Sunday, May 27, 2018

Zinedine Zidane ni nani kwa Liverpool FC?

Na Adimu Nihuka Jr
Zinedine Zidane na Nadharia za Ashindikene na Nchimbo wa Jika.
Zinedine Zidane ni jina maarufu sana kwenye wigo wa soka. Ni jina lililojizolea umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 90 had mwanzoni mwa 2000 halafu likapoa kidogo na kulipuka tena miaka mitatu iliyopita, tena limelipuka kuliko volcano yoyote iliyowahi kutokea ulimwenguni.

Zidane ama Mfalme kama wanavyomtambua wafaransa wenzie, miguu yake ilikuwa na kila kitu kinachohitajika kwenye Soka, kimombo tungeweza kusema he was a complete player. Anapiga pass accurate, anadribble vyema, anaruka juu ile mbaya, anapiga mashuti, anamark, anachenga za maudhi yaani anakila kitu. Fainali ya kombe la dunia 1998 alitumia kichwa chake kuwaadhibu Brazil na fainali ya mwaka 2006 akatumia kichwa chake kumuadhibu Materrazi.

Nadharia ya Ashindikene kwa makabila ya kusini hutumika kumaanisha MTU asiyewezekana, yaani kwa kimombo you can't compete with him. Zidane ameshindikana, hawezekani, ni kuachwa tu afanye anachotaka. Makocha wetu hawa wooteeee tunaowasifia kwa mifumo na mbinu mbalimbali wameshindwa japo tu kulichukua Mara mbili mfululizo ukiachana na akina Wenger ambao hawajawahi japo kuligusa.

Zidane ametuonya uwanjani na sasa anatuonya akiwa kwenye bench, tunapaswa kumuunga mkono tu hakuna jinsi.
Zidane pia ni Nchimbo wa Jika. Dhana ya Nchimbo wa Jika kwa Kiyao inamaanisha Nyani dume aliyepevuka na kukomaa had akafikia hatua ya kutembea peke yake.

 Inajulikana nyani huwa na mazoea ya kutembea kwa mafungu, lakini Nchimbo wa Jika anatembea peke yake na Zidane amefikia hatua hiyo tangu akiwa mchezaji had sasa akiwa kwenye bench. Team ya taifa ya Ufaransa kwa miaka kadhaa ilijengwa kupitia yeye, Zidane alikuwa dictator uwanjani, anaiendesha timu anavyotaka.

 Angeweza kupiga ile chenga yake ya kupanda ball hata mbele ya watu watatu, angeweza kummwagia majalo Henry hata akiwa katikati ya uwanja yaani anafanya lolote. Kama alivyofanya Jana tu kamrudisha Isco bench na kumtupa Bale ground huku akiwa na maelekezo 106 ya dictator Zidane. Kilichotokea wengi tunakifahamu.

Hiki kinachofanywa na Zidane nusu yake angefanya Mourinho wetu tusingelala, angefanya Pep muda huu angekuwa anaandika barua ya kujiuzulu lakini angefanya Conte ndio ingekuwa balaa. Lakini kwa bahati nzuri aliyefanya ni MTU ambaye anamahusiano na dhahabu, anaundugu na makombe, anadamu ya mafanikio anaitwa Mfalme tangu miaka 20 iliyopita.

Wapo watakaomlaumu Ramos, wapo watakaomlaumu Karius na wapo watakaosema Sallah hakuwepo lakini mwisho wa siku mchawi ni huyu Zidane.

NB: Alichokifanya Ramos kiutawala kinaitwa Sterling by Force na MTU wa mwisho kukifanya alikuwa Komando Kipensi kwenye ile movie yake ya kutisha.

Imeandaliwa na Kindamba Namlia

No comments:

Post a Comment