Hapa tutajifunza vifuatavyo:-
Ø Maktaba
ni nini?
Ø Historia
ya Maktaba
Ø Aina
za Maktaba
Ø Namna
ya kutumia Maktaba
Ø Faida
za Maktaba
Maktaba ni nini?
Maktaba
ni chumba au nyumba ambamo:-
Ø Vinahifadhiwa
vitabu, majarida, magazeti, kompyuts, n.k.
Ø Vifaa
vyote vimehifadhiwa katika mpangilio maalum ili msomaji apate mahitaji yake kwa
urahisi.
Ø Chini
ya uangalizi na mtu mwenye utaalamu katika fani ya ukutubi.
Historia ya Maktaba
Maktaba
zilikuwepo toka zama za kale- binadamu walipoanza kuandika miaka 5,500
iliyopita.
Watu
wa kwanza kabisa walikuwa:-
Sumerians (Mesopotamia):
Iraq, Syria na Uturuki. Hawa walitumia vitabu vilivyotengenezwa kwa udongo
(Clay tablets), vibao viliandikwa vibichi na kukaushwa.
Wamisri
(Egyptians): Wao walitumia papyrus (mafunjo) aina ya mkeka
uliotengenezwa kwa kupondaponda nyasi za mto Nile. Baadaye walitumia ngozi ya
wanyama hasa ndama na kondoo(Velium na Parchment)
Wachina
walikuwa wakwanza kugundua karatasi mwaka 105 A.D Maandishi yake haya
yaliyohifadhiwa pamoja katika maktaba. Waliotumia maktaba hizo ni ukoo wa
wafalme na viongozi wa dini.
AINA ZA MAKTABA
Kuna
aina mbalimbali za maktaba lakini humu nazungumzia aina mbili tu za maktaba,
nazo ni:-
· Maktaba za shule na vyuo.
Maktaba
hizi hukusanya na kuhifadhi maandishi na taarifa mbalimbali kwaajili ya;
kujenga tabia ya kujisomea miongoni mwa wanafunzi, kuwaelimisha wanafunzi
katika masomo ya fani mbalimbali, kumsaidia mwanafunzi kuandika mazoezi na
insha, kuhifadhi mahitaji ya walimu na wanafunzi katika masomo.
· Maktaba za Umma
Maktaba
hizi zinahudumia watu wote bila kubaguliwa. Lengo la maktaba hizi ni;
kuhabarisha(current affairs), kuelimisha- vitabu vya masomo mbalimbali ns
kuburudisha- hadithi na kichezo.
NAMNA YA KUTUMIA MAKTABA
Masomo
yote yamepangwa katika mafungu 10, kila fungu limepangwa namba kuanzia 000
mpaka 999 kama ifuatavyo:-
· 000 Mseto wa masomo kama vile kamusi,
Encyclopedia, n.k.
· 100 Falsafa na Saikolojia
· 200 Dini
· 300 Elimu ya Jamii
· 400 Lugha
· 500 Sayansi
· 600 Teknolojia (Ufundi wa aina mbalimbali)
· 700 Sanaa (Michezo, maigizo, miziki)
· 800 Fasihi
· 900 Historia na Jiografia
Vitabu vyote vimepangwa kufuata masomo. Hivyo vitabu
vya somo moja vitakaa pamoja vikiwa na namba zilizofanana. Mfano 200- Dini;
Vitabu vitakaa pamoja katika mpangilio wa 000- 999.
Ili
kupata vitabu:-
· Msomaji
aangalie namba ya somo kwenye rafu za vitabu. Hapo pia kuna lebo zinazoonyesha
jina la somo.
· Msomaji
atakipata kitabu kama kipo maktaba kwa kuwa vitabu vyote vimepangwa kuendanan
na somo husika.
FAIDA
ZA MAKTABA
- · Maktaba zinasaidia wanafunzi kujenga tabia ya kusoma toka utotoni hadi maisha yao yote, hivyo kuwafanya waendane na wakati.
- · Maktaba zinasaidia kutoa mwanga zaidi katika masomo anayofundishwa mwanafunzi daradsani kwa kupata maoni ya waandishi mbalimbali kuhusu somo hilo.
- · Maktaba huwasiadia walimu katika maandalizi ya masomo ya kufundisha darasani na mambo mengine yanayohusu uendeshaji wa shule.
- · Maktaba huwasaidia watu wa aina au kazi mbalimbali, kujkiendeleza kwa kusoma vitabu kuhusu fani zao. Mfano:- Mkulima au wakulima hujifunz kilimo bora ili kuongeza mazao shambani; wafanyakazi husoma ili kupanda ngazi katika sehemu zao za kazi; wafanyabiashara nao husoma ili kupata mbinu mpya za kuendeleza biashara zao; wasio na kazi wanaweza kupata taarifa za ajira katika maktaba kwa kusoma magazeti, n.k.
No comments:
Post a Comment