Na mwandishi wetu
Post hii itawalenga sana watumiaji wa computer lakini hata wale watumiaji wa smartphone ambao wapo addicted sana na simu zao yaani nkiwa namaanisha unakuta mtu karibia lisaa lizima umekodolea tu simu yako pasipo hata kugeuka kwengine.... Ebu ngoja tuangalie Tile ya hii post inahusu nini haswa.
Wote tunatambua kwamba matumizi ya computer ya muda mrefu kuna wakati haya epukiki iwe umejiajiri, umeajiriwa au hata ni mwanafunzi ni lazima utatumia computer kwa muda mrefu kwa namna moja ama nyingne.
Sasa nataka nkujuze kwamba matumizi hayo husababisha madhara mbalimbali kwenye miili yetu kuanzia kwenye macho hadi kwenye sehem nyingne za mwili kutokana na kukaa sana.
#Yatambue_matatizo_hayo
Baadhi ya matatizo au dalili zinazopatikana kwa kutumia computer muda mrefu ni pamoja na macho kuwa yanawaka moto au kuwasha, kichwa kuuma, kutokuona vizuri na hata kuona ukungu pamoja na matatizo mengne ya muda mfupi ambayo kwa ujumla wake yamepewa jina la kitaalamu #computer_vision_syndrome.
Kwa mujibu wa mtandao wa #WebMD bado hakuna ushahidi kwamba utumiaji wa computer kwa muda mrefu basi husababisha upofu badala yake watafiti hao wamegundua matatizo mbalimbali ambayo ndo kwa ujumla wake yakaitwa #Computer_vision_syndrome.
20.20.20
Lakini pamoja na matatizo yote hayo kuna njia ya kujilinda usipate matatizo hayo ... Njia moja ambayo ni muhimu ambayo ndio inayoshauriwa na wataalamu wengi ni pamoja na sheria ya 20.20.20.
Sheria hiyo sio mpya bali ni sheria inayotumiwa na watu wengi sana kwa sasa japo kwa hapa maskani TZ sidhan kama inatumika kwa upana wake na kama inavyotakiwa.
Hapo kwenye hiyo sheria najuwa bado raia bado hawajaelewa ila utaangalia picha hiyo nliopost pamoja na hii post nadhani utaelewa vema jinsi ya kufata sheria hiyo rahisi iyosaidia kutunza macho yako na kukuepusha na #computer_vision_syndrome.
#Maana_ya_sheria_ya_20.20.20
Maana yake ni kwamba endapo unaangalia computer kwa muda mrefu basi unatakiwa kupumzisha macho kila baada ya dakika 20.. Na wakati huo unapumzisha macho yako basi unayapumzisha kwa staili ya kuangalia kitu kilichopo umbali wa futi 20 kutoka mahali ulipo.. Na unatakiwa kukitazama kitu hicho kwa muda wa sekunde 20 basi hiyo ndo maana halisi ya hii sheria ya 20.20.20.
Hapa najuwa kuna raia wataanza kuhoji kwanini ni sekunde 20?.. Kwa mujibu wa tovuti ya healthline ( soma hapa kama unataka kuelewa zaidi https://www.healthline.com/health/eye-health/20-20-20-rule#definition )
Macho hutumia sekunde 20 kuweza kukamilika kikamilifu hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unafata sheria hii kikamilifu. Wataalamu mbali mbali wa maswala ya macho duniani wanashauri sana sheria hii na kuhakikisha unaifata kikamilifu pamoja na kupumzisha macho yako mara kwa mara haswa wale wafanyakazi wa maofisini ambao huangalia karatasi nyeupe na kisha kuangalia tena kioo cha computer.
#Mwisho
Sheria hii wame deal sana na watu wa matumizi ya computer ila binafsi Nawaingiza wale wenye matumizi ya simu kupitiliza, wale wanaopenda kuangalia movie sana kwenye pc zao na wengne wote mnaojijua ebu fateni sheria hii ili badae tusije vaa lens za ajabu machoni mwetu... Kama unapenda kuvaa zile lens kama wazovaa wazee wetu puuzieni hii.
Kama unataka kusoma zaidi kuhusu #Computer_vision_syndrome basi tembelea hyo link hapo chini kwa maana nimefupisha sana post na kwa kuzungumzia kile nlicho kilenga kwahyo yapo mengi zaidi ya wewe kujifunza ambayo cjayazungumzia.
https://www.webmd.com/eye-health/computer-vision-syndrome#1
No comments:
Post a Comment