Thursday, May 31, 2018

Tahadhari kwa wazazi, watoto, na ndugu wote kiujumla

Na Adimu Nihuka Jr
TAHADHALI TOKA UMOJA WA MATAIFA "Imetafsiriwa"
Biashara ya Viungo vya binadamu inashamiri au inaongezeka sana Mashariki ya Kati.

Viungo kama: Figo inauzwa takribani dola $262,000; sawa na sh.milioni 940 za kitanzania.

Moyo unauzwa dola za kimarekani $ 119,000; sawa na shilingi za Kitanzania milioni 430. Na Ini linauzwa dola za kimarekani dola $ 157,000; sawa na Shilingi za Kitanzania shilingi milioni 562.
Kwahiyo Basi, muwe makini na makampuni au mawakala wanaojifanya, kuwatafutia kazi nje ya Nchi.

Ambapo mwisho wa Siku, ukifika huko nje, unauawa, kisha kutolewa viungo vyako muhimu kama hivyo hapo juu na kuuzwa.
Hivyo Basi, ni vizuri watoto wetu na wajukuu zetu wajulishwe hali hii, ili wasiangamia kwa tamaa yakutaka kupata kazi nje ya Nchi.

Tuma ujumbe huu,ili kuweka wazi uovu huu ambao shetani kwa kushirikiana na mawakala wake wanafanya ili kuangamiza maisha ya watu.
Ili kuokoa maisha tuma na kwa mwingine.

Tetesi za usajiri ligi kuu Tanzania VPL

Na mwandishi wetu
-Juma Abdul Akubali kujiunga Azam FC baada Mkataba wake Kuisha..Unaambiwa ni M50 na Mkataba wa Miaka Miwili.

-Wengine ni Kelvin Yondani na Geoffrey Mwashiuya kutua Azam FC.

-Mghana wa Simba James Kotei Kutimka Msimbazi..Afrika Kusini Kunatajwa.. Mbadala wake Unaambiwa ni Papy Tshishimbi wa Yanga.

-Wengine ni Juma Luizio na Laudit Mavugo kutimka Simba.

-Shafiq Batambuze Kwenye Rada za Azam huku Danny Usengimana Kutimua Singida.. Mbadala wake Pichani hapo Mbrazil Felipe Oliveira Dos Santos pia kakipiga pale ASEC Mimosa Ivory Coast.

-Coastal Union Wanamtaka Kijana wao Juma Mahadhi Anaemaliza Mkataba wake Jangwani.

-Feisal Salum "fei Toto" Katua Singida United.

-Tafadzwa Kutinyu Ametua Azam FC Kutokea Singida United...Mbadala wake pale Singida ni Mghana Ernest Kwame Ofori.

*Andrew Vicent kwenye rada za Azam FC pia.

-Piere Lechantre hati hati na Kibarua Chake Msimbazi huenda Akatimua..Kocha Mkuu kuwa Masoud Djuma.

*Beno Kakolanya JKT Tanzania.

*Anko Mrisho Ngassa Mbioni Kurejea Yanga SC..

*Mohammed Ibrahim MO katua Yanga Muda Wowote Kutangazwa Jangwani.

*Beno Kakolanya, Hassan Kessy,Andrew Vicent, Nadir Haroub,Kelvin Yondani, Juma Mahadhi,Obrey Chirwa,Said Makapu,Geoffrey Mwashiuya,Juma Abdul,Emmanuel Martin na Wengine Wamemaliza mikataba yao Yanga.

Wachezaji wa klabu ya Young African waliokwenda kenya kushiriki kombe la SportPesa supper cup

MSAFARA WA YANGA SC KENYA

HAWA ni baadhi ya wachezaji waliosafiri kwenda kesho Leo hii may 31, 2018 kushiriki kombe la sportpesa supper cup litakaloanza kutimua vumbi hivi karibumi na inasemekana mechi za ufunguzi zitachezwa June 03, 2018
1. Youthe Rostand
2. Ramadhani Kabwili
3. Hassani Kessy
4. Buruani Akilimali
5. Haji Mwinyi
6. Pius Buswita
7. Abdallah Shaibu
8. Pato Ngonyani
9. Ibrahim Ajibu
10 . Maka Edward
11. Yohana Mkomola
12. Thabani Kamusoko
13. Mateo Antony
14. Amisi Tambwe
15. Juma Mahadhi
16. Saidi Juma
17 . Said Mussa
18. Papy Tshishimbi
19. Yussuf Mhilu
20. Raphael Daudi

Umuhimu wa kula vyakula mchanganyiko

Umuhimu Wa Kula Vyakula Mchanganyiko .
(MLO KAMILI).

Ni muhimu kula vyakula mchanganyiko kwa sababu baadhi ya virutubishi hutegemeana ili kuweza kufanikisha kazi zake mwilini.

πŸ₯¦πŸ₯¦mfano wa virutubishi vinavyotegemeana ni
πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

🍏🍏MADINI CHUMA NA VITAMINI C :Aina ya madini chuma yanayopatikana kwenye vyakula vya mimea kama mbogamboga za kijani na vyakula jamii ya kunde hufyonzwa kwa ufanisi mwilini iwapo katika mlo huo kuna vitamin C ambayo hupatikana kwa wingi kwenye matunda, mfano chungwa 🍊🍊🍊,Pera 🍈🍈🍈🍈,nanasi 🍍🍍🍍🍍🍍,pesheni ,ubuyu .

πŸ‡πŸ‡πŸ‡ vitamini zinazoyeyuka kwenye mafuta (A, D, E, na K) hutumika kwa ufanisi mwilini kutegemea uwepo wa mafuta katika mlo. Hivyo basi, ni muhimu kutumia mafuta wakati wa kupika hususan mbogamboga πŸ₯’πŸ₯¦πŸ†πŸ₯•πŸ…πŸŒΆ.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu ulaji bora wasiliana kwa namba 0757295056.Afya yako ni jukumu letu.

Monday, May 28, 2018

Lifahamu ziwa Tanganyika

KUHUSU ZIWA TANGANYIKA...

Hili ni miongoni mwa maziwa makubwa na mashuhuri Afrika na Duniani kwa ujumla.

Ziwa Tanganyika linapatikana Magharibi mwa Tanzania likipakana na nchi za Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia.

Sifa za Kipekee;

Ziwa Tanganyika ni la kwanza kwa urefu Duniani (the first longest lake in the world) likiwa na umbali wa kilometa 673 kutoka ncha ya Kaskazini iliyoko Bujumbura nchini Burundi hadi ncha ya kusini iliyoko Mpulungu nchini Zambia na upana wa wastani wa kilometa 50.

Ziwa Tanganyika ni la Pili kwa kina kirefu Duniani (the second deepest lake in the world) likiwa na kina cha mita 1470 likitanguliwa na Ziwa Baikal lililopo katika milima ya Siberia nchini Urusi katika mpaka wa kaskazini na Mongolia.

Ziwa Tanganyika lina ujazo mkubwa wa maji baridi (fresh water) Duniani likiwa na ujazo wa kilometa za ujazo 18,900 km³ ambazo ni sawa na 17% ya maji yote baridi duniani.

Ziwa Tanganyika lina Hifadhi mbili za Taifa katika fukwe zake za Gombe na Mahale ambazo ndizo Hifadhi pekee nchini Tanzania wanakopatikana wanyama aina ya Sokwe-mtu (Chimpanzee) wanaoishi katika mazingira yao ya asili milimani.

Ziwa Tanganyika lina zaidi ya aina 350 za samaki na wengi hupatikana katika ziwa hili tu ikiwemo mamia ya aina za samaki wa mapambo.

Ni ndani ya Ziwa Tanganyika ndiko ambako inapatikana meli kongwe zaidi ya abiria Duniani ambayo inahudumu mpaka sasa na kuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Dunia (Guinness World Book of Records) ikiwa na miaka zaidi ya 100. MV Liemba (Graf Goetzen) iliundwa nchini Ujerumani mwaka 1913 na imekuwa ikihudumu mpaka leo baina ya bandari za Kigoma (Tanzania), Kalemie (DRC) na Mpulungu (Zambia)

Miji mikubwa katika Ziwa Tanganyika ni mji Mkuu wa Bujumbura nchini Burundi, mji wa Kigoma Ujiji nchini Tanzania, mji wa Kalemie nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mji wa Mpulungu nchini Zambia.

Jina la ziwa hili "Tanganyika" (i.e the great lake spreading out like a plain) ndilo mwaka 1919 baada ya Ujerumani kushindwa vita Kuu ya   ya Dunia  (1914-1918) na kupokwa koloni lake la Afrika Mashariki (Deustcheost afrika) ndilo jina lililotumika kuliita koloni lililowekwa chini ya uangalizi wa Uingereza la Tanganyika ambalo baada ya kujipatia Uhuru wake Desemba 9, 1961 lilizaa Taifa la Tanganyika na baadae 1964 Jamuhuri ya Tanganyika na Jamuhuri ya watu wa Zanzibar ziliungana na kuzaliwa Taifa la TANZANIA ya leo.

Ukibahatika kutembelea Magharibi mwa Tanzania basi usiache kulitembelea Ziwa Tanganyika na kushuhudia mengi mazuri na ya kuvutia.

Karibu Tanzania.
Karibu SwahiliKwetu Tours

Sunday, May 27, 2018

Tahadhari kwa wanaoflash simu

Na Adimu Nihuka Jr
Unajua kuwa kuflash simu ni kosa kisheria katika nchi YETU Tanzania? Kama ulikua hujui fahamu sasa, unapoflash simu ni sawa na kubadili window katika computer kwa sababu huwa unabadili mfumo endeshi mzima na kuuweka mpya ili ufanye Kazi kwa ufanisi tofauti na mfumo uliopita.

Pia kitendo cha kuflash simu kinaendana na kuweka firmware mpya sasa hapa umakini unahitajika sana vinginevyo unaweza ukaharibu kifaa chako.

Kwa wanao flash simu uwe makini unapo flash samsung phone au simu yeyote ile  uwe makini sababu zipo version 2 carrier branded firmware au branded firmware na non-carrier branded firmware aka unbranded firmware na ikitokea ukaflash unbranded firmware ktk branded samsung device au device yeyote husika lazima ikudai unlock code na iki tokea ume flash branded firmware ktk unbranded samsung device au device yeyote jua lazima itakua locked kwa network moja ya hiyo carrier iliyo kua branded ktk firmware husika.

Mfano ume nunua tecno Cx air ambayo model ni H3713A-N-Tigo locked hii ni branded device na ina branded firmware kwa mtandao wa tigo halafu ukaflash firmware general ya cx air ambayo ni unbranded means haija lokiwa kwa mtandao wowote kuta tokea nini na hapo hapo ikatokea ukawa na cx air H3713-A-N ambayo sio beanded uka flash branded firmware ya tigo.

Mfano mwingine ni kwamba; Iwapo wewe ume nunua Tecno N2 ya tigo na mwingine aka nunua tecno N2 ya kawaida zote zikawa zina model number moja tofauti kati ya simu hizi mbili ni firmware iliyopo ambayo

1). SIMU MOJA FIRMWARE YAKE IKO CUSTOMIZED KWA MATUMIZI YA SIM CARD YA MTANDAO WA TIGO PEKEE

2).SIMU NYINGINE FIRMWARE YAKE HAINA KIZUIZI CHA SIM CARD NA KUA NI GLOBAL NA INA TUMIKA KWA SIM CARD YA MTANDAO WOWOTE

KWA MAANA HYO UNA WEZA UKA BACKUP FIRMWARE YA N2 YA TIGO NA UKA IFLASH KWA ILE YA KAWAIDA NA IKA KUBALI  VIZURI ISIPOKUA TU ITA KUJA IKIWA NA RESTRICTIONS KTK SIM CARD NA WAWEZA FLASH FIRMWARE YA ILE YA KAWAIDA KTK HYO N2 YA TIGO NA IKA KUBALI NA UKA ONDOA SIM CARD RESTRICTION ILA TU KWA MARA YA KWANZA ITA KUDAI UNLCOK CODE ILI UTUMIE MITANDAO MINGINE

Alichosema Sergio Ramos baada ya Mo Sallah kuumia

Beki wa Real Madrid ambao ni Mabigwa Wapya wa Kombe la UEFA Champions League, Sergio Ramos amesisitiza kuwa hakudhamiria kumuumiza Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah katika mchezo wa fainali uliochezwa jana
Salah alilazimika kutoka katika mchezo huo ikiwa ni baada ya dakika 30 za mchezo kufuatia kuumia bega lake kushoto alipoanguka chini alipokuwa anawania mpira na Ramos

Ramos, ambaye amelaumiwa sana na mashabiki wa soka katika mitandao ya kijamii, kupitia ukurasa wake wa Twitter amemtakia Salah kupona kwema
Aliandika "Muda mwingine mchezo wa mpira wa mguu unakuonyesha upande wake mzuri na muda mwingine upande wake mbaya. Juu ya yote sisi ni 'professionals'. Upone haraka Mo Salah"

Aidha, Daktari wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Abou El-Ela amesema kutokana na taarifa za madaktari wa Klabu ya Liverpool, Salah ameumia 'ligament' hivyo kuna uwezekano akashiriki Kombe la Dunia

Unajua kwa nini Antivirus zinablock cracked software?

Unajua kwa nini watumiaji wa cracked software zinakataa kufanyakazi kwenye computer zenye anti-virus?

Iko hivi Tunatumia Cracked versions za Software husika ambapo cracked means zime kua hacked na kuwekewa loader ambayo ni cracking software yenyewe ina execute code kwa main software na kuifanya ibypass box check au smart card check.

Kisha ina iload software husika na kuifanya ianze kufanya kazi
Sasa ikitokea una active anti virus lazima ata block ile software pamoja na visaidizi vyake kwakua ina behave kama virus sababu kuu ni kua loaders zote ni hacking tool

Ila kama ulinunua box husika ama dongle mfano Nck au miracle box uka connect box ktk pc yako na uka install box software full toka kwa miracle team  huto kua na sababu ya kudisable anti virus sababu hutumii cracked software bali ni original software.

Ikiwa na box lake ila kwakua box linauzwa bei kubwa ndio maana watu wana tumia cracked software za box au dongle mbali mbali ambazo zina kua term as virus sababu ya kuwepo kwa ike Loader pekee

Pia iko distributed freely ila zile miracle,volcano,falcnon,nck,z3x zina uzwa pamoja na box lake ambalo lina smart card ndani hvyo uki install tu software ya box husika bila kua na box software haita run sasa wale programmers wana zi hack zile software na kutengenezea loaders ambazo zitakua zina tumika kubypass box au smart card check na kuifanya software kustart bila box na hizo loaders ndizo zinazo kua blocked na kua termed as virus sababu ni hacking tool

Zinedine Zidane ni nani kwa Liverpool FC?

Na Adimu Nihuka Jr
Zinedine Zidane na Nadharia za Ashindikene na Nchimbo wa Jika.
Zinedine Zidane ni jina maarufu sana kwenye wigo wa soka. Ni jina lililojizolea umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 90 had mwanzoni mwa 2000 halafu likapoa kidogo na kulipuka tena miaka mitatu iliyopita, tena limelipuka kuliko volcano yoyote iliyowahi kutokea ulimwenguni.

