Na Mwandishi wetu
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
Habari Rafiki, kwanza Napenda kukupongeza sana kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa masomo haya natumaini yanakuwa msaada mkubwa kwako na yafanyie ili kuhakikisha unafikia malengo yako makubwa ya maisha yako, leo nimekuandalia somo ambalo nilisha wahi kulitoka lakini kutokana na watu wengi kuomba niwaandalie mchanganuo wa ufugaji wa kuku mia moja japokuwa nimekuwa bize sana na majukumu ya kazi lakini kwa kuona umuhimu mkubwa wa wewe rafiki yangu nimeamua kukaa chini kukuandalia mchanganuo huu ambayo unalenga kukupa uelewa mzuri katika kuweka mipango yango ya bajeti katika ufugaji wa kuku.
MCHANGANUO WA UFUGAJI WA KUKU MIA
Katika ufugaji wa kuku kuna gharama za aina mbili gharama za moja kwa moja na gharama za uendeshaji,
Tunapozungumza gharama za moja kwa moja ni zile gharama ambazo unatumia kwaajiri ya ujenzi wa banda, gharama za Vifaranga na vyombo Vya bandani hizi ni gharama za moja kwa moja au gharama za jumla.
Gharama za uendeshaji ni gharama ambazo zinahusu chakula na madawa hizi ndizo tunazoenda kuangalia siku hii ya leo.
Katika masomo yaliyopita katika sehemu ya ishirini tulijadili kwa undani kuhusu jinsi ya kuandaa mchanganuo wa ufugaji na katika upande wa chakula tulijifunza aina mbalimbali za chakula ambacho tunaweza kuwapa kuku wetu, sasa leo sina mda wakuchambua kuhusu vipimo Vya chakula cha kuku kwa mda wa kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja. Hapo juu nimekutumia somo ambalo nilieleza kuhusu mchanganuo wa vipimo ambavyo kuku wanakula kulingana na umri wao,
Kuku mmoja kifaranga kwa mda wa mwezi mmoja anakula gramu 700 hivyo kwa Vifaranga mia moja watakula gram 70000 ambazo nisawa na kilo 70,
Hivyo kwa mda wa mwezi mmoja kuku wetu watakuwa wametumia chakula kilo 70, ambacho tukiweka kwenye hesabu za kifedha tutapata kama ifuatavyo.
*CHAKULA CHA KUNUNUA MOJA KWA MOJA DUKANI*
👉kwa bei ya wastani ya chakula cha kuku kwa maeneo mengi ya nchi yetu huzwa kati ya 45,000 hadi 62,000 chakula cha kilo 50, hivyo katika mchanganuo wetu tutatumia Elfu hamsini (50,000) japo wewe Rafiki unaweza kuweka bei kulingana na maeneo yako. Ikiwa chakula cha kuku kwa mfuko tutanunua kwa 50,000 Basi kilo mmoja nisawa na 1000.
👉Sasa Basi tukija kwenye hesabu zetu za kuku ambapo kwa kuku mia moja tulipata kujua kuwa wanakula kilo 70. Kwada wa mwezi mmoja tukiweka kwenye hesabu zakifedha tutapata 70,000.
Hivyo tunahitimish kwa kusema kuwa kwa kuku mia watumia gharama ya 70,000 kwa mda wa mwezi mmoja. Bei hii kama chakula tutanunua moja kwa moja dukani,
*CHAKULA CHA KUTENGENEZA WEWE MWENYEWE
Katika masomo yaliyopita tulijifunza jinsi yakutengeneza chakula cha kuku kulingana na umri wa kuku ambao wanao pia nilieleza kwa undani faida za kutengeneza chakula cha kuku, kwakuwa mambo yote hayo nilisha yaeleza katika masomo yaliyopita leo sina haja yakuyaeleza tena. Ili kuweza kutengeneza chakula cha kuku rejea katika masomo yaliyopita ili nimeeleza kwaundani zaidi jinsi ya kutengeneza chakula. Leo ninakupa mahesabu tu ambayo kama utaenda kutengeneza chakula cha kuku wewe mwenyewe.
