Na mwandishi wetu
Leo tuangalie kuhusu vitamin B :Upungufu wa vitamin B imekuwa ni tatizo kubwa sana kwa sababu vitamin B ni water soluble vitamin hivyo it disolve in water .kwa hiyo haina storage kwenye mwili hivyo mlaji anapaswa kula kila siku chakula chenye vitamin B kwa wingi.
Na huwa inatoka mwilini kwa njia ya mkojo, haja kubwa, jasho, hivyo kufanya watu wenye kisukari wawe na hatari kubwa ya upungufu wa vitamin B, watoto, wajawazito, wanaonyonyesha.
KAZI YA VITAMIN B MWILINI NI :
#Kusaidia mwili kufanya kazi sawasawa hasa katika mfumo wa chakula,kinga,na fahamu.
# Huwezesha moyo na misuli kufanya kazi kwa ufanisi.
#Husaidia kutengeneza seli mpya na kukarabati seli na neva na seli nyekundu za damu.
VYANZO VYA VITAMIN B
Maini, viazi, maziwa, nafaka zisizokobolewa, vyakula vya jamii ya kunde, uyoga, karanga, mayai, kuku, samaki, nyama, matikiti, parachichi, ndizi mbivu, chungwa, mboga za majani, mbegu za alizeti, maboga, korosho, na vyakula vilivyochachushwa kama togwa au mtindi.
ZIFUATAZO NI DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMIN B MWILINI.
@ Kunyongea na kusikia uchovu.
@ Kukosa hamu ya kula.
@ Kupungua uzito.
@Maumivu mwilini.
@ Moyo na mfumo wa chakula kushindwa kufanyakazi vizuri.
@Mfumo wa fahamu kushindwa kufanyakazi vizuri.
@Vidonda kwenye kona za midomo.
@ Kuharisha.
@ Magonjwa ya ngozi.
@ Kuchanganyikiwa, kukosa usingizi.
@Kuumwa kichwa mara kwa mara.
@Upungufu wa damu.
Kwa msaada zaidi kuhusu ulaji unaofaa wasiliana na Jehsha Health Food and Drink kwa namba 0757295056.au
jhealth.food@gmail.com
No comments:
Post a Comment