Zidane ama Mfalme kama wanavyomtambua wafaransa wenzie, miguu yake ilikuwa na kila kitu kinachohitajika kwenye Soka, kimombo tungeweza kusema he was a complete player. Anapiga pass accurate, anadribble vyema, anaruka juu ile mbaya, anapiga mashuti, anamark, anachenga za maudhi yaani anakila kitu. Fainali ya kombe la dunia 1998 alitumia kichwa chake kuwaadhibu Brazil na fainali ya mwaka 2006 akatumia kichwa chake kumuadhibu Materrazi.

Nadharia ya Ashindikene kwa makabila ya kusini hutumika kumaanisha MTU asiyewezekana, yaani kwa kimombo you can't compete with him. Zidane ameshindikana, hawezekani, ni kuachwa tu afanye anachotaka. Makocha wetu hawa wooteeee tunaowasifia kwa mifumo na mbinu mbalimbali wameshindwa japo tu kulichukua Mara mbili mfululizo ukiachana na akina Wenger ambao hawajawahi japo kuligusa.

Zidane ametuonya uwanjani na sasa anatuonya akiwa kwenye bench, tunapaswa kumuunga mkono tu hakuna jinsi.
Zidane pia ni Nchimbo wa Jika. Dhana ya Nchimbo wa Jika kwa Kiyao inamaanisha Nyani dume aliyepevuka na kukomaa had akafikia hatua ya kutembea peke yake.

 Inajulikana nyani huwa na mazoea ya kutembea kwa mafungu, lakini Nchimbo wa Jika anatembea peke yake na Zidane amefikia hatua hiyo tangu akiwa mchezaji had sasa akiwa kwenye bench. Team ya taifa ya Ufaransa kwa miaka kadhaa ilijengwa kupitia yeye, Zidane alikuwa dictator uwanjani, anaiendesha timu anavyotaka.

 Angeweza kupiga ile chenga yake ya kupanda ball hata mbele ya watu watatu, angeweza kummwagia majalo Henry hata akiwa katikati ya uwanja yaani anafanya lolote. Kama alivyofanya Jana tu kamrudisha Isco bench na kumtupa Bale ground huku akiwa na maelekezo 106 ya dictator Zidane. Kilichotokea wengi tunakifahamu.

Hiki kinachofanywa na Zidane nusu yake angefanya Mourinho wetu tusingelala, angefanya Pep muda huu angekuwa anaandika barua ya kujiuzulu lakini angefanya Conte ndio ingekuwa balaa. Lakini kwa bahati nzuri aliyefanya ni MTU ambaye anamahusiano na dhahabu, anaundugu na makombe, anadamu ya mafanikio anaitwa Mfalme tangu miaka 20 iliyopita.

Wapo watakaomlaumu Ramos, wapo watakaomlaumu Karius na wapo watakaosema Sallah hakuwepo lakini mwisho wa siku mchawi ni huyu Zidane.

NB: Alichokifanya Ramos kiutawala kinaitwa Sterling by Force na MTU wa mwisho kukifanya alikuwa Komando Kipensi kwenye ile movie yake ya kutisha.

Imeandaliwa na Kindamba Namlia

Kukua kwa kiswahili Afrika Mashariki na kati

Na Adimu Nihuka Jr
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda.
Zaidi ya watu milioni 15 hutumia lugha hiyo kama lugha ya kwanza huku nchi nyengine wakitumia Kiswahili kama lugha ya pili au ya tatu.Ni lugha rasmi ya muungano wa Afrika.

KENYA
Kiswahili nchini Kenya ni lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969.Mwaka 1975 kiswahili kilianza kutumika bungeni.

Maneno ya Kiswahili yaongezwa kamusi ya Kiingereza
Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kuanzia miaka ya themanini mwishoni, takriban vyuo vikuu vyote vilivyoanzishwa na Serikali vilifundisha masomo ya Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili.

TANZANIA
Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzania na inatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa.
Watanzania washinda tuzo ya fasihi ya Kiswahili

Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu.

Vyombo mbalimbali vimeubuniwa kama Bakita, Bakiza, Takiluki, Taasisi ya Elimu, Uwavita na Ukuta. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani vilianza kusomesha Kiswahili kuanzia shahada ya kwanza, ya uzamili na uzamivu.

RWANDA
Kiswahili ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kabla mwaka 1994 , wakati wa mauaji ya kimbari lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye mji tofauti .

Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.
Mwaka wa 1976 -1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda.

UGANDA
Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo; Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima.

Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.

Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi

Wikendi hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.
Historia ya Idhaa ya Kiswahili ya

Keneth Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali zao, aidha kuwatendea uhalifu.

Cimara ameongeza kwamba sasa Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika mashariki ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi kama anavyosema tena Katibu mtendaji.

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Kiswahili kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19.Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo ,kuelekea kandokando ya mto Kongo.

Source: BBC Swahili

Saturday, May 26, 2018

Vitamin B

Na mwandishi wetu
Leo tuangalie kuhusu vitamin B :Upungufu wa vitamin B imekuwa ni tatizo kubwa sana kwa sababu vitamin B ni water soluble vitamin hivyo it disolve in water .kwa hiyo haina storage kwenye mwili hivyo mlaji anapaswa kula kila siku chakula chenye vitamin B kwa wingi.

 Na huwa inatoka mwilini kwa njia ya mkojo, haja kubwa, jasho, hivyo kufanya watu wenye kisukari wawe na hatari kubwa ya upungufu wa vitamin B, watoto, wajawazito, wanaonyonyesha.

KAZI YA VITAMIN B MWILINI  NI :
#Kusaidia mwili kufanya kazi sawasawa hasa katika mfumo wa chakula,kinga,na fahamu.

#  Huwezesha moyo na misuli kufanya kazi kwa ufanisi.

#Husaidia kutengeneza seli mpya na kukarabati seli na neva  na seli nyekundu za damu.

VYANZO VYA  VITAMIN B
 Maini, viazi, maziwa, nafaka zisizokobolewa, vyakula vya jamii ya kunde, uyoga, karanga, mayai, kuku, samaki, nyama, matikiti, parachichi, ndizi mbivu, chungwa, mboga za majani, mbegu za alizeti, maboga, korosho, na vyakula vilivyochachushwa kama togwa au mtindi.

ZIFUATAZO NI DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMIN B   MWILINI.
 @ Kunyongea na kusikia uchovu.

@ Kukosa hamu ya kula.

@ Kupungua  uzito.

@Maumivu mwilini.

@ Moyo na mfumo wa chakula kushindwa kufanyakazi vizuri.

@Mfumo wa fahamu kushindwa kufanyakazi vizuri.

@Vidonda kwenye kona  za midomo.

@ Kuharisha.

@ Magonjwa ya ngozi.

@ Kuchanganyikiwa, kukosa usingizi.

@Kuumwa  kichwa mara kwa mara.

@Upungufu wa  damu.

Kwa msaada zaidi kuhusu ulaji unaofaa wasiliana na Jehsha Health Food and Drink kwa namba 0757295056.au
 jhealth.food@gmail.com

Friday, May 25, 2018

Kikosi cha Young African VS Ruvu Shooting. Kabwili langoni

Kikosi cha Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting FC, mechi ya Ligi Kuu Bara may 25, 2018

1. Ramadhani Kabwili
2. Hassan Kessy
3. Gadiel Michael
4. Abdallah Shaibu
5. Said Juma
6. Maka Edward
7. Pius Buswita
8. Papy Tshishimbi
9. Matheo Anthony
10. Thabani Kamusoko
11. Emmanuel Martin

Kikosi cha akiba
12. Benno Kakolanya
13. Salum Hassan
14. Yusuph Seleman
15. Paul Geofrey
16. Saimon
17. Geofrey Mwashiuya
18. Baruani Akilimali

Kikosi cha Ruvu Shooting kitakachomenyana dhidi ya Yanga fc May 25, 2018

Kikosi cha Ruvu Shooting dhidi ya Yanga, mchezo wa Ligi Kuu Bara
1. Abdallah Rashid
2. George Amani
3. Yusuph Nguya
4. Hamis Kasanga
5. Rajab Zahir
6. Baraka Mtuwi
7. Abdalahrahman Mussa
8. Shaban Msala
9. Issa Kanduru
10. Fully Maganga
11. Khamis Mcha

Kikosi cha akiba
12. Bidii Hussein
13. Renatus Kisale
14. Zuberi Dabi
15. Adam Ibrahim
16. William Patrick
17. Jamal Soud
18. Ishala Juma

Thursday, May 24, 2018

Punguzo ya riba ya mikopo benki na mitego yake

Na mwandishi wetu
Hivi karibuni kuna baadhi ya taasisi za kibenki zimejinasibu kwa wananchi kuwa zimepunguza riba ya mkopo.

Baadhi ya wananchi wamefurahi na kukurupuka kwenda kukopa fedha pasipo kuwa na jicho la kidadisi kuhusu hizi riba.

Ningependa nizungumzie suala la riba (rate) na impact zake kwenye mkopo.

Kimsingi kuna rates (riba) za aina mbili: Flat rate pamoja Reducing rate/Declining balance rate.

Flat rate ikiwa 10% is equivalent to 18% Reducing rate.

Flat rate ni mfumo ambao rate charges kwenye mkopo uliokopa through the tenure, yaani kama ulikopa 5M kwa flat rate ya 11% kwa muda wa miaka 5, utachajiwa 11% ya 5M throughout 5 years regardless kwamba unarejesha monthly na principal inapungua. Ndio maana rate unaweza kuona ni ndogo lakini riba yake cumulative ni kubwa.

Reducing rate ina base kwenye principal balance mfano kama ulikopa 5M kwa 18%, rejesho la kwanza itakuwa 18% ya mkopo yaani 5M, rejesho la pili ni 18% ya principal balance baada ya kulipa rejesho la kwanza, rejesho la tatu ni 18% ya principal balanca after second installment na kuendelea.

Kwa hiyo reducing rate ina advantage zaidi kuliko flat rate.
For marketing purpose mtu anasema anatoa mikopo kwa 11% ambayo utakuta ni flat rate which is equivalent 19.8% reducing  rate.
Ni vema tunavyoenda kukopa tujue rate offered ni reducing rate or flat rate.!!

Nadhani nimeeleweka otherwise consult your financial advised

Na kama umeshaingia mkenge hakuna namna kwa sababu customer' s ignorance is of the financial institution assets

Waliofunga ramadhani wapo hatarini kupata saratani ya Tumbo

Na mwandishi wetu
Wafungaji hatarini kupata saratani ya utumbo, Daktari atoa ushauri
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Saratani Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Crispin Kahesa

Amewashauri waumini wa kiislamu katika mfungo wa Ramadhani kula chakula chepesi baada ya kufungua (Futuru) kwani humsaidia mfungaji kutopata saratani ya utumbo.

Amesema ”Kufunga ni ibada na ni jambo zuri kwa afya ya binadamu, lakini tunashauri watu kuzingatia kula vyakula vyepesi wakati wa kufungulia na si vile vigumu kwani huweza kuwasababishia matatizo ikiwamo saratani ya utumbo”. Kahesa.

Ameongezea kuwa wapo ambao hufungulia kwa kunywa maji au vyakula vya moto ni sahihi na bora zaidi kuliko wale wanaokula vyakula vigumu.

Vyakula vyepesi ni kama vile uji, chai hivyo ndivyo ambavyo tunashauri na vikiwa na moto kidogo ni vizuri kwa sababu vinalifanya tumbo lipate joto na kulishtua kwani linakuwa limekaa muda mrefu bila kupata chakula.

Amesisitiza pia chakula cha Daku kwani husaidia tumbo kutobakia tupu hadi jioni wakati wa kufuturu, amesema kuwa mtu aliyewahi kuugua vidonda vya tumbo yupo hatarani kupata saratani hiyo.

Japo inasemekana hii taarifa imenakiliwa(copy) kutoka katika moja ya vitabu vya hadithi ya mtume (S.A.W) katika uislamu.

Tunzo zitakazotolewa msimu huu VPL 2017/2018

Na Adimu Nihuka Jr
Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa Juni 23, ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni hizi zifuatazo:

Bingwa
Mshindi wa Pili
Mshindi wa Tatu
Mshindi wa Nne
Mfungaji Bora
Timu yenye nidhamu
U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan)
Mchezaji Bora Chipukizi
Mwamuzi Bora Msaidizi
Mwamuzi Bora
Kipa Bora
Kocha Bora
Goli Bora
VPL Best Eleven
Mchezaji wa heshima

Zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.

Wednesday, May 23, 2018

Unaifahamu Hanjin Afika?

Na mwandishi wetu
Hanjini Africa ni meli kubwa ambayo hubeba bidhaa kutoka Afrika kupeleka nchi za Magharibi.

Jambo linalosikitisha, bidhaa zinazotoka Afrika kwenda nchi za Magharibi ni chache kwani wapo waafrika wachache sana serious wanaofanya hivyo.

Niambie tajiri mkubwa duniani ambaye, biashara yake kubwa ni kuuza bidhaa kutoka Afrika kwenda Ulaya.

Wengi tunaowasikia kama wajasiriamali wakubwa, kazi yao kubwa ni kuchukua bidhaa kutoka China, India, Ulaya, Marekani na kuleta Afrika.
 Hanjin Africa inapotoka Afrika kwenda Ulaya, inakuwa na bidhaa chache,

Swali: Ina maana bidhaa za Afrika hazihitajiki ulaya au wengi hatuna uthubutu?

Nchi zilizoendelea zina uhitaji wa bidhaa nyingi tu kutoka nchi zinazoendelea. Inakuaje tunabaki masikini kila inapoitwa leo?

Yanahitajika mapinduzi Afrika, hasa Tanzania. Tunahitaji watanzania watakaojaza Hanjin Africa kupeleka bidhaa kwenda nchi zilizoendelea.

Ili tuweze kukuza uchumi wa Tanzania, tunahitaji watanzania wanaoweza kupeleka bidhaa nje. Lakini lazima tujue ni bidhaa gani kutoka Afrika zinahitajika kwa sana nje.

Diaspora, na watanzania wote tunaweza kuingia katika Fursa hii.
Jambo kubwa lazima ujue ni aina gani ya bidhaa zinazohitajika sana Ulaya. Ngoja nikupe bidhaa chache, ukihitaji zaidi tutachambua na wanachama ndani ya Fursa 101.

Bidhaa hizo ni kama zifuatazo:
1. Kahawa kutoka Afrika
2. Chai kutoka Afrika.
3. Matunda Kutoka Afrika.
4.Natural skin Care products kutoka Afrika.
Nyingine tutaendelea nazo ndani ya Fursa 101.