👉ukirejea katika mchanganuo wetu wa chakula cha kuku wa Mda wa mwezi mmoja nilieleza michanganuo mbalimbali sasa chukua ule mchanganuo wa DEBE 12 ambao ndio nitakao utumia hapa leo.
👉grama za michanganyiko wa chakula ni 57000
👉pumba debe 6 tukiweka katika thamani ya Pesa debe moja huuzwa 1000 hadi 2000 sasa sisi tutatumia bei ya jumla ambayo kwa maeneo mengi huuzwa hivyo ni 2000, hivyo tukizidisha kwa debe sita tutapata 12,000
👉mahindi ya kupalaza kilo 70, kwa bei ya mahindi kwa sasa kilo moja nikati ya 250 hadi 500, sasa sisi tuweke 400 hivyo tukizidisha kwa kilo 70 tutapata 28,000
👉mashine utapalaza kwa 2000
Jumla ya chakula chetu ni 99000
👉jumla ya gharama zote za kutengeneza chakula ni 99,000 Tsh.
👉mchanganyiko huo utatoa jumla ya chakula kilo 178.
👉hiki ni kiasi cha wastani kwasababu pumba nimeweka debe moja utapata kilo 10 kwa wastani kulingana na upimaji wa pumba kwa maeneo mengi ila ukipima pumba vizuri debe moja utapata kilo 11 hadi kilo 13 ila sisi tumeweka kipimo cha wastani ambacho ni kilo 10.
👉ili kupata bei halisia ya chakula hiki kwa kipimo chakilo tutachukua gharama ya Pesa tuliyotumia ambayo ni 99,000 tutagawanya wa kilo 178 zilizopatikana tutapata bei ya kilo ni 556 Tsh.
👉kwa mahesabu tukadilia 600 ili iwe hesabu nzuri ambayo tutakuwa tunaitumia mala zote.
👉kwa kifupi katika eneo hili nihitimishe kwa kusema kuwa chakula cha kutengeneza mwenyewe kina gharimu 600 kwa kilo.
👉kwa chakula cha kutengeneza kitagharimu 42,000/= tu.
*MWEZI WA PILI
Vifaranga Vya miezi miwili mia moja wanakula chuakula kilo 123
👉Kama tutanunua dukani kitatugharimu 123,000 Tsh.73800 hivyo kwa wastani tuweke 74000Tsh.
👉Tukitumia sayansi ya kutengeneza Hydroponic fodder na Azolla tutatumia jumla ya 50000
*MUHIMU
Ninaposema kutumia sayansi simaanishi unatumia Azolla na hydroponic fodder peke yake Bali ninachomaanisha nikwamba utawapa chuakula cha kutengeneza dukani na pia utatumia Hydroponic fodder na Azolla kama chukula cha ziada na siyo chakula hicho tu.
👉unachotakiwa kufanya ni kuwa kama kuku wako ni mia moja ambao kwa wastani wanakula kilo 130 kwa siku sasa wewe utakaye wapa Azolla na hydroponic dodder utawapa kilo nane hadi kumitu na hizo zilizobaki utawapa hydroponic na Azolla hiki cha ziada hakikisha hakipungui kilo nane.
👉kilo hizo nane kwa hydroponic utahitaji nusu kilo tu ya ngano na Azolla utahutaji eneo la meta mbili kwa tatu. Kiasi mbacho utatumia kuzalisha chakula hiki hakizidi 1000Tsh.
*MWEZI WA TATU
Kwa kuku mia kwa mwezi WA tatu watakula chakula kilo 173.6
👫👉kama tutanunua dukani tutatumia 173600Tsh,
👉kama tutatengeneza wenyewe tutatumia jumla ya 104000Tsh.
👉kama tutatumia sayansi tutatumia jumla ya 7000Tsh.
*MWEZI WA NNE
Kuku mia wanakula chakula kilo 217
👉kama tutanunua chakula dukani tutatumia gharama ya 217,000Tsh.
👉kama tutatengeneza chakula tutatumia gharama ya 130000Tsh.
👉kwa kutumia sayansi 90,000Tsh.
*MWEZI WA TANO
Kuku mia wanakula chakula kilo 271.6 kwa mda wa mwezi mzima.
