Wednesday, May 16, 2018

Fursa ya chakula katika nafaka

Na Geophrey Tenganamba:
Habari mwanafamilia wa Fursa 101- Natumaini siku ya leo ni njema kwako. Bado tunaendelea fursa ya chakula katika Nafaka. Najua wengi mnatamani tuongelee kilimo cha sijui nyanya, matikiti, sijui ufugaji nk. Hayo yote yapo ndani ya Fursa ya chakula.

 Fursa hii kama nilivyosema jana itatuchukua siku kadhaa. Lakini nitahakikisha tunawapata wataalamu hasa wale wanaofanya kwa vitendo. Jana tuligusia kidogo upande wa nafaka- na mwanafamilia mmoja aliweza kueleza jinsi alivyoanzisha Jehsha Health Food Company. Bado tutaendelea kugusia hapa. Lakini kabla hatujagusia hapa ngoja tuseme kidogo kuhusu kilimo cha nafaka

Unapoingia kwenye kilimo cha nafaka- ngoja nikuambie ukweli kuhusu kajitabia fulani katika kilimo. Wakulima wengi tulionao hapa Tanzania wanapigwa(wanaonewa) kwasababu wanapoingia kwenye kilimo wanaingia bila kuwa na taarifa za kutosha. Kama wangekuwa hawapigwi nina hakika wakulima wangekuwa matajiri wakubwa Tanzania. Sasa utakapoingia kwenye kilimo- utakutana na hiyo culture.

Hiyo kitu ipo sana kwenye nafaka. Sasa unafanyaje?Tafuta taarifa za wakulima-na association mbalimbali za wakulima. Pata taarifa zote ujue unaingiaje- na unatumia  kasoro za  culture hiyo kwa faida yako.Nisiguse sana hapa kiusalama

Tunapokuja katika fursa ya ku process nafaka. Bado kuna uhitaji sana hapa hasa maeneo ya mijini. Kama ni mpenzi wa chakula- kuna fursa katika: (A) Maziwa ya soya, Tofu na Yogurt. Kwa mtaji wa Tsh. Mil. 5-30 ukiwekeza nguvu, unaweza kutengeneza faida(net profit) zaidi ya million 3 kwa mwezi. Wapo wamama wajanja wanapiga hela hapa.

 TIB Bank wanatoa mpaka mikopo yenye masharti madogo hapa ukiwa umesajili kampuni. (B)Kiwanda cha kusaga na ku package unga. Tafuta taarifa. Ukiamua kitu hata kama hukijui mwalimu atajitokeza. Unachokitafuta kinakutafuta.

Hapa kuna Rice Mill, Palm oil, Kusindika asali, Kusindika karanga, Mihogo, Miwa, hivi vyote ni viwanda vidogo unavyoweza kuanza kwa mtaji usiozidi Milioni 20. Lakini pia kuna support kubwa. Watu wanaoweka nguvu na nia hapa wanajenga uchumi mkubwa sana.

Wengine wananunua mpaka ma VX kwa fursa hizo. Kilichomfanikisha Bakhresa ni chakula- alianza kwa viwanda vidogo vidogo kama hivyo.

Nina hakika bado kuna akina Bakhresa wengi watazaliwa. Yapo makampuni Morogoro yanauza unga wa sembe ulio kuwa packaged. Wameteka soko  la Bakhresa Morogoro Katika Baadhi ya maeneo. Tafuta kwenye mtandao feed the future. Sembe yao imewekwa  virutubisho vilivyopotea kwa kukobolewa

Unajua hao wakulima wanatengeneza sh ngapi? Huwa nashindwa kuelewa kabisa- ninapokutana na msomi wa masters hana kampuni wakati mkulima wa darasa la saba anamiliki kampuni ya kusindika nafaka. Unaweza ukadhani biashara hii inahitaji mtaji mkubwa- hapana. Labda tuwasikie wakulima waliomo humu ndani watupe experience yao.

Ushuhuda wao. Meshack Maganga nina imani Unaweza kusema neno Katika kilimo na chakula. Nataka tumalize fursa ya nafaka na kusindika. Tuingie dhahabu ya kijani-  hapa ni kuanzia matunda, mboga mboga nk.

Habari wanafamilia wa Fursa 101. Natumaini siku ya leo ni njema kwenu. Bado tunaendelea kuchambua fursa Katika chakula upande wa nafaka. Kama nilivyosema mwanzo kuna fursa nyingi hapa- mfano ukiwa na kampuni unaweza kuandaa profile na barua ya utambulisho kwenye taasisi kujitambulisha kama msambazaji wa nafaka.

Hapa hata kama huna mtaji au una mtaji mdogo unafanya. Wewe unadhani jeshini wanakula nini? Mawe?  mashuleni, vyuoni, kambini, sherehe nk. Ninamjua mtu mmoja aliyeanza hivyo  anasambaza  maharagwe, mahindi, mchele,ngombe mashuleni. Ana helaa! Pesa zipo kihalali- siyo lazima uuze madawa ya kulevya.

Mahoteli makubwa- unadhani wanatoa wapi nafaka, mbogamboga, nyama nk? Utasema biashara bwana ni kujuana- huwezi kupeleka nafaka kwenye hoteli wasiokujua. Kwani wale wanaopata tender kwenye mahoteli walijuanaje? Walizaliwa tumbo moja? Ngoja nikupe siri hapa- ukitaka na wewe wakujue, tafuta tatizo lao halafu jitoe kwao. Wasaidie.

 Wanahangaika masoko- angalia vipi unaweza kuwa msaada kwao. Onyesha umuhimu wako kwao na wao watakupa tender tena kwa upendeleo. Kabla ya kuuza kitu kwa mtu  jenga undugu kwanza. Wapo wengine humu wakifika kwenye what'sapp group ni kuweka matangazo tu bila kusalimia


JENGA UNDUGU  NA WATU UNAOTEGEMEA KUWAUZIA KITU KWANZA MAMBO MENGINE YATAKUWA RAHISI

Source: Fursa 101 whatsapp group

No comments:

Post a Comment