Nina imani kuwa wajasiriamali wadogo na wa kawaida wanaweza kuingia katika Fursa hii.
Yupo mtu mmoja aliyewahi kujiunga Fursa 101, akasema nataka kuanza export ya bidhaa kwenda nje. Nikamuuliza una mtaji kiasi gani? Akajibu nina Tshs.500,000. Nikamwambia ongeza Laki tano, kisha njoo nikuelekeze. Alipoongeza laki tano, nikampeleka sokoni Temeke, Ilala na kumwonyesha bidhaa zinazohitajika Commoro.

 Nikampa contacts za watu wanaosambaza bidhaa kwenda Commoro pamoja na meli zinazosafirisha, utaratibu pia kisha nikamwambia anza hapa kwanza, kisha nitakuelekeza wapi pa kwenda baada ya kufanikiwa.

Baada ya miezi mitano, alikuja akiwa na million tano. Alinishukuru sana. Iko hivi, alianza kupeleka bidhaa za vyakula Commoro na kila mzigo anatengeneza faida mara mbili. Unajua kwanini? Kwasababu alichagua bidhaa sahihi.
Unajua kwasasa anauza bidhaa zake nchi gani?

"Start small,but think Big"

Wewe huna mtaji mkubwa, unaingia kwenye biashara ya kuuza large and heavy products kama fenicha. Siyo bidhaa nzuri kuanza kwaajili ya ku export.

Au unataka kuuza nguo ulaya, serious kweli?

Au unataka kuuza bidhaa ambazo ni fast perishable nje?

Au unauza bidhaa nje zenye profit margin ndogo, no no...

Lazima ujue bidhaa zinazohitajika kwa wingi nchi za Magharibi.

Baada ya kujua bidhaa hizo, lazima uchague business model. Zipo business model tatu, kwaajili ya ku export bidhaa kwenda nje. Haya yote naomba wanachama tuendelee kukumbushana ili tuchambue hizi business model.

Kabla ya mwaka haujaisha, tupate watanzania wanaoweza kupeleka bidhaa nje.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Ibariki Fursa 101.

Geophrey Tenganamba.
0655973248.

Sehemu nzuri ya kufanyia biashara

Na mwandishi wetu
Kipindi nilipohamia Morogoro na kuanzisha Chuo , huwa nina utaratibu huu, ikitokea nimehamia sehemu Fulani lazima nitafute sehemu ya kuabudu yaani kanisa. Nikapata kanisa moja maeneo ya kihonda. Nilimpenda sana mchungaji wa lile kanisa alikuwa na bidii sana kwani alikuwa akiwatembelea waumini wake na kuwaombea biashara zao nk.

Sasa kulikuwa na dada mmoja mzuri sana, alihamia kutoka Arusha. Akafungua duka sehemu moja changanyikeni, ina waswahili wengi. Ni sehemu pekee kibuku ilikuwa inauza pombe zake za kienyeji kwa wingi, pia ukipeleka mitumba ya bei rahisi unauza sana. Zaidi ukitaka kuuza hiyo sehemu peleka vitu feki kwa bei ya chini, utauza sana.

Sasa dada huyo, alishawishiwa na Rafiki yake ambaye ametengeneza pesa si mchezo kupitia sehemu hiyo. Dada huyo akafungua duka la urembo, vipodozi na bidhaa mbalimbali original kabisa. Ofisi yake akaweka na AC, akaweka rangi nzuri sana. Ofisi ilikuwa ina pendeza sana.

Haya sasa, huyo dada nilikutana naye kwa mara ya kwanza kanisani kwa mchungaji huyo. Huyo dada alikuwa mtoaji mzuri sana kanisani, lakini kila siku alikuwa akilia sana, hapati mauzo kabisa kwenye duka lake. Hivyo basi mchungaji wetu alikuwa na utaratibu wa kwenda kuombea biashara yake kila jumamosi. Muda mwingine mchungaji alitumia mafuta ya upako, maji ya baraka nk lakini bado mauzo ya yule dada yaliendelea kushuka sana.

Siku moja, mchungaji akasema vijana wote twendeni tukaombee biashara ya yule dada. Mimi pia nilienda, tukaongozana, tulitembea kwa miguu na nikapata nafasi ya kujua mitaa na watu wanaoishi mitaa ile. Ukweli nilipofika dukani nilifurahi sana, duka lilikuwa zuri sana sana.

Mchungaji na vijana wengine walianza kuomba sana, ukweli mimi sikuomba  nilikuwa napiga kelele tu huku naangalia bidhaa za lile duka. Baada ya maombi dada wa watu alinunua maji na juisi kwaajili yetu, kisha tukaanza kutoka.

Mimi nikabaki nyuma, nikamvuta yule dada mkono na kumsogeza pembeni nikamwambia haya:
“Acha kusumbua wachungaji , hama huu mtaa”
Akauliza
“Sikuelewi mpendwa”
Nikajibu:
“Hakuna anayeloga hii biashara yako, ukweli ni kuwa biashara yako imezungukwa na wateja wasio sahihi. Hamisha hii biashara , tafuta mtaa mwingine, huu mtaa hakuna wateja wako”
Yule dada aliniona nisiye wa kiroho, akamwambia mchungaji pia, nikaitwa na kuombewa.
Miezi mitatu baadaye, nikapokea simu alikuwa yule dada akaniuliza,

“Unajua sehemu nzuri naweza kuhamishia biashara yangu?”

Nikamwelekeza, lakini sehemu hiyo ilikuwa gharama sana. Nikamwambia, chukua hiyo sehemu hata kama ni gharama. Akahamishia biashara yake sehemu hiyo. Mimi baadaye niliondoka Morogoro na kwenda Arusha, nikiwa Arusha baada ya miaka kama miwili nikapigiwa simu na yule dada, amefungua tawi lingine la vipodozi mwanza.

Akaniambia kuwa ile sehemu aliyohamia ilimfanya akue kibiashara na kupata mwanaume wa Maisha yake, ambaye kwasasa wanasaidiana kwenye biashara. Last week nikaonana nao ambapo walinisimulia love story ambayo, mimi pia nimehusishwa kama mhusika  niliyewafanya wakutane.

Ujumbe wangu ni huu: Change your position.
Hebu fanya inventory ya wateja wako, marafiki zako waliokuzunguka na aina ya biashara.
Umeanza biashara, lazima utengeneze list kwanza ya watu wenye hela zako. Kisha andaa bidhaa ya kuwauzia ili wakupe hela yako. Ikitokea upo mtaa ambao hakuna watu wenye hela zako , hama.

Hata kama ni social media, ikitokea tangu uingie social media hakuna watu wenye uwezo wa kununua bidhaa au huduma yako, badilisha marafiki.
Ukizungukwa sana na watu ambao hawawezi kulipia bidhaa yako, kuna siku utajikuta huna uwezo wa kulipia mahitaji yako.

Ukienda kwenye networking event, tumia muda mwingi na watu wenye hela zako. Ninaposema watu wenye hela zako simaanishi matajiri wakubwa bali potential customers. Kuna watu maarufu nikikutana nao siwezi kuhangaika kukaa nao kwa muda mrefu, usishangae kunikuta nipo na mtu wa kawaida sana kwasababu huyo ni potential customer kwangu.

“Be nice to everyone but spend most of your time with  people who have your money”
NOTE: TUPO KWENYE PILOT PHASE, PAKUA APP YA FURSA 101 SHOPPING KWENYE SIMU YAKO, KISHA TOA ODA YA BIDHAA KUTOKA SHAMBANI, UTALETEWA MAHALI ULIPO, NA BAADA YA HAPO KUNA ZAWADI HASA KAMA SI MWANACHAMA FURSA 101.
Geophrey Tenganamba.
0655973248

Jifunze kufuga kuku(27)

Na Mwandishi wetu
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

Habari Rafiki, kwanza Napenda kukupongeza sana kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa masomo haya natumaini yanakuwa msaada mkubwa kwako na yafanyie ili kuhakikisha unafikia malengo yako makubwa ya maisha yako, leo nimekuandalia somo ambalo nilisha wahi kulitoka lakini kutokana na watu wengi kuomba niwaandalie mchanganuo wa ufugaji wa kuku mia moja japokuwa nimekuwa bize sana na majukumu ya kazi lakini kwa kuona umuhimu mkubwa wa wewe rafiki yangu nimeamua kukaa chini kukuandalia mchanganuo huu ambayo unalenga kukupa uelewa mzuri katika kuweka mipango yango ya bajeti katika ufugaji wa kuku.

MCHANGANUO WA UFUGAJI WA KUKU MIA

Katika ufugaji wa kuku kuna gharama za aina mbili gharama za moja kwa moja na gharama za uendeshaji,

 Tunapozungumza gharama za moja kwa moja ni zile gharama ambazo unatumia kwaajiri ya ujenzi wa banda, gharama za Vifaranga na vyombo Vya bandani hizi ni gharama za moja kwa moja au gharama za jumla.

Gharama za uendeshaji ni gharama ambazo zinahusu chakula na madawa hizi ndizo tunazoenda kuangalia siku hii ya leo.

Katika masomo yaliyopita katika sehemu ya ishirini tulijadili kwa undani kuhusu jinsi ya kuandaa mchanganuo wa ufugaji na katika upande wa chakula tulijifunza aina mbalimbali za chakula ambacho tunaweza kuwapa kuku wetu, sasa leo sina mda wakuchambua kuhusu vipimo Vya chakula cha kuku kwa mda wa kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja. Hapo juu nimekutumia somo ambalo nilieleza kuhusu mchanganuo wa vipimo ambavyo kuku wanakula kulingana na umri wao,

Kuku mmoja kifaranga kwa mda wa mwezi mmoja anakula gramu 700  hivyo kwa Vifaranga mia moja watakula gram 70000 ambazo nisawa na kilo 70,

Hivyo kwa mda wa mwezi mmoja kuku wetu watakuwa wametumia chakula kilo 70, ambacho  tukiweka kwenye hesabu za kifedha tutapata kama ifuatavyo.


*CHAKULA CHA KUNUNUA MOJA KWA MOJA DUKANI*

πŸ‘‰kwa bei ya wastani ya chakula cha kuku kwa maeneo mengi ya nchi yetu huzwa kati ya 45,000 hadi 62,000 chakula cha kilo 50, hivyo katika mchanganuo wetu tutatumia Elfu hamsini (50,000) japo wewe Rafiki unaweza kuweka bei kulingana na maeneo yako. Ikiwa chakula cha kuku kwa mfuko tutanunua kwa 50,000  Basi kilo mmoja nisawa na 1000.

πŸ‘‰Sasa Basi tukija kwenye hesabu zetu za kuku ambapo kwa kuku mia moja tulipata kujua kuwa wanakula kilo 70. Kwada wa mwezi mmoja tukiweka kwenye hesabu zakifedha tutapata 70,000.

Hivyo tunahitimish kwa kusema kuwa kwa kuku mia watumia gharama ya 70,000 kwa mda wa mwezi mmoja. Bei hii kama chakula tutanunua moja kwa moja dukani,

*CHAKULA CHA KUTENGENEZA WEWE MWENYEWE

Katika masomo yaliyopita tulijifunza jinsi yakutengeneza chakula cha kuku kulingana na umri wa kuku ambao wanao pia nilieleza kwa undani faida za kutengeneza chakula cha  kuku, kwakuwa mambo yote hayo nilisha yaeleza katika masomo yaliyopita leo sina haja yakuyaeleza tena. Ili kuweza kutengeneza chakula cha kuku rejea katika masomo yaliyopita ili nimeeleza kwaundani zaidi jinsi ya kutengeneza chakula. Leo ninakupa mahesabu tu ambayo kama utaenda kutengeneza chakula cha kuku wewe mwenyewe.

πŸ‘‰ukirejea katika mchanganuo wetu wa chakula cha kuku wa Mda wa mwezi mmoja nilieleza michanganuo mbalimbali sasa chukua ule mchanganuo wa DEBE 12 ambao ndio nitakao utumia hapa leo.

πŸ‘‰grama za michanganyiko wa chakula ni 57000
πŸ‘‰pumba debe 6 tukiweka katika thamani ya Pesa debe moja huuzwa 1000 hadi 2000 sasa sisi tutatumia bei ya jumla ambayo kwa maeneo mengi huuzwa hivyo ni 2000, hivyo tukizidisha kwa debe sita tutapata 12,000
πŸ‘‰mahindi ya kupalaza kilo 70, kwa bei ya mahindi kwa sasa kilo moja nikati ya 250 hadi 500, sasa sisi tuweke 400 hivyo tukizidisha kwa kilo 70 tutapata 28,000
πŸ‘‰mashine utapalaza kwa 2000
Jumla ya chakula chetu ni 99000

πŸ‘‰jumla ya gharama zote za kutengeneza chakula ni 99,000 Tsh.
πŸ‘‰mchanganyiko huo utatoa jumla ya chakula kilo 178.
πŸ‘‰hiki ni kiasi cha wastani kwasababu pumba nimeweka debe moja utapata kilo 10 kwa wastani kulingana na upimaji wa pumba kwa maeneo mengi ila ukipima pumba vizuri debe moja utapata kilo 11 hadi kilo 13 ila sisi tumeweka kipimo cha wastani ambacho ni kilo 10.
πŸ‘‰ili kupata bei halisia ya chakula hiki kwa kipimo chakilo tutachukua gharama ya Pesa tuliyotumia ambayo ni 99,000  tutagawanya wa kilo 178 zilizopatikana tutapata bei ya kilo ni 556 Tsh.
πŸ‘‰kwa mahesabu tukadilia 600 ili iwe hesabu nzuri ambayo tutakuwa tunaitumia mala zote.
πŸ‘‰kwa kifupi katika eneo hili nihitimishe kwa kusema kuwa chakula cha kutengeneza mwenyewe kina gharimu 600 kwa kilo.
πŸ‘‰kwa chakula cha kutengeneza kitagharimu  42,000/= tu.

*MWEZI WA PILI
Vifaranga Vya miezi miwili mia moja wanakula chuakula kilo 123

πŸ‘‰Kama tutanunua dukani kitatugharimu 123,000 Tsh.73800 hivyo kwa wastani tuweke 74000Tsh.

πŸ‘‰Tukitumia sayansi ya kutengeneza Hydroponic fodder na Azolla tutatumia jumla ya 50000

*MUHIMU
Ninaposema kutumia sayansi simaanishi unatumia Azolla na hydroponic fodder peke yake Bali ninachomaanisha nikwamba utawapa chuakula cha kutengeneza dukani na pia utatumia Hydroponic fodder na Azolla kama chukula cha ziada na siyo chakula hicho tu.

πŸ‘‰unachotakiwa kufanya ni kuwa kama kuku wako ni mia moja ambao kwa wastani wanakula kilo 130 kwa siku sasa wewe utakaye wapa Azolla na  hydroponic dodder utawapa kilo nane hadi kumitu na hizo zilizobaki utawapa hydroponic na Azolla hiki cha ziada hakikisha hakipungui kilo nane.
πŸ‘‰kilo hizo nane kwa hydroponic utahitaji nusu kilo tu ya ngano na Azolla utahutaji eneo la meta mbili kwa tatu. Kiasi mbacho utatumia kuzalisha chakula hiki hakizidi 1000Tsh.

