Tuesday, November 28, 2017

Tuwe makini na msimu huu wa sikukuu wazazi

Msimu wa sikukuu hasa krismas na mwaka mpya upo njiani unakaribia hivyo wazazi tuwe makini sana, kwasababu tusijisahau kuwa januari kutakuwa na mambo mengi mapya ambayo yanahitaji fedha.

Pia kutakuwa na ulazima wa kulipia ada kwa watoto wetu, shughuli za mbolea na nyinginezo katika shamba, na mambo kadhaa. Hivyo nawapa tahadhari kuwa msisherehekee hizi sikukuu kwa mbwembwe yingi na mkasahau kuwa kuna maisha baada ya hizi sherehe. 
Pia nawatakia mema katika maandalizi ya hizo huduma za kijamii na kifamilia ila mkumbuke kuwa kuna maisha baada ya sikukuu kupita.

Watu tunaadaa mashamba na pembejeo zake hivyo zisitufanye tuwekeze fedha kwaajili ya sikukuu pekee.

No comments:

Post a Comment