Na Geophrey Tenganamba
Mimi ni sababu ya mafanikio yako. Wewe ni sababu ya mafanikio yangu. Kutoka fursa 101.
Mnamfahamu dogo mmoja anaitwa Abbas Maziku? Hapa ni fursa ya ku export. Mnamfahamu huyu kijana Abbas?
Abbas Maziku- nilikutana naye mwaka jana Huyu kijana ni mfanyabiashara wa kimataifa. Wengi wetu tunafanya biashara za kuunga unga kwasababu hatuna roho ya uthubutu.Tunaogopa kwenda kimataifa. Sijui ni lugha.. Sijui ni shetani gani huyu.
Unajua Abbas alianza biashara mwaka gani? Alianza 2013, kwa mtaji wa Tsh.2Milioni. Alianza kwa kununua korosho, ufuta, mbaazi, choroko, mtama, alizeti, mashudu ya pamba na pilipili manga. Aliyanunua mazao hayo kidogo kidogo na kuyauza kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima pamoja na minada ya mashirika ya umma huko Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida etc. Kutoka mtaji wa 2MILIONI mpaka million 200 na zaidi. Hivi karibuni amepewa $100,000 kama grants
Anachokifanya Abbas ananunua mazao hayo yote, anayafungasha vizuri kwa kusaidiana na vibarua kisha anaweka nembo ya kampuni yake. Baada ya hapo anapeleka sampuli katika maabara za kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS na ndipo hufuatia hatua ya mwisho ya usafirishaji wa mazao hayo kupitia meli za mashirika mbalimbali ikiwamo IPTL, MAERSK na nyinginezo kupeleka VIETNAM.
Zipo taratibu nyingine anazozifuata ikiwemo kulipia TRA, watalaamu wizara ya kilimo na ufugaji, wanasheria, maofisa usalama wa taifa nk. Hapa TBS wala TFDA hawahusiki. Hapa ukiamua kufanya utafiti wa mazao na masoko ya nje umetoka.
Jambo moja niwaambie ndugu zangu- fursa ya ku export bidhaa nje, pamoja na fursa zote zina changamoto. Asili yetu sisi binadamu tumeumbwa kuja kupambana na changamoto. Na kuzishinda. Binadamu yeyote anayekimbia changamoto anajijengea makaburi yake mwenyewe.
Unaweza ukajiona upo salama kwasababu huja risk kufanya kitu. Nakuambia ukweli unayapoteza maisha. Abbas aliniambia, alipoanza biashara mara ya kwanza alipata hasara kubwa, baada ya kuonekana mazao yake hayakuwa kwenye kiwango kinachotakiwa. Alipoteza pesa zote alizokopa benki. Unadhani aliishia hapo? Aliendelea- mpaka alipotengeneza milioni 200.
Mizigo inayoandaliwa kusafirishwa....
Kampuni zake ni Agromart Company Ltd na Lyone Investment . Ameweza kujenga ghorofa, anamiliki magari na anasafiri nchi mbalimbali kwenye makongamano. Labda nikuulize kwanini usijifunze kupitia mfano huu? Unadhani Abbas Maziku alizaliwa mwaka gani? 1990. Ndoto zake ni kumfikia Dewji. Hebu fikiria ni kitu gani kinachokuzuia?
No comments:
Post a Comment