*MWEZI WA TATU
Kwa kuku mia kwa mwezi WA tatu watakula chakula kilo 173.6

πŸ‘«πŸ‘‰kama tutanunua dukani tutatumia 173600Tsh,
πŸ‘‰kama tutatengeneza wenyewe tutatumia jumla ya 104000Tsh.
πŸ‘‰kama tutatumia sayansi tutatumia jumla ya 7000Tsh.

*MWEZI WA NNE
Kuku mia wanakula chakula kilo 217

πŸ‘‰kama tutanunua chakula dukani tutatumia gharama ya 217,000Tsh.
πŸ‘‰kama tutatengeneza chakula tutatumia gharama ya 130000Tsh.
πŸ‘‰kwa kutumia sayansi 90,000Tsh.

*MWEZI WA TANO
Kuku mia wanakula chakula kilo 271.6 kwa mda wa mwezi mzima.

πŸ‘‰chakula cha kununua dukani kitagharimu 271600

πŸ‘‰Chakula cha kutengeza kitagharamu 163000Tsh

πŸ‘‰kwa kutumia sayansi 100,000Tsh

*MWEZI WA SITA
Kuku kwa mwezi WA sita wote watatumia chakula kilo 343

πŸ‘‰kama utanunua dukani utatumia 343,000/=
πŸ‘‰kama utatengeneza mwenyewe utatumia 206000Tsh.
πŸ‘‰kama utatumia sayansi utatumia 150,000Tsh.

*MWEZI WA SABA
Kuku mia kwa mda wa mwezi WA sita wote watakula kilo 403.
πŸ‘‰kama utanunua chakula dukani kitakugharimu 403000Tsh.
πŸ‘‰kama chakula utatengeneza kitakugharimu 242000Tsh.
πŸ‘‰kama utatumia sayansi kitakugharimu 180,000Tsh.

*MWEZI WA NANE
Kuku mia kwa mwezi wa nane wote watatumia chakula kilo 403

πŸ‘‰kwa chakula cha dukani itatugharimu 403000Tsh.
πŸ‘‰kwa chakula cha kutengeneza kitagharimu 242,000Tsh.
πŸ‘‰kama utatumia sayansi itakugharimu 180,000

 Baada ya kuangalia gharama ya chakula kwa mda wa miezi nane kwa mda wa mwezi mmoja mmjoa sasa twende tukajumlishe ili tupate hesabu ya jumla kwa upande wa gharama za uendeshaji.

πŸ‘‰kabla ya kuangalia gharama za jumla tuongeze gharama za chanjo na tiba kwa kuku wetu,

Kwa mda wa miezi nane kuku wanatumia gharama ya 137500 hii ni kwaajiri ya chanjo na madawa kwaajiri ya vitamini na kuuwa wadudu. Sasa katika ufugaji wa kuku nimuhimu kuwa na Pesa ya dharula hii utaitumia lape kuku wako watakapo ugua na katika mchanganuo wetu tunaweka 100,000Tsh. Hivyo jumla ya Pesa kwaajiri ya tiba na chanjo ni 237500Tsh.

✍Baada ya kuona mchanganuo huo sasa twende tukahitimishe jumla ya mchanganuo wa gharama za uendeshaji kwa kuku mia, tutachukua gharama za chakula tutajumlisha na gharama za madawa.

✍Kwa chakula cha kununua dukani ni  2004000+ gharama za madawa kwamaana ya tiba, chanjo na dharula kwa ujumla wake tukaweka 237500=2241500

✍kwa chakula cha kutengeneza 1203000+237500=1440500Tsh.
πŸ‘‰kwa kutumia sayansi 866000+237500= 1103500Tsh.

πŸ‘‰hapa nimefika mwisho kwa somo la Leo natumaini mchanganuo huu utakusidia sana katika kuweka mipango yako sawa kabla ya kuingia  katika ufugaji
πŸ‘‰Mchanganuo huu unaweza kutumia kwa idadi yeyote ya kuku kwa kuongeza au kupunguza idadi ya kuku.

NI MIMI RAFIKI YAKO
FRANK MAPUNDA
UNAWEZA KUWASILIANA NAMI KWA NAMBA
0758918243/0656918243

KWA MAHITAJI YA VIFARANGA CHOTARA VINAPATIKANA POPOTE PALE ULIPO (UTAKAPOCHUKUA VIFARANGA KWETU UTAPATA NAFASI YA KUSIMAMIWA KATIKA UFIGAJI WAKO KWA KIPINDI CHOTE CHA UFUGAJI WAKO)

PIA TUNAUZA MASHINE ZA KUTOTORESHEA VIFARANGA (INCUBATOR) ZIPO ZA UMEME NA ZAFUTA YA TAA KARIBU SANA.

KITABU CHA TAJIRIKA KWA KUKU SASA KINAPATIKANA KATIKA MFUMO WA SOFT COPY

KITABU KINAUZWA KWA BEI YA 7000/=

ILI KUPATA KITABU HIKI FANYA MALIPO KWENYW NAMBA KATI YA HIZO
0758918243/0656919243
MAJINA YATATOKEA; FRANK MAPUNDA
BAADA YA KUFANYA MALIPO NITUMIE E-MAIL YAKO NAMI NITAKUTUMIA KITABU.

TUPO PAMOJA KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.

Ijue kampuni ya Mobistock

Na Adimu Nihuka Jr
Mfumo mpya wa kutumia simu yako ya mkononi unaokuwezesha kutoa huduma mbali mbali katika jamii bila ongezeko la bei na kukupatia faida kila baada ya muamala kukamilika wa kuuza.

Huduma zipatikanazo:
1. Luku
2. Vocha za kurusha za (airtel, vodacom, tigo, zantel, smart na halotel).
3. Kulipia vingamuzi (dstv, startimes, azam tv).
4. Kulipia smile internet
5. Kulipia Box office (dstv)
6. Kumnunulia mteja vifurushi ya zantel na tigo vya maongezi na internet.

Kamisheni:
Kwa kila muamala ufanyao na kukamilika utalipwa kamisheni papo hapo
1. Vocha na vifurushi 4% - 5.1%
2. Startimes 10%
3. Dstv 2%
4. Azam 1%
5. Smile 1%
6. LUKU 1%

Kuitoa Kamishen:
Utaitoa kamishen yako muda wowote ule kwa kuendelea kuuza kawaida baada ya mtaji wako kuisha pasipo kuongeza mtaji wako.

Kuweka Mtaji Katika Mobistock:
Mtaji utauweka kupitia utaratibu maalum kwa njia ya mpesa, Tigo pesa, airtel Money au Ezy Pesa kulingana na laini utakayo unganiswa nayo katika Mobistock.

Mashine Ya Mobistock:
Tunazo mashine (POS) za kuuzia Luku na huduma zingine zilizo tajwa hapo juu kwa tshs. 450,000/=, hii nashine itabaki kuwa yako, hatuitaji nyaraka zozote zile kutoka kwako, itakufikia ikiwa na mtaji tayari wa tshs. 100,000 ndani na kwa wateja wa mikoani watagharamia usafiri kuwafikia, ila kwa walioko Dar hakutokuwa na gharama yeyote ya usafiri bali kufika na kuichukua ofisini baada ya kufanya malipo hayo katika akaunti yake ya Mobistock.
Kufungwa kwa akaunti yako:
Akaunti ya wakala itafungwa endapo kama haito tumika kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo.

ILI KUSAJILIWA KUJIUNGA NA MFUMO HUU:
1. Weka mtaji wako wa tshs. 10,000 au zaidi katika akaunti yako ya simu utakayo kusajiliwa mfano. tigo pesa/ mpesa / airtel money au ezy pesa kisha tuma sms 1 yenye..
2. Jina kamili
3. Namba yako ya simu
4. Eneo ulilopo
kwenda 0755 572 777 au 0655 057 212 (namba hizi zina usajili wa id 10045761 na 10045591 zinahudumia usajili popote pale ulipo Tanzania )

Gharama za Kujiunga:
Utakatwa tshs. 500/= tuu katika mtaji ulio tuma Mobistock kwa mara ya kwanza na kiasi kinachobakia kitawekwa katika akaunti yako ya mobistock ili uanze nacho kazi.

NB: Tahadhari, usikubali kumpatia mtu pesa yoyote akuunganishe mobistock kwani huduma inatolewa "bure".

* Pesa zote zinawekwa katika akaunti ya mteja kwa utaratibu maalum wa kulipia kwa namba yetu ya kampuni 077777 iliyo sajiliwa mpesa, tigopesa na MOBISTOCK kwa ezypesa na airtel money kwa kupitia namba ya kumbukumbu ya malipo (namba yako ya uwakala ya Mobistock baada ya kusajiliwa).

Download Android application ya mobistock hapa yenye miongozo mbali mbali kwa ajili ya kumsaidia wakala.
[MEDIA=googledrive]0B1eigmszVu0-SXc1MEFBYy1YVHc[/MEDIA]

Tutembele Facebook
https://web.facebook.com/MobiStock-Tanzania-Super-Agent-152326505798917
8/
MOBISTOCK BIASHARA MKONONI *150*33#

Saturday, May 19, 2018

Mfahamu tajiri mkubwa kuwahi kutokea duniani

Na mwandishi wetu
Mansa Musa ndiye mtu tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani. Kina Bill Gates na matajiri wa dunia unaowajua hajawahi kufika rekodi ya utajiri wake. Mansa Mussa Alikuwa Mfalme Wa Mali kuanzia mwaka 1312 hadi mwaka 1337.

Alizaliwa mwaka 1280 na lipewa jina la "Mansa" likimaanisha mfalme wa wafalme, sababu alitawala ufalme mkubwa Afrika, uliojulikana kama "Malike Empire" au Mali Empire. Babu yake Mansa Musa alikuwa kaka wa Sundiata Keita ambaye alianzisha 'Mali empire'.

Anashikilia rekodi ya kuwa mtu tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani ambapo utajiri wake umetajwa kuwa dola za kimarekani bilioni 400, ambazo kina Bill Gates na hata tajiri namba moja wa sasa Jeff Bezos, hawjahi kufikia, kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg Billionaires Index

Wakati wa utawala wake alikuwa akimiliki dhahabu zenye thamani kubwa. Aliwahi kufanya safari ya kihistoria ambapo alipeleka Hija watu 60,000 kwa mpigo! na kuwasafirisha watumwa 12,000 kwa ajili ya ibada hiyo takatifu kwenye dini ya Kiislam, huku akisafiri kwa kutumia ngamia zaidi ya 100 ambao wamebeba dhahabu zenye kilo zaidi ya 100 kila mmoja.

Imeelezwa kwamba alikuwa na desturi ya kujenga misikiti kila ijumaa, na baadhi ya misikiti aliyoijenga ni pamoja na Msikiti mkubwa wa Djingareyber ambao upo mpaka leo, na umewekwa chini ya Urithi wa dunia na UNESCO.

Friday, May 18, 2018

Je, wajua kuwa kukosea ndio kufanikiwa?

Na mwandishi wetu
Siyo kila makosa ni makosa. Mengine ni makosa sahihi.

Kuna watu waliowahi kufanya makosa yaliyowafikisha sehemu sahihi.

Siyo kila maamuzi sahihi leo ni maamuzi sahihi. Kuna watu waliofanya maamuzi sahihi yaliyowafikisha sehemu isiyo sahihi.

Point yangu ni nini?

Screw It . Do it!

Wewe fanya bila kuogopa makosa. Fanya bila kuogopa watu. Fanya bila kuogopa maneno ya watu.
Muda mwingine inabidi upite njia isiyopitika ili utengeneze njia.

Njia nyingi hazikuwa njia mpaka alipopita mtu ndipo zikawa njia.

Be a pioneer.
Be a change maker.
Be a destiny helper
Be a contribution
Be a way
Be a bridge
Join fursa 101 movement and make a way for others!!

Mfahamu Abbas Maziku- Mfanyabiashara

Na Geophrey Tenganamba
Mimi ni sababu ya mafanikio yako. Wewe ni sababu ya mafanikio yangu. Kutoka fursa 101.

 Mnamfahamu dogo mmoja anaitwa Abbas Maziku? Hapa ni fursa ya ku export. Mnamfahamu huyu kijana Abbas?

 Abbas Maziku- nilikutana naye mwaka jana  Huyu kijana ni mfanyabiashara wa kimataifa. Wengi wetu tunafanya biashara za kuunga unga kwasababu hatuna roho ya uthubutu.Tunaogopa kwenda kimataifa. Sijui ni lugha.. Sijui ni shetani gani huyu.

Unajua Abbas alianza biashara mwaka gani? Alianza 2013, kwa mtaji wa Tsh.2Milioni. Alianza kwa kununua korosho, ufuta, mbaazi, choroko, mtama, alizeti, mashudu ya pamba na pilipili manga. Aliyanunua mazao hayo kidogo kidogo na kuyauza kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima pamoja na minada ya mashirika ya umma huko Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida etc. Kutoka mtaji wa 2MILIONI mpaka million 200 na zaidi. Hivi karibuni amepewa $100,000 kama grants

 Anachokifanya Abbas ananunua mazao hayo yote, anayafungasha vizuri kwa kusaidiana na vibarua kisha anaweka nembo ya kampuni yake. Baada ya hapo anapeleka sampuli katika maabara za kupima ubora wa mazao  kimataifa iitwayo SGS na ndipo hufuatia hatua ya mwisho ya usafirishaji wa mazao hayo kupitia meli za mashirika mbalimbali ikiwamo IPTL, MAERSK na nyinginezo kupeleka VIETNAM.

 Zipo taratibu nyingine  anazozifuata ikiwemo kulipia TRA, watalaamu wizara ya kilimo na ufugaji, wanasheria, maofisa usalama wa taifa nk. Hapa TBS wala TFDA hawahusiki. Hapa ukiamua kufanya utafiti wa mazao na masoko ya nje umetoka.

 Jambo moja niwaambie ndugu zangu- fursa ya ku export bidhaa nje, pamoja na fursa zote zina changamoto. Asili yetu sisi binadamu tumeumbwa kuja kupambana na changamoto. Na kuzishinda. Binadamu yeyote anayekimbia changamoto anajijengea makaburi yake mwenyewe.

Unaweza ukajiona upo salama kwasababu huja risk kufanya kitu. Nakuambia ukweli unayapoteza maisha. Abbas aliniambia, alipoanza biashara mara ya kwanza alipata hasara kubwa, baada ya kuonekana mazao yake hayakuwa kwenye kiwango kinachotakiwa. Alipoteza pesa zote alizokopa benki. Unadhani aliishia hapo? Aliendelea- mpaka alipotengeneza milioni 200.

 Mizigo inayoandaliwa kusafirishwa....

Kampuni zake ni Agromart Company Ltd na Lyone Investment . Ameweza kujenga ghorofa, anamiliki magari na anasafiri nchi mbalimbali kwenye makongamano. Labda nikuulize kwanini usijifunze kupitia mfano huu? Unadhani Abbas Maziku alizaliwa mwaka gani? 1990. Ndoto zake ni kumfikia Dewji. Hebu fikiria ni kitu gani kinachokuzuia?

