Thursday, May 17, 2018

Kama computer yako umeme unasumbua fanya hivi

Na mwandishi wetu
Power Supply Failure).
Kitendo hiki ni hali ambayo hutokea pale ambapo unajikuta Kompyuta haipokei umeme kwa ajili ya kuonesha maandishi kwenye kioo cha kompyuta.

DALILI MABLIMBALI ZINAZOONESHA KUSHINDWA KUSAMBAA KWA UMEME KWENYE KOMPYUTA.
Zipo ishara mbalimbali ambalo linadhihirisha kuwa kwa kiwango kikubwa umeme ni tatizo kwenye Kompyuta. Lakini kwa sasa tuzungumzie kwa kifupi dalili hizi;

1.Kompyuta inapowashwa hakuna kitu kinachotokea, yaani unaweka Adapter kwenye Kompyuta lakini bado haiwaki, unaisha lakini bado haioneshi dalili ya kuwaka.

2. Ukiwasha Kompyuta inawaka, na baada ya muda mfupi sana inazima na wakati huo huo umechomeka Adapter kwenye Kompyuta yako. Hii ni dalili kuwa Ubao Mama haupokei umeme wa uhakika katika utendaji wake wa kazi, kuna mapungufu.

3.Wakati mwingine wakati unaendelea kufanya kazi, huku Kompyuta umeweka Adapter, betri ni nzima na huku inaonyesha inachaji, na ghafla ikazima, hi ni dalili kuwa kuna mapungufu katika mfumo wa umeme wa Kompyuta yako.
                   
 KINACHOSABABISHA TATIZO HILI.
1.Kuwepo kwa Shoti saketi kwenye Kompyuta yako (Short Circuit), hii ni hali ambayo hutokea hasa pale ambapo saketi humwagikiwa na kimiminika(liquid), pale Kompyuta inapomwagiwa vitu kama chai, soda, maji, uji, n.k huweza kusababisha kuharibika kwa motherboard.

2.Kuwepo kwa uchafu, moshi, kwenye Ubao mama(motherboard), kama Kompyuta haifanyiwi usafi pia inaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa ubao mama.

3.Kuchemka/ kupata joto jingi kwa Kompyuta, jambo ambalo husababishwa na Kushindwa kufanya kazi kwa feni

4.Adapter (chager) ambayo haiendani na Kompyuta yako. Hapa utakuta mtu anatumia Adapter ambayo haina uwezo kwa kuwasha Kompyuta yake, hapa tunazungumzia kuwa usitumie Adapter yenye uwezo mdogo.

5.Adapter na Power cable kuwa mbovu, hii nayo inaweza kuwa sababu maana yake umeme hauingii kwenye ubao mama ili kioo kiweze kuwaka.

6.Tatizo la kimazingira, hii ni hali ambayo mara nyingi unakuta hasa kipindi cha masika vifaa vya ki-electroniki hupata ubaridi unaopelekea kusababisha kuwepo kwa hali inayosababisha hata kuungua kwa baadhi ya chip kwenye Kompyuta.

7.Kuharbika kwa Power jack. Kile kitundu ambacho Adapter inachomekwa ili ipate kuchaji kompyuta.

 JINSI YA KUTATUA TATIZO.
1.Hakikisha Power cable pamoja na Adapter vipo katika ubora yaani, kisiwepo kifaa ambacho kina tatizo. Chunguza kwa umakini, pia angalia kama kwenye chanzo cha umeme kama umeme unaingia kwenye Adapter yako.

2.Hakikisha una mazoea ya kufanya “Service” kwenye Kompyuta yako, ambapo itakupa wakati mzuri wa kutunza Kompyuta yako na kuweza kugundua baadhi ya matatizo kama “Short Circuit”, kushindwa kufanya kazi kwa feni n.k.

3.Pia unaweza kwenda kwa fundi/Technician mwenye uwezo na ujuzi wa kuitengeneza Kompyuta yako kutatua tatizo lolote hasa la Shoti kwenye Kompyuta yako.

4.Tumia Adapter ambayo inaendana na Model ya Kompyuta yako, mfano kama Kompyuta yako inatumia “Input 19.5v= 3.34A usitumie.
Adapter pungufu ya hiyo, maana wakati mwingine inaweza ikachaji lakini ikasababisha kutokea kwa tatizo la “mouse” kushidwa kutulia sehemu moja

No comments:

Post a Comment