Na Geophrey Tenganamba:
Hebu tukumbushane kuhusu biashara na mteja.
Kila biashara ipo kwaajili ya kuuza.
Kumuuzia nani? Mteja of course.
Biashara isiyouza mwisho wake kifo.
Kila mwaka mamia ya biashara zinakufa kwasababu haziuzi.
Kwanini?
#1. Unaanza biashara bila kujua uhitaji wa wateja.
"No need, no sales"
Hakuna anayetaka kununua kitu asichokitaka. Wewe umekurupuka huko sijui umesikia kuna mtu ametajirika kwa kuuza mayai ya kunguru.
Ndugu umefanya utafiti kuhusu uhitaji?
Unajua wateja wake?
Kosa utakalolifanya kibiashara ni kuuza kisichohitajika , utanunua mwenyewe.
Mfano gari yangu imejaa mafuta full tank na unataka kuniuzia lita 30, utakuwa unapoteza muda wako. Siwezi kununua nisichokihitaji.
Hata kama nina hela ya kununua hayo mafuta sintanunua.
#2. Chunguza wateja wako, wana hela kwenye mifuko?
"No money, no sales"
Mimi sina uwezo wa kununua saa origino Rolex. Wewe umekuja kunipigia kelele ninunue ....umetumwa?
Hata kama ninaipenda hiyi saa nitaishia kusema saa nzuri kweli.
Nitaitamani sana lakini wallet imechanika.
Ukiwa mfanyabiashara jifunze kuangalia wallet. Itakusaidia.
Wewe upo group la wanafunzi wa chuo unatangaza nyumba ya milioni 300. Upo serious kweli?
Au tufanye kweli nina uhitaji , nyumba yangu imekutwa ina panya wengi sana. Ukaja na dawa ya panya, nikakuuliza bei, ukasema Millioni kumi. Hivi unadhani nitanunua. Kuna watu wa kununua siyo mimi. Mara kumi nitenge siku moja nianze kuua panya mmoja mmoja kwa mpini wa jembe lakini siyo dawa ya millioni kumi.
Jifunze kutofautisha soko lako. Uwezo wa mteja wako.
#3. Jifunze kumharakisha mteja. Ukimpa muda sana ataghairi.
"No hurry, no sales"
Umewahi kukutana na matangazo ya kiingereza “Buy now at 40 percent discount. Offer valid for 30 days only!” ?
Mteja anasema nipe muda wa kufikiria unamwacha kweli?
Akufikirie wewe kwani mpenzi wak
Tabia za watu hubadilika kwa muda. Ukimpa muda imekula kwako. Jifunze kupresharaizi.
#4. Kuwa mhamasishaji, kuuza ni kuhamasisha.
"No desire, no sales"
Ili mteja anunue lazima umhamasishe kwa kutaja faida ya kitu unachouza. Mfanye aone bidhaa yako ni suluhisho la matatizo yake.
Kama amevunjika moyo, mtie moyo. Amepoteza matumaini mpe matumaini. Kama kuna tatizo alilonalo na unadhani unaweza kumsapoti, toa msaada.
Siyo unafika....
Oyaa nunua necklace Tsh. 5000 tu.
Nauza na bangiri. Nunua sasa.
Ndugu yangu hata maneno matamu huna.
Sinunui ng'o.
Niishie hapa.
Source: Fursa 101 whatsapp group
No comments:
Post a Comment