Jinsi ya kupata mtaji wa Biashara

Na mwandishi wetu.
Mitaji haisubiriwi!
Ni kweli biashara inahitaji mitaji ili iweze ku scale up lakini mitaji haisubiriwi. Ukiona viwanda vya Bakhresa Industries utadhani wameshiba mitaji, la hasha wao pia wanatafuta mitaji kwa viwango vyao.

Mohamed Enterprises, viwanda vyake vilipoanza kukua alihitaji mitaji mikubwa, na kulikuwa madeni makubwa anatakiwa kulipa lakini Benki za Tanzania hazikuwa na uwezo wa kumpatia mitaji. Alihangaika sana. Yaani kiasi alichohitaji benki hazikuweza kumpatia, unadhani aliishia hapo…akaondoka kwenda South Afrika akapata mitaji ndipo alipokuja akaipeleka biashara yake juu na kuwa juu ya wengine.

Kila biashara inahitaji mtaji, wewe unayelia sijui mimi sina mtaji …usidhani wengine wana mitaji imepandwa majumbani kwao, wapo uwanjani wanatafuta. Hakuna aliyeshiba mitaji

Nisingependa kukutia moyo, kupata mitaji siyo jambo rahisi lakini inapatikana. Yeyote anayekuambia mitaji ni rahisi kupatikana mwambie akupe mtaji wake akatafute mwingine. Kupata mitaji yataka moyo. Lazima upambane kwa nguvu, kama umekaa mahali kusubiri milango ifunguke bila kutafuta utasubiri sana.
Watu wengine ni wa ajabu sana, hawatumii nguvu yoyote kupata Zaidi ya kuishia kusema hakuna mitaji.

Wengine wanasali wakisubiri kwa matumaini wakitegemea mitaji itatokea isikojulikana bila kufanya chochote.
Wakati watu hao wanasubiri wasisahau kuwa muda unazidi kuyoyoma. Mwezi mmoja unakuwa miezi sita. Miezi sita inakuwa mwaka. Mwaka unakuwa miaka mitano. Wakati muda unayoyoma kwa matumaini , ukumbuke mawazo makubwa waliyokuwa nayo, ndoto kubwa walizokuwa nazo zinazidi kuota kutu, zinapitwa na wakati na kufifia kila siku.

Maisha ya watu wengi yanapotea wakiwa wanasubiri mambo yatakuwa mazuri kwa matumaini, bila kufanya jambo. Mwezi unakatika kwa matumaini. Mwaka wa pili unakatika kwa matumaini. Miaka mitano inapotea kwa matumaini. Simaanishi usiwe na matumaini, lakini huwezi kuishi kwa kutegemea matumaini bila kufanya jambo.

Nikikutana na mtu ana wazo kubwa halafu anasubiri mtaji kwa matumaini hiyo ni horrible excuse. Ni upuuzi. Ni kupoteza Maisha. Huwezi kupata matokeo duniani bila kusababisha, lazima ufanye kitu.
Kuliko kukaa na kusubiri kwa matumaini ili mambo yatokee , kuna mambo ya kufanya.

#Vunja vunja ndoto yako na kuigawa katika vipande vipande.
Najua hujanielewa hapa. Assume biashara inahitaji mtaji wa million 50, ukikaa kusubiri kupata pesa yote Tshs.50 million kwa matumaini itakuchukua miaka.
Muda mwingine unaweza kugundua kuwa biashara yako inahitaji laki moja tu kama kianzio, ili utengeneze mazingira ya kupata Tshs.50million.

 Ukiniambia huwezi kupata laki moja kwa ndugu na marafiki siwezi kukuelewa unless umezungukwa na watu makapuku waliopitiliza, hilo nalo ni kosa la jinai.
Siyo vibaya kuwa na ndoto kubwa lakini lazima ujifunze jinsi ya kupanda ngazi moja moja, ukiwa unatembea njiani lazima ukutane na mengine ya kukupeleka mbele. Usidharau mwanzo wako mdogo.

Inawezekana unataka kulima ekari 100, lakini unaweza kuanza ekari moja ukauza na kuwaonyesha wengine faida za ekari moja, unadhani nani hatawekeza kwako?

# Badili nafasi.
Kuna ndoto nyingine si kutokana na ukosefu wa mtaji ila sehemu uliyosimama siyo. Watu uliozungukwa siyo. Mazingira uliyozungukwa, watu uliozungukwa wana nguvu sana ya kukuzuia kwenda mbele “Change your position”

# Jenga na wateja,
Wateja ni wawekezaji wakubwa wanaosahaulika. Inawezekana unawaza huna mtaji kumbe mitaji imeshikiliwa na wateja wako. Jiulize una wateja wanaoweza kukulipa in advance?

Je una wateja wanaoweza kununua Zaidi?
Je una wateja wanaoweza kuleta wateja?
Naomba kuuliza una ukaribu kiasi gani na wateja wako?
Labda nikuambie ukweli mteja ni ndugu yako. Tatizo alilonalo mteja wangu ni tatizo langu hata kama halina mahusiano na biashara yangu. Mteja ni ndugu yangu.

Kama tungekuwa tunawahudumia wateja wetu vizuri, tunaishi nao kama ndugu tusingekuwa tunahangaika kutangaza kwenye tv .
Hakuna tangazo lenye nguvu duniani kama tangazo la mteja wako kukutangazia biashara yako.

Umejenga vipi na wateja wako?
Naomba mengine tumalizie ndani ya Fursa 101…
Mimi ni sababu ya mafanikio yako. Wewe ni sababu ya mafanikio yangu.

Geophrey Tenganamba.
0655973248.

Thursday, May 17, 2018

Uhaba wa soko la mbaazi nchini

Na Adimu Nihuka Jr
Asante mwanachama Fursa 101 kwa kuja na kesi ya mbaazi, nimeisikia sana na kuifuatilia kwa ukaribu mno.
Wakulima wa Mbaazi Tanzania wanalia, wengi wamekata tamaa. Miezi michache mimi nilipigiwa sim una wakulima wawili baada ya kipindi cha TBC wakiuliza
“Ni vipi Fursa 101 itatusaidia sisi wakulima wa Mbaazi? Imagine mimi nina magunia Zaidi ya 50 yapo ndani, sina wateja. 1kg tulikuwa tunauza kuanzia Tshs.2500 mpaka Tshs 3500 leo hii sokoni wanunuzi wanataka tuuze 1kg kwa Tshs. 300 mpaka 500.

Bei hii hairudishi hata gharama ya kulima. Mbaazi zinaharikibika Mr. Fursa 101. Tuokoeni wakulima..tuokoeni… Serikali ilisema itakuja na soko kutoka India lakini tunaona kimya. Tuokoeni jamani”

Siyo mara yangu ya kwanza kupokea kesi kama hizi kutoka kwa wakulima. Tanzania ikiwa na wakulima wadogo wadogo kama hawa Zaidi ya 31 million wanapitia maumivu ya aina hii. Hawa wakulima ndiyo walio kwenye kundi la watu masikini. Inauma sana…Hii ndiyo sababu tumeanzisha Fursa 101 ili kutatua soko la wakulima na kuwakutanisha na wateja wao moja kwa moja kwa tekinolojia, Zaidi ya hapo nipo na watalaamu ili kutengeneza mfumo wa uber kwaajili ya kusafirisha bidhaa za wakulima mpaka kwa wahitaji. Ili kupunguza post-harvest loss mfumo wa mafunzo ndani ya Fursa 101 kuhusu processing ya bidhaa mbalimbali za kilimo, kila bidhaa inayotoka shambani inaweza kuwa processed au kuongezwa thamani na kuzalisha bidhaa nyingine …

Tuachane na hayo turudi kwenye mbaazi. Ni kweli Serikali ilipewa nafasi na India ya kusaini mkataba wa kupeleka Mbaazi India, lakini haikuwa na uhakika na wakulima wa Mbaazi.

 Je watazalisha kwa viwango kulingana na mkataba? The same case ya Mihogo, Serikali ilidharirika sana kwani iliingia mkataba kuwa inaweza kukidhi soko la Mihogo nadhani ni mwaka 2015, lakini hata nusu ya mkataba haikufikisha. Swali likaja je, wakulima wa mbaazi wangeweza kukidhi soko la mbaazi? Kwasababu hiyo na sababu nyingine, Serikali ilichelewa kusaini mkataba, na india walizalisha mbaazi kwa kiasi kikubwa tu.

Na Tanzania pia tukazalisha mbaazi kwa kiasi kikubwa sana, wakulima wamehangaika kupeleka mbaazi India lakini hakuna soko tena, mwishoni wameziweka zinaliwa na wadudu.

Tufanyaje sasa? Tuungane na wakulima tuanze kulia kama watoto? Au tutafute njia mbadala ya soko la ndani?

Watu wanajua kweli kuhusu mazao ya mbaazi. Waingereza wanasema protein ya mbaazi ni beyond meat. Kuna bidhaa nyingi zinaweza kuzalishwa kwa kutumia Mbaazi. Badala ya kuungana na wakulima kuanza kulia, hii ni Fursa kwa wajasiriamali.

Food suppliments nyingi zinatengenezwa kwa kutumia mbaazi. Mbaazi ni zao pekee lenye protein nyingi sana, hivyo kutumika na watalaamu wengi kuzalisha food suppliments.
Mbaazi inaweza kutumika kuzalisha chocolate, supu ya mbaazi, mbaazi inaweza kutumika kuzalisha biscuits, mikate pia ipo…mikate ya mbaazi.Unga wa mbaazi unaweza kutumika kama lishe mbalimbali.

Mbaazi ni zao linaloweza kuzalisha bidhaa nyingi sana. Kinachokosekana ni maarifa…hii ndiyo sababu inayoisukuma Fursa 101.

Hizi zote ni suppliments zilizotengenezwa kwa kutumia mbaazi.
Kuna vinywaji vya mbaazi vinaweza kutengenezwa pia…kuliko kuungana kulia na wakulima mara kumi tujifunze kiundani kuhusu bidhaa zitokanazo na mbaazi kwaajili ya soko la hapa hapa ndani japo hatutamaliza lakini tutapunguza. Kipi bora…

Welcome to Fursa 101
Geophrey Tenganamba.
0655973248.

Ijue sheria ya 20.20.20 kwa watumiaji wa computer

Na mwandishi wetu
Post hii itawalenga sana watumiaji wa computer lakini hata wale watumiaji wa smartphone ambao wapo addicted sana na simu zao yaani nkiwa namaanisha unakuta mtu karibia lisaa lizima umekodolea tu simu yako pasipo hata kugeuka kwengine.... Ebu ngoja tuangalie Tile ya hii post inahusu nini haswa.

Wote tunatambua kwamba matumizi ya computer ya muda mrefu kuna wakati haya epukiki iwe umejiajiri, umeajiriwa au hata ni mwanafunzi ni lazima utatumia computer kwa muda mrefu kwa namna moja ama nyingne.

Sasa nataka nkujuze kwamba matumizi hayo husababisha madhara mbalimbali kwenye miili yetu kuanzia kwenye macho hadi kwenye sehem nyingne za mwili kutokana na kukaa sana.

#Yatambue_matatizo_hayo
Baadhi ya matatizo au dalili zinazopatikana kwa kutumia computer muda mrefu  ni pamoja na macho kuwa yanawaka moto au kuwasha, kichwa kuuma, kutokuona vizuri na hata kuona ukungu pamoja na matatizo mengne ya muda mfupi ambayo kwa ujumla wake yamepewa jina la kitaalamu #computer_vision_syndrome.

Kwa mujibu wa mtandao wa #WebMD bado hakuna ushahidi kwamba utumiaji wa computer kwa muda mrefu basi husababisha upofu badala yake watafiti hao wamegundua matatizo mbalimbali  ambayo ndo kwa ujumla wake yakaitwa #Computer_vision_syndrome.

20.20.20
Lakini pamoja na matatizo yote hayo kuna njia ya kujilinda usipate matatizo hayo ... Njia moja ambayo ni muhimu ambayo ndio inayoshauriwa na wataalamu  wengi ni pamoja na sheria ya 20.20.20.

Sheria hiyo sio mpya bali ni sheria inayotumiwa na watu wengi sana kwa sasa japo kwa hapa maskani TZ   sidhan kama inatumika kwa upana wake na kama inavyotakiwa.

Hapo kwenye hiyo sheria najuwa bado raia bado hawajaelewa ila utaangalia picha hiyo nliopost pamoja na hii post nadhani utaelewa vema jinsi ya kufata sheria hiyo rahisi iyosaidia kutunza macho yako na kukuepusha na #computer_vision_syndrome.

#Maana_ya_sheria_ya_20.20.20
Maana yake ni kwamba endapo unaangalia computer kwa muda mrefu basi unatakiwa kupumzisha macho kila baada ya dakika 20.. Na wakati huo unapumzisha macho yako basi unayapumzisha kwa staili ya kuangalia kitu kilichopo umbali wa futi 20 kutoka mahali ulipo.. Na unatakiwa kukitazama kitu hicho kwa muda wa sekunde 20 basi hiyo ndo maana halisi ya hii sheria ya 20.20.20.

Hapa najuwa kuna raia wataanza kuhoji kwanini ni sekunde 20?..  Kwa mujibu wa tovuti ya healthline ( soma hapa kama unataka kuelewa zaidi https://www.healthline.com/health/eye-health/20-20-20-rule#definition )

Macho hutumia sekunde 20 kuweza kukamilika kikamilifu hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unafata sheria hii kikamilifu. Wataalamu mbali mbali wa maswala ya macho duniani wanashauri sana sheria hii  na kuhakikisha unaifata kikamilifu pamoja na kupumzisha macho yako  mara kwa mara haswa wale wafanyakazi wa maofisini ambao huangalia karatasi nyeupe na kisha kuangalia tena kioo cha computer.

#Mwisho
Sheria hii wame deal sana na watu wa matumizi ya computer ila binafsi Nawaingiza wale wenye matumizi ya simu kupitiliza, wale wanaopenda kuangalia movie sana kwenye pc zao na wengne wote mnaojijua ebu fateni sheria hii ili badae tusije vaa lens za ajabu machoni mwetu... Kama unapenda kuvaa zile lens kama wazovaa wazee wetu puuzieni hii.

Kama unataka kusoma zaidi kuhusu #Computer_vision_syndrome basi tembelea hyo link hapo chini kwa maana nimefupisha sana post na kwa kuzungumzia kile nlicho kilenga kwahyo yapo mengi zaidi ya wewe kujifunza ambayo cjayazungumzia.

https://www.webmd.com/eye-health/computer-vision-syndrome#1

Do you know?

The richest person in the history of earth was Mansa Musa from Mali (Black).
.
The greatest pop singer was Michael Jackson(Black).
.
The greatest footballer was Pele (Black).
.
The greatest boxer was Mahumed Ali (Black).
.
The greatest and richest golfer is Tiger Woods(Black).
.
Greatest female tennis player is Serena Williams (Black).
.
Greatest hip hop artist was 2Pac (Black).
.
Greatest philosopher was Malcom X and Martin Luther King Jr (Black).
.
The greatest Reggae artist was Bob Marley(Black).
.
Most educated president is Robert Mugabe(Black).

