Na Adimu Nihuka Jr.
M
|
aumivu ya chini ya kitovu kwa mwanamke na
mwanaume kitaalamu huitwa lower abdominal pain ni tatizo ambalo huwakumba watu
wengi lakini kwa bahati mbaya wengi hulichukulia kuwa ni jambo la kawaida kitu
ambacho baadae husababisha wagonjwa wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya
kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.
Maumivu ya chini ya kitovu yapo yale ya chini
yake, katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo
ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa ya upande mmoja lakini husambaa kwa
urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili
lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au
pande zote mbili bila kusambaa kwa urefu.
Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata
wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya
kitovu. Pia yapo ambayo huwapake wakati wameinama, wakati wa kunyaynyua vitu
vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala
kifudifudi.
Maumivu chini ya kitovu yanaashiria matatizo kwa
wanawake kama vile mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia
yai kutembea kwenye mirija ua uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na
daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake au mirija ya uzazi na wakati
huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna
uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji
machafu.
Lakini pia maumivu hayo yanaashiria kutokukomaa
kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba ovaritis
na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithiri ya kichomi.
Mwananmke ambaye anamaumivu chini ya kitovu na
wakati huo huo ana matatizo ya hedhi kukoma au kutoka kwa mpangilio maalum kuna
uwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuka vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza
mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na
hatimaye humsababishia mwanamke maumivu makali au kitu kama kichomi.
Pia humsababishia kuvimba kwa kuta za mji wa
mimba na kuta za mirija ya uzazi yaani Pelvic inflammatory Disease(PID).
Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu, katikati na pembeni lakini pia
akawa anatokwa na uchafu mzito mithiri ya maziwa mtindi kuna uwezekano akawa na
PID hasa kama amawahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla
haijafikisha miezi mitano.
Ieleweke kuwa maumivu chini ya kitovu
yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja
ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.
Mumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia
tatizo la tenzi dume liitwalo prostatitis yaani kuvimba kwa tenzi dume. Mumivu
haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili hasa kama mwanaume
anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa unaelekea
miaka 50 au zaidi.
Dalili nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo
ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na maumivu kiuno na
mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na usaha na damu,
maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni na dama maji ya uzazi.
Kwa wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu
huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu huulikana kwa jina la hernia ambayo
waswahili huita ngiri. Mwanaume anaposiia maumivu haya ya chini ya kitovu
ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua
zaidi au zote mbili kukua au kupotea ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu
ubora wa uzalishwaji wa megu za kiume ambazo zaweza kuzalisha chache au ambazo
hazina kasi ya kutosha ya kusafiri kwenye via vya uzazi vya mwanamke na hivyo
mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume kama ilivyo
kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfuko wa haja ndogo yaani
Urinary Track Infection(UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za mwanamke hapo
juu.
HITIMISHO
Vipimo vya tiba vyahitajika mapema bila
kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa
chakula.
Chanzo: Gazeti la Ijumaa
wikienda(April 03-09, 2017); ukurasa wa 13.
No comments:
Post a Comment