Na mwandishi wetu
Kipindi nilipohamia Morogoro na kuanzisha Chuo , huwa nina utaratibu huu, ikitokea nimehamia sehemu Fulani lazima nitafute sehemu ya kuabudu yaani kanisa. Nikapata kanisa moja maeneo ya kihonda. Nilimpenda sana mchungaji wa lile kanisa alikuwa na bidii sana kwani alikuwa akiwatembelea waumini wake na kuwaombea biashara zao nk.
Sasa kulikuwa na dada mmoja mzuri sana, alihamia kutoka Arusha. Akafungua duka sehemu moja changanyikeni, ina waswahili wengi. Ni sehemu pekee kibuku ilikuwa inauza pombe zake za kienyeji kwa wingi, pia ukipeleka mitumba ya bei rahisi unauza sana. Zaidi ukitaka kuuza hiyo sehemu peleka vitu feki kwa bei ya chini, utauza sana.
Sasa dada huyo, alishawishiwa na Rafiki yake ambaye ametengeneza pesa si mchezo kupitia sehemu hiyo. Dada huyo akafungua duka la urembo, vipodozi na bidhaa mbalimbali original kabisa. Ofisi yake akaweka na AC, akaweka rangi nzuri sana. Ofisi ilikuwa ina pendeza sana.
Haya sasa, huyo dada nilikutana naye kwa mara ya kwanza kanisani kwa mchungaji huyo. Huyo dada alikuwa mtoaji mzuri sana kanisani, lakini kila siku alikuwa akilia sana, hapati mauzo kabisa kwenye duka lake. Hivyo basi mchungaji wetu alikuwa na utaratibu wa kwenda kuombea biashara yake kila jumamosi. Muda mwingine mchungaji alitumia mafuta ya upako, maji ya baraka nk lakini bado mauzo ya yule dada yaliendelea kushuka sana.
Siku moja, mchungaji akasema vijana wote twendeni tukaombee biashara ya yule dada. Mimi pia nilienda, tukaongozana, tulitembea kwa miguu na nikapata nafasi ya kujua mitaa na watu wanaoishi mitaa ile. Ukweli nilipofika dukani nilifurahi sana, duka lilikuwa zuri sana sana.
Mchungaji na vijana wengine walianza kuomba sana, ukweli mimi sikuomba nilikuwa napiga kelele tu huku naangalia bidhaa za lile duka. Baada ya maombi dada wa watu alinunua maji na juisi kwaajili yetu, kisha tukaanza kutoka.
Mimi nikabaki nyuma, nikamvuta yule dada mkono na kumsogeza pembeni nikamwambia haya:
“Acha kusumbua wachungaji , hama huu mtaa”
Akauliza
“Sikuelewi mpendwa”
Nikajibu:
“Hakuna anayeloga hii biashara yako, ukweli ni kuwa biashara yako imezungukwa na wateja wasio sahihi. Hamisha hii biashara , tafuta mtaa mwingine, huu mtaa hakuna wateja wako”
Yule dada aliniona nisiye wa kiroho, akamwambia mchungaji pia, nikaitwa na kuombewa.
Miezi mitatu baadaye, nikapokea simu alikuwa yule dada akaniuliza,
“Unajua sehemu nzuri naweza kuhamishia biashara yangu?”
Nikamwelekeza, lakini sehemu hiyo ilikuwa gharama sana. Nikamwambia, chukua hiyo sehemu hata kama ni gharama. Akahamishia biashara yake sehemu hiyo. Mimi baadaye niliondoka Morogoro na kwenda Arusha, nikiwa Arusha baada ya miaka kama miwili nikapigiwa simu na yule dada, amefungua tawi lingine la vipodozi mwanza.
Akaniambia kuwa ile sehemu aliyohamia ilimfanya akue kibiashara na kupata mwanaume wa Maisha yake, ambaye kwasasa wanasaidiana kwenye biashara. Last week nikaonana nao ambapo walinisimulia love story ambayo, mimi pia nimehusishwa kama mhusika niliyewafanya wakutane.
Ujumbe wangu ni huu: Change your position.
Hebu fanya inventory ya wateja wako, marafiki zako waliokuzunguka na aina ya biashara.
Umeanza biashara, lazima utengeneze list kwanza ya watu wenye hela zako. Kisha andaa bidhaa ya kuwauzia ili wakupe hela yako. Ikitokea upo mtaa ambao hakuna watu wenye hela zako , hama.
Hata kama ni social media, ikitokea tangu uingie social media hakuna watu wenye uwezo wa kununua bidhaa au huduma yako, badilisha marafiki.
Ukizungukwa sana na watu ambao hawawezi kulipia bidhaa yako, kuna siku utajikuta huna uwezo wa kulipia mahitaji yako.
Ukienda kwenye networking event, tumia muda mwingi na watu wenye hela zako. Ninaposema watu wenye hela zako simaanishi matajiri wakubwa bali potential customers. Kuna watu maarufu nikikutana nao siwezi kuhangaika kukaa nao kwa muda mrefu, usishangae kunikuta nipo na mtu wa kawaida sana kwasababu huyo ni potential customer kwangu.
“Be nice to everyone but spend most of your time with people who have your money”
NOTE: TUPO KWENYE PILOT PHASE, PAKUA APP YA FURSA 101 SHOPPING KWENYE SIMU YAKO, KISHA TOA ODA YA BIDHAA KUTOKA SHAMBANI, UTALETEWA MAHALI ULIPO, NA BAADA YA HAPO KUNA ZAWADI HASA KAMA SI MWANACHAMA FURSA 101.
Geophrey Tenganamba.
0655973248
No comments:
Post a Comment