.The greatest President in the world Nelson Madela (black)

. The Man who directed very successfully the USA Space shuttle to moon was called "Arineitwe" a Ugandan born {mukiga} & (Black)
.
Stop thinking white people are superior than us. Black people are the most superior in this world. Start discovering the superiority in you & stop undermining yourself.

Share if you feel positive about these.

Tatizo la ajira Tanzania

*Anaandika Hamis Ndyetabula;Phd : CoICT - UDSM*

Colleagues,

Let us not misconceive the concept of self employment. Literally, at any time, there MUST be employers and employees. The entrepreneurship literature say both employers and employees MUST be entrepreneurial if the firm is to carve a competitive edge in the market. This is to therefore say, whether you are an employee or employer, u must be entrepreneurial if u want to be relevant for the organization.

My biggest problem with pple who perceive kuajiriwa negatively is that, they advocate for self employment as if everybody in this world MUST be self employed. No this is inconsistent with entrepreneurship literature and the reality. If everybody becomes self employed, who will work for them? The bottom line if we want to have a vibrant economy, everyone (employed or self employed) must be entrepreneurial.

Tusichukie kuajiriwa, tuchukie mazingira ya kazi za kuajiriwa kwenye nchi zetu masikini. Ngoja niwaambie, ngoma ya nachukia kuajiriwa ni ya kampeni ya serikali za nchi masikini kukabiliana na unemployment challenge. Usipoifahamu hii ngoma utaicheza vibaya.

 Because they have such a huge challenge that they cannot address, they come with slogans, nachukia kuajiriwa, etc.  Kibaya zaidi they equate entrepreneurship with self employment. Ndio maana wanasema entrepreneurship ifundishwe vyuoni ili eventually vijana waweze kujiajiri. From today, wale ambao hawafahamu, naomba wafahamu kwamba entrepreneurship and self employment are two different things (but may have only sporadic elements of commonality).

 Nihitimishe kwa kusema hivi:

Chuki dhidi ya dhana ya kuajiriwa inaweza kusababishwa na mambo makubwa mawili:
1. Msukumo wa nchi kwa watu wake baada ya kushindwa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira ( kwa hiyo matokeo yake ni kuwafunza watu kuchukia kuajiriwa)

2. Mazingira mabovu ya ajira (malipo duni sana, mazingira hatarishi ya kazi, ukandamizaji, kutojali afya na stahiki za mfanyakazi, kukosa ujasiriamali kwa waajiriwa n.k n.k)

Kuhusu hilo jambo la pili, nenda kasome ripoti za ILO za kila mwaka kuhusu definition ya ajira, halafu ufanye assessment  ya mtu aliyeajiriwa hapa  Tz. Utakachojifunza ni kwamba sehemu kubwa ya watu walioajiriwa wanaganga njaa tu. Wapo kwenye ajira ambazo si ajira kwa tafsiri za kitaalamu. Kwa hiyo kijana ambaye anatafuta maisha akimtazama mganga njaa anavyoishi kwa kuunga unga maisha (ingawaje aneajiriwa), lazima atasema, nachukia kuajiriwa.

Take these words from me, ukiajiriwa kwa stabdard ya definition ya ajira as per ILO, nakuhakikishia hilo neno nachukia kuajiriwa litakua msamiati.

Mfano mdogo: wachezaji wa mpira wa timu kubwa ambao wana mishahara ya bilioni moja kwa mwezi ni waajiriwa. Na usipompangia kazi (kumpanga kucheza mechi) anakasirika vibaya sana hata kama akikaa benchi atapata mshahara wake kama kawaida bado anakasirika sana. Huku nyumbani mtu akikaa bila kazi mshahara ukiwa unaingia tu anachekelea hadi jino la mwisho.

Tafakari concept yangu ya kila mtu awe mwajiri au mwajiriwa lazima awe mjasiriamali NA ujasiriamali sio sawasawa na kujiajiri; ni vitu viwili tofauti

Kama computer yako umeme unasumbua fanya hivi

Na mwandishi wetu
Power Supply Failure).
Kitendo hiki ni hali ambayo hutokea pale ambapo unajikuta Kompyuta haipokei umeme kwa ajili ya kuonesha maandishi kwenye kioo cha kompyuta.

DALILI MABLIMBALI ZINAZOONESHA KUSHINDWA KUSAMBAA KWA UMEME KWENYE KOMPYUTA.
Zipo ishara mbalimbali ambalo linadhihirisha kuwa kwa kiwango kikubwa umeme ni tatizo kwenye Kompyuta. Lakini kwa sasa tuzungumzie kwa kifupi dalili hizi;

1.Kompyuta inapowashwa hakuna kitu kinachotokea, yaani unaweka Adapter kwenye Kompyuta lakini bado haiwaki, unaisha lakini bado haioneshi dalili ya kuwaka.

2. Ukiwasha Kompyuta inawaka, na baada ya muda mfupi sana inazima na wakati huo huo umechomeka Adapter kwenye Kompyuta yako. Hii ni dalili kuwa Ubao Mama haupokei umeme wa uhakika katika utendaji wake wa kazi, kuna mapungufu.

3.Wakati mwingine wakati unaendelea kufanya kazi, huku Kompyuta umeweka Adapter, betri ni nzima na huku inaonyesha inachaji, na ghafla ikazima, hi ni dalili kuwa kuna mapungufu katika mfumo wa umeme wa Kompyuta yako.
                   
 KINACHOSABABISHA TATIZO HILI.
1.Kuwepo kwa Shoti saketi kwenye Kompyuta yako (Short Circuit), hii ni hali ambayo hutokea hasa pale ambapo saketi humwagikiwa na kimiminika(liquid), pale Kompyuta inapomwagiwa vitu kama chai, soda, maji, uji, n.k huweza kusababisha kuharibika kwa motherboard.

2.Kuwepo kwa uchafu, moshi, kwenye Ubao mama(motherboard), kama Kompyuta haifanyiwi usafi pia inaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa ubao mama.

3.Kuchemka/ kupata joto jingi kwa Kompyuta, jambo ambalo husababishwa na Kushindwa kufanya kazi kwa feni

4.Adapter (chager) ambayo haiendani na Kompyuta yako. Hapa utakuta mtu anatumia Adapter ambayo haina uwezo kwa kuwasha Kompyuta yake, hapa tunazungumzia kuwa usitumie Adapter yenye uwezo mdogo.

5.Adapter na Power cable kuwa mbovu, hii nayo inaweza kuwa sababu maana yake umeme hauingii kwenye ubao mama ili kioo kiweze kuwaka.

6.Tatizo la kimazingira, hii ni hali ambayo mara nyingi unakuta hasa kipindi cha masika vifaa vya ki-electroniki hupata ubaridi unaopelekea kusababisha kuwepo kwa hali inayosababisha hata kuungua kwa baadhi ya chip kwenye Kompyuta.

7.Kuharbika kwa Power jack. Kile kitundu ambacho Adapter inachomekwa ili ipate kuchaji kompyuta.

 JINSI YA KUTATUA TATIZO.
1.Hakikisha Power cable pamoja na Adapter vipo katika ubora yaani, kisiwepo kifaa ambacho kina tatizo. Chunguza kwa umakini, pia angalia kama kwenye chanzo cha umeme kama umeme unaingia kwenye Adapter yako.

2.Hakikisha una mazoea ya kufanya “Service” kwenye Kompyuta yako, ambapo itakupa wakati mzuri wa kutunza Kompyuta yako na kuweza kugundua baadhi ya matatizo kama “Short Circuit”, kushindwa kufanya kazi kwa feni n.k.

3.Pia unaweza kwenda kwa fundi/Technician mwenye uwezo na ujuzi wa kuitengeneza Kompyuta yako kutatua tatizo lolote hasa la Shoti kwenye Kompyuta yako.

4.Tumia Adapter ambayo inaendana na Model ya Kompyuta yako, mfano kama Kompyuta yako inatumia “Input 19.5v= 3.34A usitumie.
Adapter pungufu ya hiyo, maana wakati mwingine inaweza ikachaji lakini ikasababisha kutokea kwa tatizo la “mouse” kushidwa kutulia sehemu moja

Faida ya ulaji wa mbaazi

VIiRUTUBISHO MUHIMU VILIVYOMO KWENYE.
MBAAZI.

Vitamin B1.B9,C.

MADINI :
Manganese, phosphorus, calcium, potassium, copper, magnesium, zinc, iron.  Pia Protein

FAIDA ZA MBAAZI MWILINI.

***Inasaidia kuweka sawa pressure ya kupanda kwa sababu madini ya potassium yaliyopo yanafanya kazi ya kuzuia kukakamaa kwa misuli na kuifanya damu ipenye vizuri kwenye mishipa ya moyo. Kitaalamu tunaita (it acts as a vasodilator so it reduce the blood constriction  so that's reduces blood pressure)

****Inasaidia katika ukuaji.
Kama tulivyoona mbaazi zina uwingi wa protein na protein inasaidia katika ukuaji na maendeleo mwilini kama cells, mifupa, misuli, mishipa. Pia hutengeneza cell zilizokufa hivyo ni chakula kizuri kwa wajawazito, watoto, wanaonyonyesha na wazee. Pia huupa mwili nguvu.

***Inazuia upungufu wa damu kutokana na iron iliyopo .
Pia folate iliyopo inasaidia kuzuia mtoto kuzaliwa na ulemavu kama mgongo wazi (neural tube defects)

****Huupa mwili nguvu.
Vitamin B iliyopo inasaidia kwenye carbohydrate metabolism hivyo kuzuia mafuta mabaya kurundikana kwa sababu hiyo mwili utakuwa na nguvu.

****Husaidia kinga mwilini.
Vitamin C iliyopo inaleta afya katika chembe chembe nyeupe za damu ambazo zinafanya kazi kama antoxidant (kitoa taka mwilini) hivyo kuufanya mwili kuwa na kinga.

***Afya ya moyo.
Madini ya potassium na kiwango kidogo cha cholesterol yanasaidia kuufanya moyo kuwa na afya. Hivyo kupunguza au kuzuia magonjwa ya moyo.

****Inasaidia katika mmeng'enyo wa chakula (digestive health) yaani inazuia kupata Choo kigumu (constipation)by reducing the strain as well as inflammation.

Huo ni ufupisho tu wa faida za mbaazi lakini ziko nyingi nimejaribu kufafanua katika kiswanglish ili tuelewe wote 😁kwa kuwa terminology za afya kuzitafsiri kiswahili ni shida...

Kwa msaada zaidi kuhusu lishe na ulaji unaofaa wasiliana na Jehsha Health Food and Drink kwa namba 0757295056.au barua pepe  jhealth. food @gmail. com.

Afya yako ndio jukumu letu.

Namna ya kutatua tatizo la invalid au null IMEI katika simu za mtk

Na Adimu Nihuka Jr
Baada ya kuflash simu yako piga *#06# ili kuangalia kama IMEI ipo sahihi, kuna baadhi ya simu baada ya kuflash kwenye upande wa IMEI inakuletea invalid IMEI au null IMEI. Ukigundua tatizo hili fanya yafuatayo

Download MTK Engineering mode App kutoka playstore. Ifungue na uende kwenye option ya "MTK settings"

Baada ya hapo utaona neno la juu limeandikwa "Telephony" slide kutoka kulia kwenda kushoto utaona neno la juu limeandikwa "Connectivity" Tafuta "CDS Information" na uclick hapo Chagua "Radio Information" Chagua "Phone 1" ili kurudisha IMEI ya SIM 1

Then click neno "AT+" alafu mbele ya neno hilo andika AT+EGMR=1,7,"namba ya IMEI unayotaka Kuirudisha" au ufungua simu yako na utoe betri then copy IMEI namba pembeni ili uje uiandike kwenye command.

Mfano AT+EGMR=1,7,"358765008365495" baada ya hapo bonyeza batani iliyoandikwa "SEND AT COMMAND" kama itakubali utaambiwa " SENT OK" na kama imekataa itakuambia "SENT FAILED" kama ikikataabjaribu kuacha nafasi kati ya neno AT+ EGMR=1,7"IMEI namba" tuma tena command then back na uchague "Phone 2" Weka command hii AT+EGMR=1,10"IMEI namba ikiwa ni tofauti na IMEI ya SIM 1" then bonyeza batani ya "SEND AT COMMAND"Restart simu yako Ikiwaka piga *#06# kuangalia IMEI natumaini IMEI itarudi kama mwanzo

Note: Ubadilishaji wa IMEI ni kinyume cha sheria.

Fursa ya umeme wa jua

Na Geophrey Tenganamba
Tujikumbushe japo tuliyosoma ndani ya Fursa 101.
Bado tunaendelea...

Mimi ni sababu ya mafanikio yako. Wewe ni sababu ya mafanikio yangu!
Ndugu wanafursa 101, habari za muda huu.

Fursa 101 inajivunia kuwa baadhi ya wanaDiaspora wamechukua hatua na kuanza kuwekeza Tanzania kupitia Fursa 101. Wapo wengine walioomba kuandaliwa mpaka business plan, marketing research etc.Tunaenda mbele,

Fursa 101 inawagusa wakulima kwa kuuza bidhaa za wakulima moja kwa moja kutoka shambani mpaka nyumbani kupitia www.fursa101.co.tz tena kwa bei ya shambani. Huna haja ya kwenda buguruni tena, unatoa oda yako unaletewa mahali ulipo.  Unaweza kudownload apps za Fursa 101 pia.

 Fursa 101 inataka kukukutanisha na watu wenye njaa ya kufanikiwa kibiashara, wenye uelewa mpana kuhusu biashara, wenye maono na taasisi kubwa kubwa.

Hivyo tunahitaji uchangamfu mkubwa. Kama hujaanza biashara ndiyo muda sasa wa kuanza na chochote ulichonacho, kama una biashara ni muda muafaka wa kutuma taarifa zako, tuunganishane masoko, maarifa na taarifa kiundani kusababisha mapinduzi.

Kuna mengi yanakuja ambayo wengine mtashangaa. Nasisitiza kama una changamoto yoyote kibiashara….masoko nk. njoo Fursa 101

Ngoja tuendelee na fursa zetu. Bado tupo kwenye Fursa ya Nishati ya Jua(Solar power)
Kama nilivyosema mwanzo, kuna shida kubwa ya umeme Afrika - Tanzania

Chini ya asilimia 20 ya waafrika wana access ya umeme. Fikiria chini ya asilimia 20. Hali ya umeme vijijini ndiyo balaa. Kwa kifupi ni kuwa asilimia kubwa ya watu wanaoishi vijijini hawana access ya umeme kabisa.

Tunafanyaje sasa? Hapo sasa ndiyo umuhimu wa nishati ya jua.

Wafanyabiashara kama akina Patrick Ngowi , waligundua Fursa hii ya nishati ya umeme na kuanza kutengeneza mamilioni ya pesa mapema kabisa kukiwa asubuhi.

Yupo ndugu yangu kijijini anayesafiri kwa baiskeli kwa masaa matatu kwenda maeneo karibu na mjini kuchaji simu yake tu.

