Wednesday, May 16, 2018

Brand bora za viatu Afrika

Na Adimu Nihuka Jr
Tunataka ubora. Lakini tunataka tupige kelele.
Nataka kutaja brands za viatu zinazotisha Duniani kutoka Africa. Zinazalishwa Africa.

 #Brand ya kwanza ni Sole Rebels kutoka Ethiopia.

Brand hii inauzwa zaidi ya nchi 50 ikiwa ni pamoja na   USA, Canada, Japan na Switzerland.

Mnamkumbuka Bethlehem Alemu, brand hii ilianzishwa na mwanamke  2004  kwa mtaji wa chini ya Milioni 15 .....tena alichangiwa na familia yake.

Anazalisha zaidi ya bilioni 2 Tsh kwa mwaka.
Niliwasimulia historia yake. Sitaki kurudia.

#Brand ya pili ni Della kutoka Ghana.

Brand hii waliungana watu kutoka US na Ghana.
Vijana hao ni Tina Tangalakis kutoka US na Nii Addotey, kutoka Ghana. Brand hii inauzwa nchi nyingi sana duniani.

#Brand ya tatu ni  ENZI kutoka Kenya & Ethiopia.

Watu waliosababisha brand hii ni marafiki wa karibu na wa muda mrefu Christian Ward (UK), Jawad Braye (USA), Sam Imende (Kenya) na  Azariah Mengistu kutoka (Ethiopia).

Kiwanda cha brand hii kina office kubwa Ethiopia na Kenya. Mimi sijui na sisi watanzania tutaamka lini. Wanafursa 101 amkeni kumekucha.

Brand hii ina retail shops ina maduka makubwa katika nchi duniani hiyo ni pamoja na  London, Hong Kong, Paris, New York na Johannesburg.

#Brand ya nne ni Buqisi-Ruux  kutoka Kenya & Uganda.
Brand hii ilianzishwa na vijana watatu Nuba Elamin, Lynn na Tetsi Bugaari.

Maana halisi ya brand ya  Buqisi-Ruux ni “Malkia wa kijiji”
Kiwanda cha brand hii kipo Nairobi, Kenya na wana ofisi  Kampala (Uganda) , Cape Town (South Africa), na wanauza nchi mbalimbali duniani.

#Brand ya tano ni  T.T. Dalk (Nigeria)

Brand hii ilianzishwa na Temilade Osinfade. Akiwa chuo alikuwa anapenda kuchora design mbalimbali za viatu kwenye madaftari yake. Akiwa shule akaanza kutengeneza kiatu kimoja baada ya kingine. Kwasasa anauza duniani.

 #Brand ya sita ni Swaheelies (Kenya)

Tena brand hii wanatumia sana malighafi sana kutoka Tanzania, Ghana, Kenya na Nigeria.

Sana wanategemea malighafi za Tanzania. Wanakuja kuchukua malighafi hapa hapa tukiwa tunatoa macho.

Aliyesababisha brand hii ni Chania Lackey, kijana ambaye alikuwa ni mwanasheria. Mwanamke huyu. Chania huyu aliamua kuwaunganisha mafundi na watalaamu kama akina Baraka maeneo ya Kibera Nairobi.Vijana hawa wa Kibera hawakuwa na uwezo wa kulea familia zao lakini walikuwa na ujuzi huo. Mimi sijui na sisi Fursa 101 tunaamka lini. Kuna vijana wengi wenye ujuzi wa vitu vingi mitaani tumekaa kimya tunasubiri mishahara. Mungu anawaona nyie wanadamu.

#Brand ya saba ni  HTW – Heel The World (Ghana)
Nimewahi kuwasimulia kuhusu Fred Deegbe’s.

Baada ya Fred kununua kiatu cha bei ghari sana kutoka nje, akashangaa kwanini Ghana imejaa vijana wenye vipaji na uwezo wa kuzalisha viatu vizuri zaidi ya hivi?

Nini tatizo?
Akaacha kazi benki na kuanzisha brand hiyo.
Brand hii ilianzia kwenye gereji ya baba yake, Accra, Ghana. Akakusanya vijana hao wakaanza kuzalishia viatu hivyo kwao kwenye gereji.
Kwasasa anauza dunia nzima.

Najiuliza kwa akili ya kuku ina maana hatuwezi kushirikiana tukafanya kitu cha maana au ni ubinafsi tu unatutafuna watanzania jamani???

#Brand ya nane ni Haus of Hercules (Nigeria)

Brand hii ilianzishwa na kijana designer mmoja  Christopher Jeje. Brand hii alianza mwaka 2010 kwa mtaji wa 60,000Tshs.Sasa anauza kimataifa na kusikika. Hivi umesikia alianza kwa mtaji wa elfu sitini.....upo???

#Brand ya tisa ni Passport ADV (Ethiopia)
Brand hii ilianzishwa na kijana Mikhayel “MikJagga” Tesfaye mwaka 2009.

#Brand ya kumi ni  Hesey Designs (Nigeria)

Aliyesababisha brand hii ni Odiete Eseoghene, akiwa na miaka 25 miaka miwili baada ya kumaliza chuo. Huyu binti alitengeneza brand hiyo mpaka Richard Branson tajiri mkubwa akavaa...hapo ndipo alipopata umaarufu.

Sasa basi. Fursa 101 tunahitaji kuingia kwenye brand ya kumi na moja. Tunahitaji kuzalisha bidhaa humu ndani..

Hapa sisemei viatu peke yake yaani bidhaa zote.

Brand ya chai kupita chai bora izaliwe humu.

Brand ya sanitary pads

Brand ya mashine za kilimo

Brands za sabuni

Brands za nguo

Tufanyaje sasa?

Source:  Fursa 101 whatsapp na telegram group

No comments:

Post a Comment