Na Geophrey Tenganamba
Tujikumbushe japo tuliyosoma ndani ya Fursa 101.
Bado tunaendelea...
Mimi ni sababu ya mafanikio yako. Wewe ni sababu ya mafanikio yangu!
Ndugu wanafursa 101, habari za muda huu.
Fursa 101 inajivunia kuwa baadhi ya wanaDiaspora wamechukua hatua na kuanza kuwekeza Tanzania kupitia Fursa 101. Wapo wengine walioomba kuandaliwa mpaka business plan, marketing research etc.Tunaenda mbele,
Fursa 101 inawagusa wakulima kwa kuuza bidhaa za wakulima moja kwa moja kutoka shambani mpaka nyumbani kupitia www.fursa101.co.tz tena kwa bei ya shambani. Huna haja ya kwenda buguruni tena, unatoa oda yako unaletewa mahali ulipo. Unaweza kudownload apps za Fursa 101 pia.
Fursa 101 inataka kukukutanisha na watu wenye njaa ya kufanikiwa kibiashara, wenye uelewa mpana kuhusu biashara, wenye maono na taasisi kubwa kubwa.
Hivyo tunahitaji uchangamfu mkubwa. Kama hujaanza biashara ndiyo muda sasa wa kuanza na chochote ulichonacho, kama una biashara ni muda muafaka wa kutuma taarifa zako, tuunganishane masoko, maarifa na taarifa kiundani kusababisha mapinduzi.
Kuna mengi yanakuja ambayo wengine mtashangaa. Nasisitiza kama una changamoto yoyote kibiashara….masoko nk. njoo Fursa 101
Ngoja tuendelee na fursa zetu. Bado tupo kwenye Fursa ya Nishati ya Jua(Solar power)
Kama nilivyosema mwanzo, kuna shida kubwa ya umeme Afrika - Tanzania
Chini ya asilimia 20 ya waafrika wana access ya umeme. Fikiria chini ya asilimia 20. Hali ya umeme vijijini ndiyo balaa. Kwa kifupi ni kuwa asilimia kubwa ya watu wanaoishi vijijini hawana access ya umeme kabisa.
Tunafanyaje sasa? Hapo sasa ndiyo umuhimu wa nishati ya jua.
Wafanyabiashara kama akina Patrick Ngowi , waligundua Fursa hii ya nishati ya umeme na kuanza kutengeneza mamilioni ya pesa mapema kabisa kukiwa asubuhi.
Yupo ndugu yangu kijijini anayesafiri kwa baiskeli kwa masaa matatu kwenda maeneo karibu na mjini kuchaji simu yake tu.
Ukifuatilia maeneo ya vijijini utagundua kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaishi maisha ya aina hiyo.
Wale waliogundua Fursa hiyo wanajitengenezea pesa vijijini wakati sisi tupo mijini tunapakana jasho kwenye daladala.
Najua sisi tunaoishi mijini tunashangaa haya. Hivi karibuni nikiwa Arusha nilikutana na vijana kutoka Dar es salaam hawajasoma, wao wanasambaza taa za solar vijijini, wanatembea kila kijiji, wanauza taa hizo za solar pamoja na chargers zake kwa jumla na reja reja. Kuna mtu mmoja kariakoo karibu na gerezani anauza kupitia vijana hao. Hao vijana wanasema kila siku wanaingiza zaidi ya Tsh.50,000 kama malipo yao kila mmoja. Hawajasoma kabisa, lakini wamejifunza sanaa ya kuuza. Wana ushawishi hatarii. Nikafikiria kama vijana hawa wanatengeneza hii hela…bosi wao anaingiza shilingi ngapi?
Fikiria tu kwa akili ya kawaida.