Ukifuatilia maeneo ya vijijini utagundua kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaishi maisha ya aina hiyo.

Wale waliogundua Fursa hiyo wanajitengenezea pesa vijijini wakati sisi tupo mijini tunapakana jasho kwenye daladala.

Najua sisi tunaoishi mijini tunashangaa haya. Hivi karibuni nikiwa Arusha nilikutana na vijana kutoka Dar es salaam hawajasoma, wao wanasambaza taa za solar vijijini, wanatembea kila kijiji, wanauza taa hizo za solar pamoja na chargers zake kwa jumla na reja reja. Kuna mtu mmoja kariakoo karibu na gerezani anauza kupitia vijana hao. Hao vijana wanasema kila siku wanaingiza zaidi ya Tsh.50,000 kama malipo yao kila mmoja. Hawajasoma kabisa, lakini wamejifunza sanaa ya kuuza. Wana ushawishi hatarii. Nikafikiria kama vijana hawa wanatengeneza hii hela…bosi wao anaingiza shilingi ngapi?

Fikiria tu kwa akili ya kawaida.

Jana nilianza kuwasimulia kuhusu jamaa mmoja jina lake Richard Awuor. Huyu mtu alizaliwa Kenya, Mombasa. Akiwa kama mfanyakazi wa kampuni ya Heineken, alipangiwa kikazi Tanzania kama Country manager. Alipata nafasi ya kusafiri mikoani, ukweli alishangaa sana kuona maeneo mengi hayana umeme. Siku moja akiwa Airport ilimuuma sana alipoona umeme umekatika kwa muda mrefu. Hapo ndipo wazo la kuanzisha kampuni ya nishati ya jua Cellulike ilipozaliwa katika kichwa chake.

Hilo wazo lilitokea akiwa Mtwara, Airport …alijiuliza “Inakuaje hii jamani?”

Ilikuwa mwaka 2014.
Kutokana na hilo akaamua kuungana na wenzake na kuanza kufanya utafiti. Walisafiri Mwanza, Arusha na mikoa mingine.

Waligundua maeneo mengi yenye uhitaji wa solar power. Ngoja niwaambie wanafursa 101. Unajua kwanini tulianzisha Fursa 101?

Lengo pia ni kuwa sisi kwa sisi tutasaidiana kufanya utafiti kila mkoa bila kusafiri. Mfano kuna habari nimepata kuwa kuna mkoa mmoja ndizi zinaharibika, wanatafuta njia vipi wanaweza kuzisambaza ndizi hizo maeneo yenye uhitaji au hata kuzisindika. Ndizi tunaweza kuzalisha mikate, unga, Biscuits, Chapati etc. Sasa tukifanya haya mambo kama timu..huna haja ya kwenda Kyela, bali ni kwamba mwanachama wa Kyela anaweza kukupa taarifa kuhusu hali halisi ya masoko, bidhaa mbalimbali na fursa huko mwanza.

Hiyo kitu haiwezi kutokea mpaka tujengwe kiukaribu, kwa kuwa na tamaduni ya kusaidiana sisi kwa sisi, kuwa na tabia ya kuwa sababu ya mafanikio kwa wengine. Wengi wetu ni wabinafsi, lakini kupitia Fursa 101 tabia mpya itazaliwa.

Tunaendelea, baada ya Richard na wenzake kugundua fursa hii , wakaenda Rwanda, Uganda na Kenya …ukweli waligundua gap kubwa. Kulikuwa na uhitaji wa solar power kupita maelezo. Hapo ndipo Richard alipoacha kazi na kuanzisha kampuni ya Cellulike.

Alinunua units 50 za mifumo ya solar, na kuanza kuunganisha. Wameweza kuunganisha nyumba zaidi ya 200 kwa mifumo ya solar. Na zaidi ya mifumo ya taa 508 katika maeneo ya mwanza, Kagera na mikoa mingine.

Kampuni hiyo inafanya vizuri sana na wanatengeneza mamilioni ya pesa kupitia fursa hii. Hebu fikiria Richard kutoka Kenya amegundua Fursa hii na kutajirika hapa hapa Tanzania…ni kitu gani kinatuzuia watanzania?

Mimi ninalipa deni kuwaambia ukweli…utafiti huu hautapotea bure. Nina imani wapo matajiri watakaozaliwa…kupitia haya, lakini wale wanaosoma haya kama simulizi za akina Shigongo Mungu hatawaacha salama

Tuligusia mambo kadhaa kuhusu fursa ya Nishati ya jua. Na nikatoa mfano wa Richard aliyekuja kutoka Kenya na kufanikiwa hapa hapa Tanzania tukiwa tunamuona.
Najua watu mtaniuliza…sasa Geophrey ni vipi mtu anaweza kuanza biashara hii katika Fursa ya Nishati ya jua?

Najua Fursa hii muda mwingine inahitaji mtaji mkubwa tofauti na Fursa nyingine tulizogusia, ingawa kuna Niche markets(soko maalumu) ambazo unaweza kuanza na mtaji mdogo tu kama Fursa nyingine.

Source:  Fursa 101 whatsapp group

Sanaa ya kuuza(Art of sellng)

Somo linaitwa sales....sanaa ya kuuza.

Kama huna watu wanaokuchukia

Wala watu wanaokupenda

Nashindwa kukuelewa kabisa

Dunia ya leo inawapa nafasi wapiga kelele hata kama wana Ujinga wa  kuonyesha na kuwatupilia mbali wakimya hata kama wana mazuri ya kuonyesha.

Kuna  kauli ya kiingereza inasema hivi, “I don’t care if you love me or hate me but shame on me if you don’t know me"

Mimi sijali kama unanipenda au unanichukia ila ni aibu kubwa ya milenia kama hunijui.

Unaweza ukawa na bidhaa nzuri sana. Unaweza ukawa na mawazo yaliyoshiba. Na usipate wateja wala watu wa kukusapoti.

Dunia ya leo ni dunia yenye kelele nyingi ukijifanya mkimya na kujiamini kuwa eti vizuri vyajiuza vibaya vyajitembeza,  utakula majani

Utachemka mazima.

Kuna watu wapo humu ndani hawajawahi hata kujionyesha Wanauza nini wapo kimya kama matofali. Sikia nikuambie hatua ya kwanza ya kuuza ni kutafuta massive attention.

Mnadhani kwanini nataka mikutano ya fursa 101 kila mkoa...tunatafuta attention.

Kisichojulikana hakipo hata kama ni kweli kipo.

Fedha hufuata kinachojulikana.

Money follows attention.

Kuna bidhaa nyingi nzuri sana zimewahi kuanzishwa na zikafa unajua kwanini?

Attention

Kuna wasanii wengi wamewahi kuja na kupotea unajua kwanini?

Attention.

Kisichojulikana hakipo hata kama ni kweli kipo

Ili kuhakikisha unapata kujulikana...yaani kupata attention kuna mambo makuu mawili.

 1. Upo tayari kufanya kituko kinachovuka mipaka kiasi gani ili ujulikane?

2. Upo tayari kuendelea kufanya kwa kurudia na kuendelea kufanya vituko hivyo kwa muda gani ili uendelee kupata attention hiyo?

Waandishi wa habari watakufuata wewe

Watu watakuona wewe.

Of course kuna watu watakereka kweli...shida ni kwamba wangapi humu wanafanya vitu vya kusababisha attention??

Kama hakuna macho yanayokuangalia sahau kuuza. Hata kama una bidhaa nzuri kumzidi Bakhresa....

Kuna watu wenye bidhaa mbaya mbaya wanauza kama kawaida ...unajua kwanini??

Najua wengi tunashindwa kuvuka mipaka fulani ya kupata attention kwasababu tunaogopa watu watatuchukuliaje??????

Sikia nikuambie soko halitakupa nafasi kabisa kama ukijifanya unaplay safe.

Kuwa kichaa.....tafuta attention.

Najua wengi tunashindwa kuvuka mipaka fulani ya kupata attention kwasababu tunaogopa watu watatuchukuliaje??????

Sikia nikuambie soko halitakupa nafasi kabisa kama ukijifanya unaplay safe.

Kuwa kichaa.....tafuta attention.

Namalizia kwa kiingereza hapa:

Get attention for who you are, what you know and what your business has to offer.

 Someone who isn’t afraid to get attention will push past you and leave you in the dust. Get known, your business’ survival depends on it.

Wewe ambaye una bidhaa halafu upo kimya ...unafanya dhambi kubwa sana. Wewe ambaye upo nasi muda mrefu hujawahi kusema helo unafanya dhambi kubwa zaidi.

Jionyeshe tafadhali

Kama huna watu wanaokuchukia basi ujue wewe ni mvivu sana sana

Get attention Get attention .

The marketplace doesn’t reward those who play it safe and coast under the radar.

Be on the spotlight!!

Kama hakuna watu wanaokuongelea basi ujue umelala.

Amka tupige kelele.

Toeni taarifa kuhusu fursa 101 tubadili Tanzania. Toeni taarifa kuhusu Uzuri wa Tanzania

Karibu tuungane pamoja.

Fursa 101

0655973248

Wednesday, May 16, 2018

Brand bora za viatu Afrika

Na Adimu Nihuka Jr
Tunataka ubora. Lakini tunataka tupige kelele.
Nataka kutaja brands za viatu zinazotisha Duniani kutoka Africa. Zinazalishwa Africa.

 #Brand ya kwanza ni Sole Rebels kutoka Ethiopia.

Brand hii inauzwa zaidi ya nchi 50 ikiwa ni pamoja na   USA, Canada, Japan na Switzerland.

Mnamkumbuka Bethlehem Alemu, brand hii ilianzishwa na mwanamke  2004  kwa mtaji wa chini ya Milioni 15 .....tena alichangiwa na familia yake.

Anazalisha zaidi ya bilioni 2 Tsh kwa mwaka.
Niliwasimulia historia yake. Sitaki kurudia.

#Brand ya pili ni Della kutoka Ghana.

Brand hii waliungana watu kutoka US na Ghana.
Vijana hao ni Tina Tangalakis kutoka US na Nii Addotey, kutoka Ghana. Brand hii inauzwa nchi nyingi sana duniani.

#Brand ya tatu ni  ENZI kutoka Kenya & Ethiopia.

Watu waliosababisha brand hii ni marafiki wa karibu na wa muda mrefu Christian Ward (UK), Jawad Braye (USA), Sam Imende (Kenya) na  Azariah Mengistu kutoka (Ethiopia).

Kiwanda cha brand hii kina office kubwa Ethiopia na Kenya. Mimi sijui na sisi watanzania tutaamka lini. Wanafursa 101 amkeni kumekucha.

Brand hii ina retail shops ina maduka makubwa katika nchi duniani hiyo ni pamoja na  London, Hong Kong, Paris, New York na Johannesburg.

#Brand ya nne ni Buqisi-Ruux  kutoka Kenya & Uganda.
Brand hii ilianzishwa na vijana watatu Nuba Elamin, Lynn na Tetsi Bugaari.

Maana halisi ya brand ya  Buqisi-Ruux ni “Malkia wa kijiji”
Kiwanda cha brand hii kipo Nairobi, Kenya na wana ofisi  Kampala (Uganda) , Cape Town (South Africa), na wanauza nchi mbalimbali duniani.

#Brand ya tano ni  T.T. Dalk (Nigeria)

Brand hii ilianzishwa na Temilade Osinfade. Akiwa chuo alikuwa anapenda kuchora design mbalimbali za viatu kwenye madaftari yake. Akiwa shule akaanza kutengeneza kiatu kimoja baada ya kingine. Kwasasa anauza duniani.

 #Brand ya sita ni Swaheelies (Kenya)

Tena brand hii wanatumia sana malighafi sana kutoka Tanzania, Ghana, Kenya na Nigeria.

Sana wanategemea malighafi za Tanzania. Wanakuja kuchukua malighafi hapa hapa tukiwa tunatoa macho.

Aliyesababisha brand hii ni Chania Lackey, kijana ambaye alikuwa ni mwanasheria. Mwanamke huyu. Chania huyu aliamua kuwaunganisha mafundi na watalaamu kama akina Baraka maeneo ya Kibera Nairobi.Vijana hawa wa Kibera hawakuwa na uwezo wa kulea familia zao lakini walikuwa na ujuzi huo. Mimi sijui na sisi Fursa 101 tunaamka lini. Kuna vijana wengi wenye ujuzi wa vitu vingi mitaani tumekaa kimya tunasubiri mishahara. Mungu anawaona nyie wanadamu.

#Brand ya saba ni  HTW – Heel The World (Ghana)
Nimewahi kuwasimulia kuhusu Fred Deegbe’s.

Baada ya Fred kununua kiatu cha bei ghari sana kutoka nje, akashangaa kwanini Ghana imejaa vijana wenye vipaji na uwezo wa kuzalisha viatu vizuri zaidi ya hivi?

Nini tatizo?
Akaacha kazi benki na kuanzisha brand hiyo.
Brand hii ilianzia kwenye gereji ya baba yake, Accra, Ghana. Akakusanya vijana hao wakaanza kuzalishia viatu hivyo kwao kwenye gereji.
Kwasasa anauza dunia nzima.

Najiuliza kwa akili ya kuku ina maana hatuwezi kushirikiana tukafanya kitu cha maana au ni ubinafsi tu unatutafuna watanzania jamani???

#Brand ya nane ni Haus of Hercules (Nigeria)

Brand hii ilianzishwa na kijana designer mmoja  Christopher Jeje. Brand hii alianza mwaka 2010 kwa mtaji wa 60,000Tshs.Sasa anauza kimataifa na kusikika. Hivi umesikia alianza kwa mtaji wa elfu sitini.....upo???

#Brand ya tisa ni Passport ADV (Ethiopia)
Brand hii ilianzishwa na kijana Mikhayel “MikJagga” Tesfaye mwaka 2009.

#Brand ya kumi ni  Hesey Designs (Nigeria)

Aliyesababisha brand hii ni Odiete Eseoghene, akiwa na miaka 25 miaka miwili baada ya kumaliza chuo. Huyu binti alitengeneza brand hiyo mpaka Richard Branson tajiri mkubwa akavaa...hapo ndipo alipopata umaarufu.

Sasa basi. Fursa 101 tunahitaji kuingia kwenye brand ya kumi na moja. Tunahitaji kuzalisha bidhaa humu ndani..

Hapa sisemei viatu peke yake yaani bidhaa zote.

Brand ya chai kupita chai bora izaliwe humu.

Brand ya sanitary pads

Brand ya mashine za kilimo

Brands za sabuni

Brands za nguo

Tufanyaje sasa?

Source:  Fursa 101 whatsapp na telegram group

Fursa ya chakula katika nafaka

Na Geophrey Tenganamba:
Habari mwanafamilia wa Fursa 101- Natumaini siku ya leo ni njema kwako. Bado tunaendelea fursa ya chakula katika Nafaka. Najua wengi mnatamani tuongelee kilimo cha sijui nyanya, matikiti, sijui ufugaji nk. Hayo yote yapo ndani ya Fursa ya chakula.

