenga na wateja,
Wateja ni wawekezaji wakubwa wanaosahaulika. Inawezekana unawaza huna mtaji kumbe mitaji imeshikiliwa na wateja wako. Jiulize una wateja wanaoweza kukulipa in advance?

Je una wateja wanaoweza kununua Zaidi?
Je una wateja wanaoweza kuleta wateja?
Naomba kuuliza una ukaribu kiasi gani na wateja wako?
Labda nikuambie ukweli mteja ni ndugu yako. Tatizo alilonalo mteja wangu ni tatizo langu hata kama halina mahusiano na biashara yangu. Mteja ni ndugu yangu.

Kama tungekuwa tunawahudumia wateja wetu vizuri, tunaishi nao kama ndugu tusingekuwa tunahangaika kutangaza kwenye tv .
Hakuna tangazo lenye nguvu duniani kama tangazo la mteja wako kukutangazia biashara yako.

Umejenga vipi na wateja wako?
Naomba mengine tumalizie ndani ya Fursa 101…
Mimi ni sababu ya mafanikio yako. Wewe ni sababu ya mafanikio yangu.

Geophrey Tenganamba.
0655973248.

No comments:

Post a Comment