Na Adimu Nihuka Jr
Asante mwanachama Fursa 101 kwa kuja na kesi ya mbaazi, nimeisikia sana na kuifuatilia kwa ukaribu mno.
Wakulima wa Mbaazi Tanzania wanalia, wengi wamekata tamaa. Miezi michache mimi nilipigiwa sim una wakulima wawili baada ya kipindi cha TBC wakiuliza
“Ni vipi Fursa 101 itatusaidia sisi wakulima wa Mbaazi? Imagine mimi nina magunia Zaidi ya 50 yapo ndani, sina wateja. 1kg tulikuwa tunauza kuanzia Tshs.2500 mpaka Tshs 3500 leo hii sokoni wanunuzi wanataka tuuze 1kg kwa Tshs. 300 mpaka 500.
Bei hii hairudishi hata gharama ya kulima. Mbaazi zinaharikibika Mr. Fursa 101. Tuokoeni wakulima..tuokoeni… Serikali ilisema itakuja na soko kutoka India lakini tunaona kimya. Tuokoeni jamani”
Siyo mara yangu ya kwanza kupokea kesi kama hizi kutoka kwa wakulima. Tanzania ikiwa na wakulima wadogo wadogo kama hawa Zaidi ya 31 million wanapitia maumivu ya aina hii. Hawa wakulima ndiyo walio kwenye kundi la watu masikini. Inauma sana…Hii ndiyo sababu tumeanzisha Fursa 101 ili kutatua soko la wakulima na kuwakutanisha na wateja wao moja kwa moja kwa tekinolojia, Zaidi ya hapo nipo na watalaamu ili kutengeneza mfumo wa uber kwaajili ya kusafirisha bidhaa za wakulima mpaka kwa wahitaji. Ili kupunguza post-harvest loss mfumo wa mafunzo ndani ya Fursa 101 kuhusu processing ya bidhaa mbalimbali za kilimo, kila bidhaa inayotoka shambani inaweza kuwa processed au kuongezwa thamani na kuzalisha bidhaa nyingine …
Tuachane na hayo turudi kwenye mbaazi. Ni kweli Serikali ilipewa nafasi na India ya kusaini mkataba wa kupeleka Mbaazi India, lakini haikuwa na uhakika na wakulima wa Mbaazi.
Je watazalisha kwa viwango kulingana na mkataba? The same case ya Mihogo, Serikali ilidharirika sana kwani iliingia mkataba kuwa inaweza kukidhi soko la Mihogo nadhani ni mwaka 2015, lakini hata nusu ya mkataba haikufikisha. Swali likaja je, wakulima wa mbaazi wangeweza kukidhi soko la mbaazi? Kwasababu hiyo na sababu nyingine, Serikali ilichelewa kusaini mkataba, na india walizalisha mbaazi kwa kiasi kikubwa tu.
Na Tanzania pia tukazalisha mbaazi kwa kiasi kikubwa sana, wakulima wamehangaika kupeleka mbaazi India lakini hakuna soko tena, mwishoni wameziweka zinaliwa na wadudu.
Tufanyaje sasa? Tuungane na wakulima tuanze kulia kama watoto? Au tutafute njia mbadala ya soko la ndani?
Watu wanajua kweli kuhusu mazao ya mbaazi. Waingereza wanasema protein ya mbaazi ni beyond meat. Kuna bidhaa nyingi zinaweza kuzalishwa kwa kutumia Mbaazi. Badala ya kuungana na wakulima kuanza kulia, hii ni Fursa kwa wajasiriamali.
Food suppliments nyingi zinatengenezwa kwa kutumia mbaazi. Mbaazi ni zao pekee lenye protein nyingi sana, hivyo kutumika na watalaamu wengi kuzalisha food suppliments.
Mbaazi inaweza kutumika kuzalisha chocolate, supu ya mbaazi, mbaazi inaweza kutumika kuzalisha biscuits, mikate pia ipo…mikate ya mbaazi.Unga wa mbaazi unaweza kutumika kama lishe mbalimbali.
Mbaazi ni zao linaloweza kuzalisha bidhaa nyingi sana. Kinachokosekana ni maarifa…hii ndiyo sababu inayoisukuma Fursa 101.
Hizi zote ni suppliments zilizotengenezwa kwa kutumia mbaazi.
Kuna vinywaji vya mbaazi vinaweza kutengenezwa pia…kuliko kuungana kulia na wakulima mara kumi tujifunze kiundani kuhusu bidhaa zitokanazo na mbaazi kwaajili ya soko la hapa hapa ndani japo hatutamaliza lakini tutapunguza. Kipi bora…
Welcome to Fursa 101
Geophrey Tenganamba.
0655973248.
No comments:
Post a Comment