 Fursa hii kama nilivyosema jana itatuchukua siku kadhaa. Lakini nitahakikisha tunawapata wataalamu hasa wale wanaofanya kwa vitendo. Jana tuligusia kidogo upande wa nafaka- na mwanafamilia mmoja aliweza kueleza jinsi alivyoanzisha Jehsha Health Food Company. Bado tutaendelea kugusia hapa. Lakini kabla hatujagusia hapa ngoja tuseme kidogo kuhusu kilimo cha nafaka

Unapoingia kwenye kilimo cha nafaka- ngoja nikuambie ukweli kuhusu kajitabia fulani katika kilimo. Wakulima wengi tulionao hapa Tanzania wanapigwa(wanaonewa) kwasababu wanapoingia kwenye kilimo wanaingia bila kuwa na taarifa za kutosha. Kama wangekuwa hawapigwi nina hakika wakulima wangekuwa matajiri wakubwa Tanzania. Sasa utakapoingia kwenye kilimo- utakutana na hiyo culture.

Hiyo kitu ipo sana kwenye nafaka. Sasa unafanyaje?Tafuta taarifa za wakulima-na association mbalimbali za wakulima. Pata taarifa zote ujue unaingiaje- na unatumia  kasoro za  culture hiyo kwa faida yako.Nisiguse sana hapa kiusalama

Tunapokuja katika fursa ya ku process nafaka. Bado kuna uhitaji sana hapa hasa maeneo ya mijini. Kama ni mpenzi wa chakula- kuna fursa katika: (A) Maziwa ya soya, Tofu na Yogurt. Kwa mtaji wa Tsh. Mil. 5-30 ukiwekeza nguvu, unaweza kutengeneza faida(net profit) zaidi ya million 3 kwa mwezi. Wapo wamama wajanja wanapiga hela hapa.

 TIB Bank wanatoa mpaka mikopo yenye masharti madogo hapa ukiwa umesajili kampuni. (B)Kiwanda cha kusaga na ku package unga. Tafuta taarifa. Ukiamua kitu hata kama hukijui mwalimu atajitokeza. Unachokitafuta kinakutafuta.

Hapa kuna Rice Mill, Palm oil, Kusindika asali, Kusindika karanga, Mihogo, Miwa, hivi vyote ni viwanda vidogo unavyoweza kuanza kwa mtaji usiozidi Milioni 20. Lakini pia kuna support kubwa. Watu wanaoweka nguvu na nia hapa wanajenga uchumi mkubwa sana.

Wengine wananunua mpaka ma VX kwa fursa hizo. Kilichomfanikisha Bakhresa ni chakula- alianza kwa viwanda vidogo vidogo kama hivyo.

Nina hakika bado kuna akina Bakhresa wengi watazaliwa. Yapo makampuni Morogoro yanauza unga wa sembe ulio kuwa packaged. Wameteka soko  la Bakhresa Morogoro Katika Baadhi ya maeneo. Tafuta kwenye mtandao feed the future. Sembe yao imewekwa  virutubisho vilivyopotea kwa kukobolewa

Unajua hao wakulima wanatengeneza sh ngapi? Huwa nashindwa kuelewa kabisa- ninapokutana na msomi wa masters hana kampuni wakati mkulima wa darasa la saba anamiliki kampuni ya kusindika nafaka. Unaweza ukadhani biashara hii inahitaji mtaji mkubwa- hapana. Labda tuwasikie wakulima waliomo humu ndani watupe experience yao.

Ushuhuda wao. Meshack Maganga nina imani Unaweza kusema neno Katika kilimo na chakula. Nataka tumalize fursa ya nafaka na kusindika. Tuingie dhahabu ya kijani-  hapa ni kuanzia matunda, mboga mboga nk.

Habari wanafamilia wa Fursa 101. Natumaini siku ya leo ni njema kwenu. Bado tunaendelea kuchambua fursa Katika chakula upande wa nafaka. Kama nilivyosema mwanzo kuna fursa nyingi hapa- mfano ukiwa na kampuni unaweza kuandaa profile na barua ya utambulisho kwenye taasisi kujitambulisha kama msambazaji wa nafaka.

Hapa hata kama huna mtaji au una mtaji mdogo unafanya. Wewe unadhani jeshini wanakula nini? Mawe?  mashuleni, vyuoni, kambini, sherehe nk. Ninamjua mtu mmoja aliyeanza hivyo  anasambaza  maharagwe, mahindi, mchele,ngombe mashuleni. Ana helaa! Pesa zipo kihalali- siyo lazima uuze madawa ya kulevya.

Mahoteli makubwa- unadhani wanatoa wapi nafaka, mbogamboga, nyama nk? Utasema biashara bwana ni kujuana- huwezi kupeleka nafaka kwenye hoteli wasiokujua. Kwani wale wanaopata tender kwenye mahoteli walijuanaje? Walizaliwa tumbo moja? Ngoja nikupe siri hapa- ukitaka na wewe wakujue, tafuta tatizo lao halafu jitoe kwao. Wasaidie.

 Wanahangaika masoko- angalia vipi unaweza kuwa msaada kwao. Onyesha umuhimu wako kwao na wao watakupa tender tena kwa upendeleo. Kabla ya kuuza kitu kwa mtu  jenga undugu kwanza. Wapo wengine humu wakifika kwenye what'sapp group ni kuweka matangazo tu bila kusalimia


JENGA UNDUGU  NA WATU UNAOTEGEMEA KUWAUZIA KITU KWANZA MAMBO MENGINE YATAKUWA RAHISI

Source: Fursa 101 whatsapp group

Jifunze jinsi fursa ya elimu ilivyo

Na Geophrey Tenganamba:
Leo kwasababu ya muda naomba nianze na mifano. Fursa ya elimu ina nafasi kila sekta. Chochote unachokijua fahamu kuwa kuna mwingine yupo tayari kulipia ili kujifunza. Hiyo ni fursa ya elimu. Mfano Moses anawezs kutengeneza pesa kama trainer lakini pia kama mzalishaji wa sabuni za kisasa. Tena yeye ni rahisi kuaminika kwasbabu anafanya kwa vitendo na sabuni yake inapendwa.
So fursa ya elimu ni pana sana zaidi ya unavyofikiria.

Mnamuona huyu dada? Anatengeneza mabilioni ya pesa kupitia sweet cakes schools, sweet cakes tv...hiyo ni fursa ya Elimu

Jina anaitwa Maria Makanjuola

Alitumia nafasi ya maarifa aliyonayo kufungua shule yake na Tv show yake...najua utakuwa unajiuliza ameanza na mabilioni ya mtaji nifuatilie nitakujulisha. Hii itakusaidia sana kutumia mbinu hiyo kwenye kitu chochote unachokijua na kubadili kuwa fursa katika elimu

Kabla sijaendelea naomba nikuulize mwanafursa 101. Ni ujuzi gani unaojua kwasasa...kama upo humu ndani na huna ujuzi wowote tafuta kila njia uwe na ujuzi au utalaamu fulani.

Maria Makanjuola ni mwanadada mjanja aliyeamua kuanzisha chuo chake kupitia mtandao.

Huamini?

Ndiyo chuo kupitia mtandaoni.

Kama mnavyojua watu wengi wanahangaika wapi wakajifunze jinsi ya kutengeneza keki, mikate etc Maria akaona fursa na kuanzisha chuo cha mafunzo kupitia mtandaoni.

Nifuatilia..

Huyu mwanadada alimaliza degree yake ya sayansi ya chakula.

 Siku moja akawa anatafuta keki ya birthday ya mtoto wake. Sasa mtoto wake alikuwa na allergies nyingi za vyakula ikiwemo mayai.

Ikabidi atafute michanganyiko mbalimbali.

Akafanya tafiti mbalimbali mpaka alipoweza kumtengenezea mtoto wake keki inayofaa.

Baada ya hapo akawa mtalaamu sana wa kuzalisha keki. Alianza kupata oda makanisani bila ofisi alifanya kazi hiyo. Akajikuta yupo vizuri sana. Muda mwingine wamama wa kanisani walimuomba awafundishe jinsi ya kutengeneza ikawa kama sehemu ya kazi yake. Na safari yake ikaanzia hapo.

Baada ya kuona uhitaji wa maarifa yake akaanzisha Sweet Cake TV School.

Hiki ni chuo kikubwa sana sana cha kufundisha jinsi ya kuzalisha mikate, keki na wanafunzi wake wakimaliza kwenye chuo hicho hufahamika kama Sweet Cakers ....
Katika mafunzo yake kuna DVD , podcasts, audio na vitabu kabisa aliviandaa. Kuna watu ulaya Marekani wanatumia contents zake kujifunza.

Wale watu wanaotaka kujifunza keki pitieni kwa huyu dada mtaduwaa...ni machachariii

Alianzaje huyu mwanadada??

Alianza kwa kufungua  Facebook group, kwa jina la  Cake Business Club, April  2015  kundi likakua na kufikia watu ....25,000 ndani ya mwaka mmoka. Habari ziwafikie wale wanaofungua facebook na kupost picha wanakula makange badala ya kuweka picha za bidhaa zao Mungu anawaona.

Alifanya hivyo kwa lengo la kuwasaidia waafrika wanaopenda mapambo na kutengeneza keki.

Alikuwa anatoa hints mbalimbali na akapendwa sana kwa hilo.

 Aliwaelimisha kuanzia jinsi ya kuandaa mpaka kibiashara.

Articles zake zilianza kupendwa na kila mtu ikawa Afrika nzima sasa. Akaanza kusikika kila mtaa ndani ya mtandao.

Ndipo chuo kilipoanzia...


Ninakuuliza leo una ujuzi gani unaoweza kuutumia ikawa fursa yako ndani ya elimu??

Baada ya kupendwa sana akaamua kuanzisha sasa shule ya mtandaoni ambayo ni hii hapa (www.sweetcaketvschool.com)

Hapa unajifunza baking na jinsi ya kuendesha biashara ya baking kiundani, utawala na uongozi katika biashara hii.

Of course kuna watu wengine walikuwa wakimsafirisha na kumpeleka Marekani kwenda kufundisha tena kwa gharama kubwa, ingawa shule ya mtandao ilikuwa rahisi kwa wengi na alikuwa na wateja wengi sana.

Kutokana na Sweet Cake TV School ameanzisha Sweet Cake TV special kwaajili ya akina mama kuwaandalia watoto cakes hasa wenye allergies, pia ameanzisha Sweet Cake Magazine, na vitabu mbalimbali.

Nina hakika kwa kasi ya sasa sote tunaweza kuiga mfumo wa huyu dada kutokana na maarifa aliyoyatumia na kuanzisha chuo chake

Unaweza kumpata dada huyu kwa kumfuatilia kupitia website hii... (www.sweetcaketvschool.com)

Au mtumie email hapa :hello@sweetcaketv.com

Huwezi kujua anaweza kuwa best hako.


Page zake za facebook ni :Facebook: @sweetcaketvschool —Instagram: @sweetcaketvschool

Page ya Twitter: @sweetcaketvsch.

Au mfuatilie facebook kabisa hapa: @mariamakanjuola

Asante kwa kunisikiliza.

Cheers!!

Source:  Fursa 101 whatsapp group

Tuesday, May 15, 2018

Fahamu maana ya convenience foods industries

Na Geophrey Tenganamba:
Convenience foods Industries? Maana yake nini?
Convinience foods ni vyakula vilivyo rahisi kutayarishwa tayari kwa kula.
Inawezekana vikawa vimekaangwa au vimepikwa au vimekaushwa na kufanyiwa package vizuri..
Unajua kuna watu watatengeneza pesa kupitia biashara hii ya convenience foods?

Mnamfahamu Salbena? Mnaifahamu asali ya Salbena? Mnajua ameanzaje?
Saimon Majeni ni mfano wa kuigwa kwa wanafursa 101 walioanza ndani ya Fursa 101. Na kuanza kuonyesha njia, nimetoa mfano wa Salbena ili uweze kuelewa Convinience foods ni kitu gani?

Sasa unaweza kuanzisha kampuni ya convenience foods, yaani vyakula vilivyoongezewa thamani na mteja akinunua anaweza kula hapo hapo au akatumia dakika chache kuanda/kupika na kula.

Ni rahisi sana ku export convenience foods nje, hasa ukifanikiwa kibali. Sasa watakaoleta mapinduzi kwenye Tanzania ya viwanda ni wale walioamua kujikita katika convenience foods. Hebu jaribu kufanya tafiti utanielewa…
Kuna kampuni kadhaa nimekuwa nikizifuatilia Afrika zinazofanya vizuri sana katika convenience foods…labda nikikutajia utaweza kujifunza kwa mifano…hutatoka bure hapa…

1) Ayoola Foods, kampuni hii ipo Nigeria.
Vyakula vyao wanauza Nigeria na nje ya Nigeria…kama Ulaya, Amerika….
Vyakula vyao ni pamoja na unga wa maharage, unga wa muhogo, yam flour, na plantain flour…
Wametengeneza vyakula hivi, kiasi ambacho mteja akinunua ni rahisi kutengeneza chakula anachotaka.

2. Kampuni nyingine ya vyakula ambayo ni mpya ni Cherebut Foods.
Kampuni hii ni kutoka Kenya wanakuja kwa kasi sana hasa katika uuzaji wa vyakula vilivyosindikwa, kaangwa na kukaushwa kwaajili ya matumizi kwa watu walio busy.
Kampuni hii wanauza nafaka na vyakula vilivyokaangwa, au kukaushwa au kusindikwa katika ubora na kuuza katika supermarket mbalimbali ndani na nje ya Kenya.

Kampuni hii imeanzishwa na dada mmoja Mary Cherop Maritim, aliyekuwa secretary wa ngazi za chini sana. Wazo hili lilikuja baada ya kuona anabanwa sana kazini, na muda mwingi anakuwa kazini na kuchelewa kurudi, akafikiri ni njia ipi ya kumrahisia kupika chakula chake kwa muda mfupi..? Akaona ajifunze jinsi ya kupika au kukaanga chakula chake na kukikausha kwaajili ya kula baadaye akitoka kazini kwa kuchelewa.

Hapo ndipo alipogundua wafanyakazi wengi wanahitaji vyakula hivyo kwani wapo busy pia.Leo hii kampuni yake imekuwa kiwanda na imeajiri watu wengi tu. Bidhaa zake zimeanza kuhitajika kw asana kuliko kawaida. Anasambaza katika supermarket mbalimbali za Kenya na hivi karibuni ameanza kusambaza nje ya Kenya.

Tanzania tuna vyakula vingi sana tunavyoweza kuvibadili, kuvisindika, kupika na kuvikausha na kuwa convenience foods…kwaajili ya watu walio busy, shida inakuja wengi wetu hatuna uthubutu. Either hatuna taarifa sahihi au waoga au tumezoea kuishi ukawaida…Natumaini kupitia Fursa 101 tutaamsha viungo wengine watakaoleta mapinduzi na kutuzalishia convenience foods kwaajili ya watu walio busy.

Source: Fursa 101 whatsapp grouo