Jana nilianza kuwasimulia kuhusu jamaa mmoja jina lake Richard Awuor. Huyu mtu alizaliwa Kenya, Mombasa. Akiwa kama mfanyakazi wa kampuni ya Heineken, alipangiwa kikazi Tanzania kama Country manager. Alipata nafasi ya kusafiri mikoani, ukweli alishangaa sana kuona maeneo mengi hayana umeme. Siku moja akiwa Airport ilimuuma sana alipoona umeme umekatika kwa muda mrefu. Hapo ndipo wazo la kuanzisha kampuni ya nishati ya jua Cellulike ilipozaliwa katika kichwa chake.
Hilo wazo lilitokea akiwa Mtwara, Airport …alijiuliza “Inakuaje hii jamani?”
Ilikuwa mwaka 2014.
Kutokana na hilo akaamua kuungana na wenzake na kuanza kufanya utafiti. Walisafiri Mwanza, Arusha na mikoa mingine.
Waligundua maeneo mengi yenye uhitaji wa solar power. Ngoja niwaambie wanafursa 101. Unajua kwanini tulianzisha Fursa 101?
Lengo pia ni kuwa sisi kwa sisi tutasaidiana kufanya utafiti kila mkoa bila kusafiri. Mfano kuna habari nimepata kuwa kuna mkoa mmoja ndizi zinaharibika, wanatafuta njia vipi wanaweza kuzisambaza ndizi hizo maeneo yenye uhitaji au hata kuzisindika. Ndizi tunaweza kuzalisha mikate, unga, Biscuits, Chapati etc. Sasa tukifanya haya mambo kama timu..huna haja ya kwenda Kyela, bali ni kwamba mwanachama wa Kyela anaweza kukupa taarifa kuhusu hali halisi ya masoko, bidhaa mbalimbali na fursa huko mwanza.
Hiyo kitu haiwezi kutokea mpaka tujengwe kiukaribu, kwa kuwa na tamaduni ya kusaidiana sisi kwa sisi, kuwa na tabia ya kuwa sababu ya mafanikio kwa wengine. Wengi wetu ni wabinafsi, lakini kupitia Fursa 101 tabia mpya itazaliwa.
Tunaendelea, baada ya Richard na wenzake kugundua fursa hii , wakaenda Rwanda, Uganda na Kenya …ukweli waligundua gap kubwa. Kulikuwa na uhitaji wa solar power kupita maelezo. Hapo ndipo Richard alipoacha kazi na kuanzisha kampuni ya Cellulike.
Alinunua units 50 za mifumo ya solar, na kuanza kuunganisha. Wameweza kuunganisha nyumba zaidi ya 200 kwa mifumo ya solar. Na zaidi ya mifumo ya taa 508 katika maeneo ya mwanza, Kagera na mikoa mingine.
Kampuni hiyo inafanya vizuri sana na wanatengeneza mamilioni ya pesa kupitia fursa hii. Hebu fikiria Richard kutoka Kenya amegundua Fursa hii na kutajirika hapa hapa Tanzania…ni kitu gani kinatuzuia watanzania?
Mimi ninalipa deni kuwaambia ukweli…utafiti huu hautapotea bure. Nina imani wapo matajiri watakaozaliwa…kupitia haya, lakini wale wanaosoma haya kama simulizi za akina Shigongo Mungu hatawaacha salama
Tuligusia mambo kadhaa kuhusu fursa ya Nishati ya jua. Na nikatoa mfano wa Richard aliyekuja kutoka Kenya na kufanikiwa hapa hapa Tanzania tukiwa tunamuona.
Najua watu mtaniuliza…sasa Geophrey ni vipi mtu anaweza kuanza biashara hii katika Fursa ya Nishati ya jua?
Najua Fursa hii muda mwingine inahitaji mtaji mkubwa tofauti na Fursa nyingine tulizogusia, ingawa kuna Niche markets(soko maalumu) ambazo unaweza kuanza na mtaji mdogo tu kama Fursa nyingine.
Source: Fursa 101 whatsapp group
No comments:
Post a Comment