👉chakula cha kununua dukani kitagharimu 271600
👉Chakula cha kutengeza kitagharamu 163000Tsh
👉kwa kutumia sayansi 100,000Tsh
*MWEZI WA SITA
Kuku kwa mwezi WA sita wote watatumia chakula kilo 343
👉kama utanunua dukani utatumia 343,000/=
👉kama utatengeneza mwenyewe utatumia 206000Tsh.
👉kama utatumia sayansi utatumia 150,000Tsh.
*MWEZI WA SABA
Kuku mia kwa mda wa mwezi WA sita wote watakula kilo 403.
👉kama utanunua chakula dukani kitakugharimu 403000Tsh.
👉kama chakula utatengeneza kitakugharimu 242000Tsh.
👉kama utatumia sayansi kitakugharimu 180,000Tsh.
*MWEZI WA NANE
Kuku mia kwa mwezi wa nane wote watatumia chakula kilo 403
👉kwa chakula cha dukani itatugharimu 403000Tsh.
👉kwa chakula cha kutengeneza kitagharimu 242,000Tsh.
👉kama utatumia sayansi itakugharimu 180,000
Baada ya kuangalia gharama ya chakula kwa mda wa miezi nane kwa mda wa mwezi mmoja mmjoa sasa twende tukajumlishe ili tupate hesabu ya jumla kwa upande wa gharama za uendeshaji.
👉kabla ya kuangalia gharama za jumla tuongeze gharama za chanjo na tiba kwa kuku wetu,
Kwa mda wa miezi nane kuku wanatumia gharama ya 137500 hii ni kwaajiri ya chanjo na madawa kwaajiri ya vitamini na kuuwa wadudu. Sasa katika ufugaji wa kuku nimuhimu kuwa na Pesa ya dharula hii utaitumia lape kuku wako watakapo ugua na katika mchanganuo wetu tunaweka 100,000Tsh. Hivyo jumla ya Pesa kwaajiri ya tiba na chanjo ni 237500Tsh.
✍Baada ya kuona mchanganuo huo sasa twende tukahitimishe jumla ya mchanganuo wa gharama za uendeshaji kwa kuku mia, tutachukua gharama za chakula tutajumlisha na gharama za madawa.
✍Kwa chakula cha kununua dukani ni 2004000+ gharama za madawa kwamaana ya tiba, chanjo na dharula kwa ujumla wake tukaweka 237500=2241500
✍kwa chakula cha kutengeneza 1203000+237500=1440500Tsh.
👉kwa kutumia sayansi 866000+237500= 1103500Tsh.
👉hapa nimefika mwisho kwa somo la Leo natumaini mchanganuo huu utakusidia sana katika kuweka mipango yako sawa kabla ya kuingia katika ufugaji
👉Mchanganuo huu unaweza kutumia kwa idadi yeyote ya kuku kwa kuongeza au kupunguza idadi ya kuku.
NI MIMI RAFIKI YAKO
FRANK MAPUNDA
UNAWEZA KUWASILIANA NAMI KWA NAMBA
0758918243/0656918243
KWA MAHITAJI YA VIFARANGA CHOTARA VINAPATIKANA POPOTE PALE ULIPO (UTAKAPOCHUKUA VIFARANGA KWETU UTAPATA NAFASI YA KUSIMAMIWA KATIKA UFIGAJI WAKO KWA KIPINDI CHOTE CHA UFUGAJI WAKO)
PIA TUNAUZA MASHINE ZA KUTOTORESHEA VIFARANGA (INCUBATOR) ZIPO ZA UMEME NA ZAFUTA YA TAA KARIBU SANA.
KITABU CHA TAJIRIKA KWA KUKU SASA KINAPATIKANA KATIKA MFUMO WA SOFT COPY
KITABU KINAUZWA KWA BEI YA 7000/=
ILI KUPATA KITABU HIKI FANYA MALIPO KWENYW NAMBA KATI YA HIZO
0758918243/0656919243
MAJINA YATATOKEA; FRANK MAPUNDA
BAADA YA KUFANYA MALIPO NITUMIE E-MAIL YAKO NAMI NITAKUTUMIA KITABU.
TUPO PAMOJA KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
No comments:
Post a Comment